Habari wana JF! Jamani tuweni makini UKIMWI upo na hauchagui mtu,hivyo tunapaswa kuchukua tahadhari kubwa. Najua kuna watu wanachukulia UKIMWI kama ugonjwa wa kawaida ila kiukweli sio wa kawaida kiasi hicho kwani ni ugonjwa unaoweza kuzima ndoto zako ilihali una uwezo wa kujikinga kirahisi zaidi. Kilichonisukuma kuandika haya ni kile nilichokishuhudia leo. Leo nilienda hospitali kwa maswala ya kijamii,bahati mbaya nilitakiwa kuonana na dokta anayehusika na ushauri nasaha, nikiwa kwenye foleni,mbele yangu kulikuwa na watu wawili ambao niligundua ni wachumba wanaotarajia kufunga ndoa karibuni hivyo waliamua kucheck afya kwanza.Niliwaza kuwa wanapoteza muda wao bure kwani walikuwa ni wazee sana,hivyo nikajua haiwezekani wakutwe na virus kwa umri walionao. Muda ukafika wa wao kuingia kwa mnasihi,kwa bahati mbaya chumba cha mnasihi hakikuwa na privacy ya kutosha hivyo nilisikia baadhi ya maongezi yao ikiwemo umri, me ana miaka 78,ke ana miaka 74. Majibu yalionesha kuwa bibi yule ana virus,maskini babu wa watu akatahayari, akataka kuondoka bila hata kuaga huku akilaumu kuwa yule bibie angemuua bure! FUNZO:UKIMWI haupimwi kwa macho,take care.