PreGE2025 POTOSHI Gwajima amjibu Jerry Muro na Msukuma

PreGE2025 POTOSHI Gwajima amjibu Jerry Muro na Msukuma

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Uhalisia wa taarifa hii umepindishwa ili kupotosha
Source #1
View Source #1
Wakuu nimekutana na hii sauti inadaiwa kuwa ni ya Gwajima akimjibu Msukuma na Muro.

1748334445151.png
 
Tunachokijua
Madai

Kuna kipande cha sauti kinachosambazwa katika mitandao mbalimbali ya kijamii ikielezwa kuwa ni sauti ya Askofu Josephat Gwajima akiwajibu Mbunge wa Geita vijini Joseph Kasheku Msukuma na aliyewahi kuwa mkuu wa wilaya Jerry Muro.

Sauti hiyo imeambatanishwa na grafiki yenye nembo na kufanana na Millard ayo ikidaiwa kuwa ni ya Mei 26, 2025.

Uhalisia wa madai hayo

JamiiCheck imefuatilia taarifa hiyo na kubaini kuwa inapotosha kwani si ya Mei 26, 2025 kama inavyoelezwa. Ufuatiliaji kwa njia ya maneno muhimu (keywords search) yanayosikika katika kipande hiko cha video na kujiridhisha kuwa sauti hiyo ni Julai 24, 2016.

Ufuatiliaji umebaini kuwa sauti hiyo ilichapishwa katika mtandao wa Youtube unaojulikana kama Josephat Gwajima Rudisha TV mwezi Julai 24, 2016 na hadi kufikia wakati ripoti hii inaandaliwa video hiyo ilikuwa na watizamaji zaidi ya laki moja na elfu tisini na tano.

Sauti hiyo iliambatanishwa na ujumbe katika mtandao huo ikisomeka Gwajima amjibu Makamba 24/07/2016, aidha video hiyo ina urefu wa dakika 13:55 ambapo pamoja na maneno mengine alitamka maneno ambayo yamesambazwa tena Mei 26, 2025 na kudaiwa kuwa ni ya wakati huo.

Vyanzo mbalimbali viliripoti pia tukio hilo ikiwemo Tikisa media na Global publishers kupitia tovuti zao waliripoti taarifa hiyo ikiwa na vichwa vilivyosomeka “Gwajima amjibu katibu mkuu wa zamani wa CCM Yusuf Makamba”

Taarifa hizo zilieleza kuwa Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima amemjibu katibu mkuu wa zamani wa CCM, Yusuf Makamba aliyemtuhumu kuwa ni mwongo akisema leseni yake ni ya kuendesha magari makubwa na siyo vibajaji na maguta.

Akihubiri katika kanisa lake jana, Gwajima bila kutaja jina la Makamba, alisema: “Siwezi kushughulika na vigari vidogovidogo nyie mnanifahamu, mimi nina leseni ya kuendesha semi trailer …nadhani mmenielewa,” alisema huku waumini wake wakimshangilia
Vita mbichi hili jlni jibu sahihi kabisa Kwa watu aina ya Musukuma na Jerry Muro
 
Daaaaaaaahhh.... Huyu ni One Man Army. Wanaume ndo tunapaswa kuwa hivi. Hapoi haboi. Halafu siyo mwoga. Na Mbususu anachakata. Yaani hakuna pa kumshindia kabisa.

Ameonesha dharau sana kwa Muro na Msukuma. Hawa walitaka jipatia Umaarufu kupitoa Gwajiman. Amewakataa tu kirahisi sana. Sasa wataanza kuwa wanatoa povu kila sehemu zao za wazi.

 
Gwajima amelonga.
Ajibiwe kwa hoja na VIHOJA vya VIROJA.
Mpaka sasa hakuna mbwa yyte aliyemjibu gwajima bado.
Wanabweka tu.
Wamjaribu mwijaku labda ataokoa jahazi
 
Gwajima shikilia hapo hapo mpaka vilaza wa Mama watoe haja kubwa!
 
🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣 huyo ndio Gwajima, alishindwa Bashite tena kwenye ubora wake sembuse hawa.
 
Gwaji boy kasema yeye ana leseni kubwa ya kuendesha malori, kwaiyo hawezi bishana na wenye leseni za Bajaji na Guta...km wakina msukuma.
Kwa ufupi wenye akili kwenye hili sakata wamejaa kimya Bado wanatafakari yaliyojiri...maana Gwaji boy kapiga kwenye Codes zote ni kazi kwenu kuzifungua.
 
Back
Top Bottom