Guninita amkaanga Dk. Magufuli | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Guninita amkaanga Dk. Magufuli

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, May 18, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  May 18, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  IJUMAA, MEI 18, 2012
  NA MAREGESI PAUL, DAR ES SALAAM


  MWENYEKITI wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Dar es Salaam, John Guninita, amesema Waziri wa Ujenzi Dk. John Magufuli ana kauli za kibabe ambazo haziwezi kukubalika.

  Amesema kuwa, pamoja na kwamba Dk. Magufuli ni kiongozi wa Serikali, amekuwa akitoa kauli zisizofaa katika jamii ambapo alitolea mfano kauli ya kuwataka wananchi wapige mbizi kama hawawezi kulipa nauli mpya ya Kivuko cha Kigamboni.

  Guninita alitoa shutuma hizo mwanzoni mwa wiki Mjini Dodoma, alipokuwa akizungumza kwenye kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM.

  Chanzo chetu kilichokuwa katika kikao hicho kilisema kuwa, Guninita alisema Dk. Magufuli alitakiwa kuwaomba radhi wakazi wa Dar es Salaam kwa kuwa, kauli ya kuwataka wapige mbizi ilikuwa ni ya kejeli ambayo haiwezi kukubalika kwa namna yoyote.

  "Guninita alilazimika kumpasha Magufuli kwa sababu inaonekana hakuridhishwa na kauli alizozitoa kipindi kile wakati nauli ya Kivuko cha Kigamboni inapandishwa na wananchi wakaonyesha kulalamika.

  "Alisema viongozi wengine wa Serikali wanafanya maamuzi kwa kiburi na kwamba maamuzi mengine yanapofanywa, huwa hakuna ushirikishwaji kwa baadhi ya viongozi, bali mtu anaamua kufanya kama anavyotaka kisha anatoa kauli za kijeuri.

  "Akatolea mfano nauli ya kigamboni, akasema Magufuli alichukua uamuzi mbaya sana kupandisha nauli wakati akijua maisha ya watu ni ya shida na kibaya zaidi ni pale aliposhindwa kuwasikiliza hata wabunge wa Mkoa wa Dar es Salaam, walipoanza kulalamikia ongezeko hilo.

  "Akasema yeye alitarajia baada ya kauli ile ya Magufuli, Waziri Mkuu angemtaka awaombe radhi wananchi wa Dar es Salaam, lakini hilo halikufanyika, sasa akasema kuna haja kwa viongozi kubadilika kwa sababu kauli nyingine zinaleta taswira mbaya kwa Serikali," kilisema chanzo chetu.

  Pamoja na mashambulizi hayo, chanzo chetu kilisema Guninita alizungumzia pia msongamano wa magari katika Jiji la Dar es Salaam. Alisema msongamano huo ni kero kwa wananchi na kwamba Serikali imekuwa ikiahidi kuutatua bila utekelezaji.

  Pia chanzo hicho kilisema mwana CCM huyo aligusia uendelezaji wa Mji wa Kigamboni, ambapo alisema suala la fidia kwa wananchi limekuwa ni kero kwa sababu hawajalipwa fidia, ingawa Serikali imekuwa ikiahidi kufanya hivyo ili kuuendeleza mji huo.

  Kuhusu mfumuko wa bei, chanzo chetu kilisema kuwa, Guninita alionyesha kutoridhishwa nao na kutaka Serikali ichukue hatua za haraka kukabiliana nao kwa kuwa unawavunja moyo wananchi.

  Kikao hicho cha NEC kilimalizika mwanzoni mwa wiki hii, huku kikitawaliwa na vijembe mbalimbali kwa baadhi ya viongozi wa Serikali pamoja na viongozi wa ngazi za juu wa CCM.

  Miongoni mwa waliotoa shutuma nzito katika kikao hicho ni kada wa chama hicho, Peter Kisumo, ambaye alimshambulia Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama kwa kile alichosema kuwa kiongozi huyo ni sehemu ya chanzo cha kudhoofika kwa chama hicho.

