NAMBA MOJA AJAYE NCHINI
JF-Expert Member
- Oct 29, 2019
- 8,512
- 17,417
Ndani ya misimu minne ntashinda taji moja. Ndivyo Klopp alivowaambia waandishi wa habari misimu mitatu na nusu iliyopita. Jamier Ghalagher alimuonya Klopp kuwa siyo rahisi kihivyo na ni kosa kubwa sana kuahidi taji ndani ya misimu minne.
Alianza na mfumo wake wa gegen pressing kwa wachezaji plastic kama Sturidge alishindwa kabisa, wazito kama Benteke walikoma! Maumivu ya misuli yalishamiri ndani ya kikosi na madaktari wa viungo walimponda sana Klopp hata Ferguson alidiriki kusema hajawahi kuona tim ina press muda wote. Klopp alijibu kirahisi kuwa anahitaji msimu mmoja kuweka msingi wa utimamu wa mwili wa wachezaji wake.
Hakukurupuka kusajili kwa bei bali alianza kuingiza falsafa yake pole pole kwa wachezaji aliowakuta huku akiwauza wale walioshindwa na kuwaingiza wapya pole pole ndani ya timu. Hadi sasa ni wachezaji wanne tu wa kikosi cha kwanza aliowakuta wamebaki ndani ya kikosi na hata hivyo hawana uhakika wa kuanza kikosi cha kwanza. Adam Lallana, Jordan Henderson, Firmino na Origi ndiyo pekee waliobaki katika kikosi cha Klopp.
Ninapoandika huu ni msimu wa tatu na nusu kwa Klopp na ameshatwaa mataji makubwa matatu yaani UCL, FIFA CLUB W.CUP na UEFA SUPER CUP amezidi matarajio ya mashabiki wa Liverpool na sasa anaongoza ligi kwa point 13 akiwa na mchezo moja wa kiporo dhidi ya Westham.
Huyo ndiyo Klopp alietaka kuwageuza wasio na imani wawe na imani na timu yao, wakati sherehe zikishamiri mashabiki pinzani wamebaki na gubu mioyoni mwao huku wakisingizia teknolojia ya video eti inawabeba Liverpool. Wamesahau kuwa TAA amebadilishwa kuwa Kevin Debruyne, Robertson kawa Marcel Henderson kwa makelele n.k. Unathubutu vipi kusema liva inabebwa kwa VAR? hamuoni MANE, SALAH na FIRMINO wanavyofanya kazi yao? Hamuona Gini na Hendo wanavyokaba?
Hamuoni Origi alivo super sub? Acheni uchawi, Furahieni angalau mmebahatika kuona kikosi bora zaidi katika historia ya EPL. Liver hii inaenda kutawala EPL kwa miaka kumi.
Mashabiki pinzani mjilaumu wenyewe kwa tim zenu kufanya maamuzi ya hovyo!kwa mfano eti leo Ancelotti yupo Everton halafu man utd wamemkumbatia Ole wakati Massimiliano hana timu nyie mnampa Arteta timu, wakati Mourinho yupo Spurs. Chelsea eti ina Lampard. Huo ni uhuni ambao hata Masau Bwire hawezi kuufanya hapa Bongo.
Nawashauri furahieni maisha ya soka kwa kuishangilia Liverpool hii ya mabingwa ya Mjerumani JURGEN NOBERT KLOPP.