Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 284,456
- 738,846
Nimecheka sana baada ya Diamond kutoa wimbo wenye maudhui ya kisiasa huku akimtaja Gwajima na ile reaction ya Gwajima kisha diamond kuomba radhi kwa unyenyekevu na woga wa dhadhiri
Sio diamond tu watu wengi maarufu viongozi na wanasiasa kwasasa ni watu wanaomgwaya mno Gwajima mzee wa single touch double manifestation.... Haogopi na hashindwi kupata habari zako za siri akikuamulia
Kila enzi na zama zake, Mtikila alitamba sana enzi ya Mwinyi na Mkapa kidogo... Lakini huyu nguvu yake ilitokana na LIBERTY DESK (weakleaks ya sasa)...hiki ndio kilikuwa chanzo chake muhimu.. Walikuja kumtelekeza baada ya kumuona anachanganya na yake.... Nguvu yake ikapungungua sana
Mwishoni mwalimu utawala wa Mkapa na kipindi chote cha kikwete aliibuka mwingine japo yeye alilenga sana mambo ya kisiasa kupitia chama cha siasa, Dr. Slaa! Huyu chanzo chake kilikuwa ikulu, na mambo yalipokuja kuvuja wote tunajua nini kilitokea
Ni kipindi hicho cha kuelekea utawala wa mwisho wa Kikwete alianza kujitokeza mtu aitwaye Gwajima kwenye ulingo wa siasa na alianza kumblast Slaa.... Gwajima alisaidia pakubwa kumaliza Slaa
Tangu hapo Gwajima akachukua rasmi mikoba yote ya Mtikila na Slaa... Ikawa sasa akitaka kuongea ujue anamlipua mtu
Mfanano wao...wote hawa watatu ni viongozi wa dini
Tofauti zao
Mtikila alikuwa na chama cha kisiasa DP, pengine na kanisa dogo ila madongo yake alitumia jukwaa la siasa na alikuwa mwanasheria mahiri
Slaa alikuwa Katibu wa chama tishio kwa utawala, akiwa katokea kwenye upadri... Huyu alitumia jukwaa la siasa kulipua mambo
Gwajima amekuwa tofauti kidogo, haweki wazi ana mrengo wa chama gani, yeye ni mhubiri maarufu na tajiri akitumia kanisa lake kama jukwaa la mifupa madongo ...kwa kuwa kwake neutral ameweza kuwateka watu wa dini na itikadi zote,...
Kanisa lake limekuwa kama sehemu muhimu ya kuzodoa wengine. Huyu chanzo chake hakijajulikana vema ana vyanzo vingi lakini vilivyoshindwa kupenya kuta za mamlaka Kama ilivyokuwa kwa watangulizi wake
Lakini vyovyote iwavyo Gwajima ni kama hybrid ya Mtikila, akiwa amejijenga zaidi kwenye jamii kupitia kanisa lake... Hiki ni kipindi chake kitapita na Pengine mrithi wake Kwa mshangao wa wengi anaweza kuwa Mange Kimambi