Gwajima amkubali Dk. Magufuli

singidadodoma

JF-Expert Member
Nov 11, 2013
4,394
1,536
Askofu Josephat Gwajima afunguka kuwa Rais wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Magufuli ni mpango wa Mungu ukiwa umetokea Kwa wakati na nyakati sahihi katika kuibadilisha Tanzania ili kuwafikisha watanzania katika nchi ya maziwa na asali.

Askofu Gwajima amewataka viongozi wa dini zote na waumini wote wazidi kumuombea Dkt Magufuli ili akaukamilishe mpango wa Mungu. Pia amewataka wanasiasa walioshindwa katika uchaguzi uliopita kumuunga mkono na kuacha chokochoko ili mpango wa Mungu juu ya Tanzania utimie.

Amemaliza Kwa kusema Yeye si muumini wa Mtu bali Maendeleo Ya kweli ya Taifa la Tanzania.
 
Source Ya Hbr Yako Tafadhari!! SIO Kutueleza MAONI Yako, Kwa Vile Umepewa Nafasi Ya Kutoa MAONI Yako!! WEKA CHANZO CHA HBR YAKO!!!
 
Kama ni kweli.... Basi hakuna Mungu ndani ya huyu kiumbe. Kuna upotevu wa maadili ya maono yake toka kwa Mungu mpotevu akipingana na Mungu anayehai.
Mungu wake alimwonyesha Lowasa ndiye.
Sasa amebadili kaona Magu ndie. Maajabu.
 
Asilete unafiki hapa, yeye asubiri TRA wakagonge mlango ndio atajua magufuli ni nani.
 
Askofu Josephat Gwajima afunguka kuwa Rais wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Magufuli ni mpango wa Mungu ukiwa umetokea Kwa wakati na nyakati sahihi katika kuibadilisha Tanzania ili kuwafikisha watanzania katika nchi ya maziwa na asali.

Askofu Gwajima amewataka viongozi wa dini zote na waumini wote wazidi kumuombea Dkt Magufuli ili akaukamilishe mpango wa Mungu. Pia amewataka wanasiasa walioshindwa katika uchaguzi uliopita kumuunga mkono na kuacha chokochoko ili mpango wa Mungu juu ya Tanzania utimie.

Amemaliza Kwa kusema Yeye si muumini wa Mtu bali Maendeleo Ya kweli ya Taifa la Tanzania.
Itakuwa Mungu wake kabadili mawazo!
 
Asante Ngwajima atakaye leta choko choko atatandikwa...!

Lowasa habari anayo....
 
Hapa ndipo ninapoweza jua manabii wamesahau jukumu la tafakuri sahihi za ukweli wa mustakabali wa nchi kwa mtizamo wa kiungu km ni yy kweli ktk kichwa cha habari hii we've no prophets to trust in this world bana huyu jmaa hatuhitaji kumtofautisha na siasa.
 
Kimsingi nimemkubali Gwajima. Kwanini? Anachotuambia watz ni 'jamani mi nilikosea kumpigia debe el. shetani alinijanjia lakini sasa natambua kuwa chaguo la Mungu aliye hai ni jpm.'

Kuna viongozi wengi wa dini mbalimbali ambao kwa maneno na matendo yao walikuwa upande el. Hata baada ya el kushindwa na jpm kupiga kazi ya uhakika viongozi hawa wamekaa kimya. Mmoja alifikia kusema auawe ikiwa el hatakuwa rais. Mwingine aliwaombea kansa ya damu...... nk. Wanaugulia rohoni kama si kiburi ni nini? Wanasubiri jpm ajikwae ndipo waanze kusema. Nawashauri watoke gizani na kukiri hadharani kama Gwajima kuwa jpm ndiye.

Sisi wengine ambao ni wa kambi ya jpm tuwapokee wale wote ambao walikuwa upande wa el lakini sasa wanacheza muziki wa jpm. Tusiwanange.
 
Back
Top Bottom