Vitendo vya watu wenye silaha (bunduki, visu na silaha nyingine) kuwaua Wamarekani wenzao vinaweza kuongezeka kama sera ya ubepari mkali inayoendeshwa Marekani haitabadilishwa. Mazingira wanayoishi wamerekani yanawachanganya (provocative) hata Wamarekani wenyewe. hii inaweza kuwa chanzo cha watu kuchanganyikiwa na kujikuta mtu akitafuta namna ya kuondokana na maisha yale. Kufanyakazi kwa muda mrefu kwa siku, upweke, kukaa sehemu moja ya Amerika kwa muda mrefu, ukosefu wa kazi, fulsa za elimu na matibabu ni vichocheo muhimu katika kuchanganyikiwa.
Vita inazopigana Marekani dunia nzima ama zinapoteza, kuacha majeraha ama kuwaweka askali na watumishi wengine mbali na ndugu na jamaa zao, hivyo familia zinaachwa zikiwa bila ya ndugu na jamaa zao muhimu sana kijamii. Wenye nafuu Marekani ni wale wenye uwezo wa kutoka nje ya marekani na kurudi angalau kila baada ya miaka 3-5 hivi. Wako wamarekani wengi ambao hawajui kama kuna maisha mengine zaidi ya Marekani, maana wao wanangalia TV, movies, CD, michezo, n.k za Kimarekani tu. Ukiwaangalia vijana wa Kimarekani utagundua kuwa wana dalili zote za kuchanganyikiwa kama vile kuvaa chupi tu na kuingia darasani ama kutembea barabarani, kuvaa nguo zilizotoboka, kuvaa viatu tofauti miguuni ama kuvaa viatu vya upande mmoja (kushoto ama kulia), kunywa pombe kupita kiasi na kutumia madawa ya kulevya hata kwa wenyewe umri mdogo, vitendo vya ushoga, n.k.
Watu wenye maisha kama haya ukiwaruhusi wamiliki silaha utategemea nini?