Habari Hizi ! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Habari Hizi !

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Bikra, Jun 2, 2009.

 1. Bikra

  Bikra Senior Member

  #1
  Jun 2, 2009
  Joined: May 13, 2009
  Messages: 103
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  BIBLIA inasema, "Mjinga huamini kila neno; bali mwenye busara huangalia sana aendavyo." (Mithali 14:15).

  Na Waarabu wa Yemen,ambao hapa Tanzania wanaitwa Washihiri, wana msemmo wao unaokaribiana sana kwa maana na methali hiyo. Wao wanamsema,"Ikiwa msemaji ana wazimu, msikilizaji huwa ana akili!"

  Kwa mwenye kuzingatia hataacha kugundua kuwa misemo yote hiyo miwili ina maana moja tu.. Yote inasema kuwa mtu asiamini kila analolisikia. Ni lazima kwanza ayafanyie utafiti yale yanayosemwa ajue ni ya kweli au ni ya uongo; kisha ndiyo aamue kuyakubali au kuyakataa.Asipofanya hivyo atakuwa hana tofauti na mjinga au punguani!

  Siku moja nilikuwa nimesimama sehemu fulani nikizungumza na mwenzangu mmoja. Akapita kijana mmoja wa Kihindi. Nilikuwa nikimfahamu siku nyingi. Aikuwa ni kijana mwenye kuipenda sana dini; lakini alikuwa ana tatizo la akili.

  Alipotuona, alitutolea salamu, kisha akamgeukia yule mwenzangu akamwuliza, "Habari za siku nyingi Sheikh? Mko wapi siku hizi, mbona huonekani?" Yule mwenzangu AKAMJIBU. "Habari nzuri; kwani huna habari? Siku hizi nimehamia mbinguni, sishuki isipokuwa siku za Alhamisi tu!" Kusikia hivyo yule kijana wa Kihindi ambaye ni mgonjwa wa akili aliangua kicheko, akacheka kwa sauti kubwa sana, kisha akauliza kwa kustaajabu, "Hizi ni habari kubwa! Hivyo siku hizi binadamu wanaishi mbinguni? Si ajabu hiyo?"

  Naam, kweli hiyo ni ajabu! Hakuna binadamu anayeweza kuishi huko. Juu ya maendeleo ya sayansi na teknolojia, bado mwanadamu hajaweza kuifanya mbingu kuwa maskini yake.Ndiyo maana,hata yule mgonjwa wa akili aliona vigumu kuamini yale maneno ya mwenzangu, alipomwambia kuwa yeye siku hizi amehamia mbinguni.

  Lakini jambo la ajabu ni kuwa vipi chizi aweze kuchuja habari, akaelewa zipi za kweli, azikubali,na zipi za uongo, azikatae; wakati sisi wenye akili timamu, iwe rahisi, kwetu kukubali mambo tunayoyasikia hata bila ya kuyachunguza kwanza?

  Hapa JF Utajuaeje Habari ya kweli ?
   
 2. Mnyisunura

  Mnyisunura Member

  #2
  Jun 2, 2009
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 69
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 15
  Is this a question?
  Jiulize jinsi unavyomwamini mkeo wakati hukumuoa bikra!
   
 3. Kinyambiss

  Kinyambiss JF-Expert Member

  #3
  Jun 2, 2009
  Joined: Dec 2, 2007
  Messages: 1,372
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  kwani hiyo bikra ukiitoa ndio inakuwa na cctv?lol
   
 4. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #4
  Jun 2, 2009
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,645
  Likes Received: 1,470
  Trophy Points: 280

  hahahahahah Kinyambiss.....sina mbavu
   
 5. R

  Rwabugiri JF-Expert Member

  #5
  Jun 2, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 2,777
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135

  Duu, this is JF.. well ni kumwamini tu mkuu!

  By the way, Imani ni imani, waweza amua kuamini hata uongo, alimradi umeamua kuuamini, ni wewe tu utakavo ueekeza ubongo wako kuamini unacho kiona/kisikia/kigusa.. na fahamu zingine.
   
 6. AljuniorTz

  AljuniorTz JF-Expert Member

  #6
  Jun 3, 2009
  Joined: Jan 6, 2009
  Messages: 544
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Swali la mhusika na kuoa mke bikra vinauhusiano gani na mada husika??? au ni personal attack kwa mleta mada???

  Ustaarabu hauuzwi ni kitu cha bure, kama huwezi kuchangia post, kaa kimya utaonekana ni mwenye busara zaidi.
   
 7. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #7
  Jun 3, 2009
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Jf imejaa wachambuzi na wanajua kitu cha kuamini na kutoamini Bikra. Hapa ni kisima cha wachambuzi sijapata kuona. Ndio sababu sikatizi wala kuikosa kona hii. Lakini wengi tuna akili timamu kiasi kwamba hata tusiposema au kuchangia lolote tunajua huu ni uongo na huu ni ukweli.
  Na labda niweke sawa kwamba huu mfano wako unawahusu wananchi wa danganyika yote na c jf pekee. Si unakumbuka mfano wa Busanda siku za karibuni tu?
  Ndio sababu mimi ni mmoja wa watu ambao sikuwahi kuikubali kauli mbiu/mbinu ya maisha bora kwa kila mtanzania a.k.a kujaza watu mapesa mifukoni:) maana ni sawa na kuniambia unaishi mbinguni na kuja kila alhamisi duniani. Strange technology! NI WEHU!
   
 8. M

  Mzee Kibiongo JF-Expert Member

  #8
  Jun 3, 2009
  Joined: Jun 18, 2008
  Messages: 241
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hii ni changamoto kwa wazushi
   
 9. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #9
  Jun 3, 2009
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Fafanua zaidi.
   
Loading...