Stroke
JF-Expert Member
- Feb 17, 2012
- 36,982
- 45,898
Kauli za hivi karibuni za Askofu Gwajima, zinaonyesha wazi kabisa kua yeye anamalengo ya kisiasa zaidi kuliko ilivyo wajibu wake wa kuhudumia roho za watu anaowaongoza.
Sote tunafahamu kua, kiongozi wa dini analojukumu la kuhakikisha kwamba watu anaowasimamia wanakua kiroho na kimwili, lakini sana sana kiroho ambalo ndilo jukumu lake la msingi.
Katika kila jamii iliyostaarabika, kuna migawanyo ya majukumu ambayo inaheshimika na watu wote, kuna wale ambao wanalo jukumu la kuhudumia mwili, na wale wenye jukumu la kuhudumia roho. Wenye jukumu la kuhudumia mwili ni kama madaktari, waalimu na hata viongozi ambao ndio tunaowaiti wanasiasa.
Hivyo platform ya kiroho ni moja ja platform muhimu sana katika maisha ya mwanadamu kwani huongozwa na imani ambayo ni moja kati ya vitu sensitive sana kwa mwanadamu.
Maswala la kisiasa yanawahusika wake na maswala ya kiroho(imani yana wahusika wake).
Dunia hii tunayoishi, inayo mifano ya kutosha ya namna maisha ya mwanadamu yanavyoweza kuvurugwa kwa kuchanganya mambo haya mawili " Dini na Siasa", hivi ni vitu viwili vinavyofanana kwa namna fulani lakini havijawahi kuleta matokeo mazuri pale vinapowekwa pamoja.
Kazi ya Mungu inahitajika kufanyika bila kuonesha upendeleo wa wazi kwa kundi fulani lenye mrengo fulani. Ni hatari pale kiongozi wa dini anaposimama na kuzungumza kwa wazi kabisa mambo fulani ambayo yanaeleza mawazo ya watu fulani ambao wote tunatambua kua ni marafiki zake, ili kujaribu kuvuruga amani ya nchi.
Tunapata mashaka na nia nzuri kama ipo ya matamshi wa kiongozi wa dini ilhali matamshi yake yanaonekana kabisa kutolewa kwa niaba ya watu fulani.
Mara zote jamii zilizostaarabika zinawaelekeza watu wake kuchagua jambo moja na kulifanya kwa ufasaha.
Kama Gwajima ameamua kua mwanasiasa, basi aweke pembeni majoho apande jukwaani kupiga siasa. Lakini kama bado anafanya kazi ya Mungu ya kuhudumia roho za watu, sio sahihi kutumia madhabahu ya bwana kufanya siasa.