Grief reliase

Horseshoe Arch

JF-Expert Member
Joined
Aug 10, 2009
Posts
13,402
Reaction score
12,792
Ndugu wana JF,nasikitika kupoteza ndugu zangu watatu jana 15/05/2011 kwa matukio tofauti tofauti km ifuatavyo:-

Tukio la kwanza ni mama mkubwa aliyekua mgonjwa (wa wastani ) aliyefariki asubuhi ya jana kwenye harakati za kuwahishwa hospitali.Habari zilipotufikia tukaamua kutulia nazo kwa kua hali ya afya ya baba mkubwa (mume wa marehemu) haikua nzuri kupokea taarifa hizo...wakati tunaendelea kutafuta watu wa kumweka vizuri mzee kisaikology ili apewe taarifa zikaja taarifa nyingine za kaka yangu (age mate) aliyefariki Muhimbili Hospital alikokua amelazwa baada ya kuteleza kidogo wakati akitembea na kuvunjika uti wa mgongo!

Kwa kujua tayari tuna misiba miwili tukaazimia jioni ya jana tukampe taarifa baba mkubwa na kuweka misiba miwili kwake (kwa kua ndugu kijana alikua amepanga Mwananyamala) lakini hatukujua mipango ya Mungu kwani naye hali ilibadilika ghafla na katika harakati za kujaribu kuokoa uhai wake safari yake ya mwisho ikaishia mapokezi Mwananyamala Hospital!Kwa kutambua nasi njia yetu ni moja nitumie fursa hii kuwaombea dua njema marehemu wote!
 
Poleni sana. Mungu awatie nguvu katika kipindi hiki cha majonzi na awape marehemu pumziko la amani.
 
Pole sana kaka mkubwa, ni jaribu kubwa sana!
 
Pole ndugu kwa misiba na majonzi makubwa katika familia yenu.

Steve Dii
 
Dahhh poleni sana mkuu ndio khatma ya mwanaadamu ashukuriwe Muumba kwa maamuzi yake....awalaze pema..Aaamin
 
Nikushukuruni sana ndugu kwa kuwaombea ndugu zangu dua njema...ni imani yetu Mola amezisikia....Ni punde tu nimetoka katika kikao cha familia ambacho kimepanga siku ya alhamis tumzike baba mkubwa na mkewe ilihali kaka azikwe siku ya ijumaa...Mungu alotupa nguvu hadi sasa ni imani yangu ataendelea kutuimarisha hadi matatizo haya yafike pwani! Wabillah Tawfiq
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…