  Kwa mujibu wa Kisumo, Mukama hana mikakati ya kukiinua chama na pia hajui kufanya tathmini kujua kama chama kimepanda hadhi au kimeshuka miongoni mwa jamii.

  Wengine walioshusha makombora ni Mwenyekiti wa CCM, Mkoa wa Shinyanga, Khamis Mgeja, ambaye alimshushia lawama Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kwamba hana sababu ya kubaki madarakani wakati baadhi ya mawaziri wameng'olewa madarakani kutokana na kushindwa kuwajibika.

  Alisema kwamba, baadhi ya mawaziri hao wametolewa kafara kwa sababu aliyetakiwa kuwajibika ni Waziri Mkuu, kwa kuwa madudu mengi yaliyofanywa na mawaziri yamefanywa akiwa madarakani.

  Sambamba na huyo, Katibu Mkuu mstaafu wa CCM, Yusuf Makamba, naye alimshutumu Waziri Mkuu na kusema mtu akiwa na shida, ni rahisi sana kuonana na Rais Jakaya Kikwete kuliko Waziri Mkuu. Katika hatua nyingine, Makamba alimrushia kombora, Katibu wa Idara ya Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, kwamba anakiua chama hicho kwa kuwa amekigeuza na kuwa kama kampuni yake binafsi.

  Wengine walioishambulia Serikali na Chama cha Mapinduzi ni Mbunge wa Mbinga Magharibi, Kapteni John Komba, Mwenyekiti wa chama hicho, Mkoa wa Arusha, Onesmo ole Nangole, Waziri wa zamani wa Maliasili na Utalii, Shamsa Mwangunga na mwanasiasa mkongwe, Kingunge Ngombale Mwiru.

   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  May 18, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Haya Magufuli amelalamikiwa kwenye Halmashauri kuu ya CCM; Kweli ana Makosa yake lakini Makosa yake Ni Madogo zaidi ya Mafanikio yake? Ukilinganisha na Mawaziri wetu wote?

  Kwenye Halmashauri Kuu hatujasikia Malalamiko binafsi ya aliyekuwa Waziri wa Fedha, au William Ngeleja? na wote matumbo yao yamejaa $$$ Ukiangalia Magufuli angalau utaona Mafanikio yake hapa nchini sio tumboni Mwake

  CCM ni wa ajabu haswa
   
 3. F

  FJM JF-Expert Member

  #3
  May 18, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Guninita analalamika kuhusu kupanda nauli ya Kigamboni? Mbona hakusema chochote bei ya mafuta ya taa ilipopandishwa? Na anataka watu waamini kinachoifanya ccm ichukiwe na 'ubabe' wa Magufuli? Guninita amesoma report ya CAG?

  Anaweza kuwaambia watanzania kwa nini mtu aliyekuwa anasimamia biashara ya magendo ya kusafirisha sukari nje ya nchi na hata kufanya bei kupanda kwa kiasi kikubwa nchini bado yuko kwenye baraza la Mawaziri? Guninita alikuwa wapi wakati mabomu yanauwa watu wa Mbagala na Gongo la Mboto? Mabwemapande hadi leo watu wanalalamika fidia, Guninita anasemaje?

  Katumwa na mtandao gani huyu Guninita?
   
 4. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #4
  May 18, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,196
  Likes Received: 1,977
  Trophy Points: 280
  Magufuli ni mfujaji anayetia Taifa hasara kubwa sanaaaaa
   
 5. j

  joely JF-Expert Member

  #5
  May 18, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 1,030
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 160
  Hamna jipya ndani ya ccm bora wasiwe wanafanya vikao vyenye maazimio fake
  ni heri wangepanga jinsi ya kugawana mbao tu, kwa kuwa matundu sasa ni makubwa mno
   
 6. Nyakageni

  Nyakageni JF-Expert Member

  #6
  May 18, 2012
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 13,948
  Likes Received: 1,274
  Trophy Points: 280
  nao wanataka
   
 7. rmashauri

  rmashauri JF-Expert Member

  #7
  May 18, 2012
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 3,008
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Huyu Mwandishi naye ni shabiki wa mafisadi tu. Kichwa cha habari utafikiri kuna kitu cha maana humo ndani kumbe kauli ya kuwaambia wana Kigamboni tu wapige mbizi? Halafu huyu Guninita si ndo yule kuwadi wa lile genge la mafisadi?
   
