Candid Scope
JF-Expert Member
- Nov 8, 2010
- 11,897
- 6,933
Ndiyo madhara ya kuruhusu bangi haya, yaani wamarekani wanavuta bangi hadharani tu na polisi wanapita mitaa hiyo hiyo wala hawafanyi kitu. Yaani kuwa marekani ni kuwa kwenye risk kubwa sana. Hasa wale wamarekani weusi ni kero tupu humo mitaani. Wanaboa kweli wanapovamia kila mtu ili awape dola moja ya kuvutia bangi. Kati ya nchi ambazo huwa naona ustaarabu wao una utata, Marekani ni mojawapo....Kama umechoka kuishi si ujimalize mwenyewe tu inahusu nini kwenda kuwaua watoto wadogo chungu nzima na kuwaachia wazazi wao, ndugu na jamaa majonzi makubwa na ya muda mrefu? Halafu bunduki aliyotumia/alizotumia huyu kichaa zilikuwa ni za mama yake ambaye naye kauwawa na huyu lunatic.
hivi hawa wamarekani wana matatizo gani?? mbona wanakuwa kama vichaa!??
Hilo la obama kulia hadharani hata mimi niliona ni la kisiasa zaidi na halikuwa na mantiki kabisa. Ni upuuzi kwa kiongozi wa nchi kutoa machozi mbele za watu wanaokutegemea kwamba wewe ndiyo baba, utasimama imara na kutoa suluhisho la matatizo yanayoikabili nchi yako.itakuwaje lini? Kwa sasa hivi na miaka yote ya nyumba hakuna vitu kama hivyo kwenye "nchi zetu hizi." Marekani ndio kuna utamaduni wa bunduki, usilinganishe maembe na machungwa, Tanzania hakuna kitu hicho!
Na huyo Obama unaemzungumzia nadhani antics zake zinaweza kuwa ndio mara ya kwanza kutokea katika historia, kwa kujiliza hadharani. Kwenye matatizo tunategemea kiongozi wa "dunia huru" akija hadharani atoe masuluhusho, sio machozi!
Hilo la obama kulia hadharani hata mimi niliona ni la kisiasa zaidi na halikuwa na mantiki kabisa. Ni upuuzi kwa kiongozi wa nchi kutoa machozi mbele za watu wanaokutegemea kwamba wewe ndiyo baba, utasimama imara na kutoa suluhisho la matatizo yanayoikabili nchi yako.
Lakini kuhusu Tanzania, ni kweli haijawahi kutokea, but ni rahisi zaidi kwetu kutokea. Sema tu bahati tuliyonayo ni kwamba hatuna mateja wengi humu nchini ukilinganisha na marekani. Ile nchi ni kama ya wendawazimu. Yaani ukiwa marekani, usalama wako ni mdogo kuliko ukiwa Tanzania. Maana Tanzania utakabiliana na vibaka tu, lakini marekani unakutana na mtu anataka kukuuzia bastola, au anakuomba dola moja ya kununulia bangi huku ameshika bastola, yaani ni shida tupu.
Hata hiyo utulivu tulionao hautoshi kutuhakikishia kwamba tupo salama refer wenzetu wa Uganda walioteketea zaidi ya 30 kwa bomu. So inawezekana huku kwetu isiwe ni kwa bunduki lakini ikawa ni mabomu kama ambavyo imetokea Uganda na Kenya. Ni vema kuchukua tahadhari wakati wote.
Ninakubali kabisa mkuu. Ila nafikiri ukiwa kama baba, likitokea tatizo nyumbani kwako, watoto wakawa wanakuangalia wewe kama mbabe wa matatizo, kwa bahati mbaya wakakuona na wewe unalia nafikiri watakata tamaa kabisa. Kwa ajili tu ya kuonyesha ubaba wake, alitakiwa angalau aongee katika hali ya kuonyesha masikitiko na atoe way forward kwa ajili ya longterm solution. Matukio ya aina hii si mageni kabisa huko marekani, miaka miwili tu wanachuo waliuawa kwa style hiihii. kwahiyo ni suala la kuamua kwamba anafanya nini kahakikisha huu uhuni hautokei tena na si kutoa machozi kutafuta huruma za watu waliopoteza watoto wao. Katika hali ya kawaida, ni jukumu la serikali ya nchi kuhakikisha usalama wa kila raia ndani ya nchi. Kwa kushindwa kwake kuhakikisha usalama wa wale watoto anatakiwa ajiuzuru na si kulia.Lukolo Obama ni mwanadamu kama wewe, mara ngapi raia wa Marekani wameuwawa hajalia? Juzi balozi kauwawa huko Libya sikumbuki kumuona akilia. Kuwamaliza malaika kama wale bila sababu ni kitendo cha kinyama sana so binafsi simlaumu kwa kulia, I'm sure aliimagine kama yeye ni mmoja wa wazazi wa watoto waliopotezewa maisha. Na isitoshe kitendo cha kulia hadharani sidhani kama kinamaanisha kwamba hatua hazitachukuliwa, unaweza usilie na hatua usichukue pia. Na unaweza ukamwaga chozi na bado ukaplay part yako kama Commander in Chief.
Kaua na baba yake mzazi
aliyeua inasemekana alikuwa na ukichaa flani so haujakosea. poor kids
Right wing nuts hawakubali,wanasema guns dont kill people,people do kill people.
Lakini ukweli ni kwamba people kill people with guns.Na hivyo madhara ya kutumia assault riffles ni makubwa zaidi.
Ila tatizo lilipofikia sijui kama wata lisolve vipi,guns ni kama culture ya wamarekani.Na ukishakuwa nayo(most of them have),hutopenda mtu akunyang'anye.
ukichaa haijapita hata wiki,juzi tu kulikuwa na tukio la hivyo hivyo hapo USA.?
Bado ana sura ya kitoto kabisa. Ndiyo madhara ya kugawa silaha kama karanga ukichanganya na action movies na computer games za mauaji.