Teknolojia ni Yetu sote
JF-Expert Member
- Apr 28, 2020
- 1,221
- 2,425
Kampuni ya rockstargames imetoa Tarehe Rasmi ya kuachiwa kwa game mpya aina ya grand theft auto GTA 6 ambapo itaachiwa 26 Mei 2026 Mwakani. Wengi walitegemea itaachiwa mwaka huu lakini kampuni hiyo imesogeza mbele.
Game hii kwa upande wa graphics wametisha sana Iko poa balaa, GTA 6 franchise , hule Mji wa Vice city ambao ulikuwepo kwenye GTA vice City stori ya mwaka 2006 sasa unapatikana kwenye Gta 6.
Maeneo ambayo GTA 6 imechezewa ni katika miji mbalimbali kama ifuatavyo;
⚡Vice city ambao ndo Mji mkuu
⚡ Leonidas keys
⚡ Port Gelhorn na
⚡ Mount kalaga
💡Muhusika mkuu kwenye game hii ni Jason Duval akiwa na Rafiki wake wa Kike ambaye anaitwa Lucia Camino's, wengi walitegemea wakongwe watakuwepo lakini wahusika wengi ni wapya.
Kwa ufupi TU story inamuhusu jamaa anaitwa Jason Duval mwanaume anayepambana kutafuta maisha mepesi lakini inakua ngumu baada ya kukaa jeshini kwa muda mrefu Hatimaye anaacha kazi ya Jeshi na kujiunga na kundi la wauzaji wa dawa za kulevya.
Wakati kwa upande wa Mwanamke anaitwa Lucia amefungwa Gerezani baada ya kuipambania familia kutoka kwenye mji wa liberty City. Mission ziko jumla 107.
Trailer lake angalia 👇🏾👇🏾
Kwa upande wa Specs Hakikisha una storage ya kutosha kwenye playstation 4 na XB1 Gb 45, kwenye kompyuta ni Gb 65 kwa ajili ya kufanya installation.