 8. N

  Njoka Ereguu JF-Expert Member

  #8
  May 18, 2012
  Joined: Apr 7, 2012
  Messages: 822
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 35
  Wakti mwingine viongozi wetu ni vipofu wa fikra, na fikra zao zinaishia pale tu maslahi yao yalipo, hivi katika hali ilivyo sasa kuna sababu ya kulalamika nauli ya mia mbili kweli, kama hiyo basi ni tabu serikali itowe hiyo huduma bure. Katika mazungumzo yote ya Kamati kuu hakuna aliyefikiria hata kuzungumza namna ya kuboresha bei za mazo ya wakulima. Bei za bidhaa zote zinapanda hovyo, lakini kulima anazuiliwa kutoa mahidi yake kuuza sehemu anayoamini anaweza kupata faida. Hivi sasa kilimo kimepaki kuwa siasa, mkulima akivuna haruhusiwi kuuza ziada yake nje hata ya mkoa wake na bei zinabaki kuwa za kikandamizi. Mkulima huyo huyo nahitaji huduma muhimu ambazo bei zake zimekuwa zipanda kila dakika. Hii ni haki kweli.

  Nadhani imefika mahali wakulima kuandaa maandamano ya kudai haki zao, sasa vinginevyo waruhusiwe kununua bidhaa muhimi bila kodi.
   
 9. Pinokyo Jujuman

  Pinokyo Jujuman JF-Expert Member

  #9
  May 18, 2012
  Joined: Feb 5, 2012
  Messages: 553
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kama Mungu mwenyewe anapingwa na wanadamu alotuumba iweje kwa Magufuli? Fanya kazi Dr. kwa kuzingatia sheria na taratibu zinavyokutaka ufanye na si kwa kumfurahisha mtu bali kwa manufaa ya Taifa hili, kwani huyu mwenyekiti mbona sikumsikia akimlalamikia Masaburi alipowatukana Wabunge wa DSM kwa kuwaambia wanafikiri kwa kutumia ******?; kaliona la Magufuli kupngana na Mbunge wa Kgamboni ni kubwa zaidi; hizo ni Siasa za kinafiki kwa kuwafurahisha wampao "KULA" badala ya kuwajibika ili kuijenga kesho yetu"
   
 10. masatujr1985

  masatujr1985 JF-Expert Member

  #10
  May 18, 2012
  Joined: Oct 27, 2011
  Messages: 1,933
  Likes Received: 392
  Trophy Points: 180
  Mhhhhh, haya bana walau Magufuli tulidhani hana baya ndani ya CCM kumbe wote kushine!!! CCM weupeeeee
   
 11. Nyetk

  Nyetk JF-Expert Member

  #11
  May 18, 2012
  Joined: Feb 28, 2012
  Messages: 1,624
  Likes Received: 819
  Trophy Points: 280
  Hata kama tukifanikiwa kuing'oa CCM leo jinamizi la kifisadi litatutesa kwa miongo mingi. Why this necessary hate on people who show seriousness and accountability in their stewardship? WHY? Hili ni jinamizi la kifisadi!
   
 12. Nyetk

  Nyetk JF-Expert Member

  #12
  May 18, 2012
  Joined: Feb 28, 2012
  Messages: 1,624
  Likes Received: 819
  Trophy Points: 280
  Hata kama tukifanikiwa kuing'oa CCM leo jinamizi la kifisadi litatutesa kwa miongo mingi. Why this necessary hate on people who show seriousness and accountability in their stewardship? WHY? Hili ni jinamizi la kifisadi!
   
 13. idawa

  idawa JF-Expert Member

  #13
  May 18, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 18,527
  Likes Received: 10,441
  Trophy Points: 280
  Tatizo Magufuli hayupo upande wao ndio maana anasakamwa, yupo kwa wenye chongo halafu ana macho mawili yote hivyo lazima wamwone sio mwenzao.
   
 14. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #14
  May 18, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Yaani huyu dingi nilikuwa namheshimu badala ya kulalmikia mambo ya msingi unalalamikia stm kupiga mbizi ndo altenative.
  Kwani kabla ya kivuko kuwekwa walikuwa wanaendaje makawao.
  Watu maskini zaidi ya wakazi wa DSM wanalipa ela kubwa kuliko ninyi CHATO ni 500,Kilombero kama sikosei 300tshs.
  Tuone haya sometimes
   
 15. brazilian

  brazilian JF-Expert Member

  #15
  May 18, 2012
  Joined: Feb 10, 2012
  Messages: 607
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Guninita na mnafiki. Anaacha kuzungumzia mfumuko wa bei kwenye vyakula analalamika nyongeza ya sh 200 kwenye kivuko. Bonge la gamba hili halafu lioga ajabu. Cr*P
   
 16. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #16
  May 18, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Kwani Magufuli ni Waziri wa Kilimo ? kwanini azungumzie mfumuko wa bei kwenye Vyakula wakati yeye ni Waziri wa Ujenzi?

  Au tunampa kazi zisizomhusu halafu tunalalamika kwani yeye ni Mrema wakati wa Utawala wa Rais Mwinyi; Naibu Waziri Mkuu; Kila kitu anagusa anakiacha nusu anarukia kingine anaacha nusu anakimbilia kingine. Ndiyo Vyeo Vya CCM.
   
 17. N

  Njaare JF-Expert Member

  #17
  May 19, 2012
  Joined: Sep 26, 2010
  Messages: 1,075
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135

  Kwani yeye alishawaomba radhi wakazi wa Dar es Salaam kwa kuua mradi wa mabasi ya wanafunzi? Ama kweli nyani haoni kundule!
   
 18. B

  BULOLE BUKOMBE JF-Expert Member

  #18
  May 19, 2012
  Joined: Apr 7, 2011
  Messages: 488
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  ujinga wa viongozi wa dar wakiwemo wabunge hasa ndugulile na mtemvu ndicho kilichomfanya dr. Magufuli awaambie wapige mbizi kwani kwa akili ya kwaida mtu hawezi kubisha ongezeko la shilingi mia tatu akaacha ongezeko la sukari la shili 2500/= akakaa kimya. Tena narudia wakazi wa dar kama hawawezi kulipa tsh.300 wapige mbizi kwa uvivu wao magufuli yuko sahihi 10000000% na wote wanaompinga magufuli wamelaniwa akiwemo guninita. Wafujaji wanawaacha wanahangika na mtumishi wa watu asiyetaka rushwa, bali kazi na ukweli tu Mungu mbariki Dr. Magufuli. Guninita ni mjinga kuliko wajinga wengine wote tena ni mnafiki toka akiwa UVCCM angekuwa na mapenzi na watu wa Dar angewatetea wamachinga na akina Mama lishe wanaodhulumiwa kila siku na Mgambo wa Jiji, pia angetetea huduma muhimu kupelekwa Mabwepande zaidi ya yote angetetea Wakazi wa Mbagala walipwe fidia zao kwa nyumba zilizobomolewa na Mabomu lakini kwa ushenzi wake amekalia habari iliyokufa ya nauli ya kigamboni, watu walishasahau na wanalipa kama kawaida yeye anaibuka na wendawazimu wake eti Magufuli mbabe, Magufuli siyo mtu wa kubembelezabembeleza yuko kikazi zaidi. Kama wanaona Magufuli hafai wamuulize JK kwa nini anamteua kila wakati kushika wizara ya Ujenzi?
   
 19. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #19
  May 19, 2012
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,520
  Likes Received: 1,690
  Trophy Points: 280
  Makosa hayawi cleared na mafanikio. Magufuli ni fisadi kama alivyo jk.
   
 20. UmkhontoweSizwe

  UmkhontoweSizwe JF-Expert Member

  #20
  May 19, 2012
  Joined: Dec 19, 2008
  Messages: 2,967
  Likes Received: 240
  Trophy Points: 160
  ​Shangaa na wewe bwana hakimu!
   
Loading...