Hapana Bwana Jerrymsigwa,Green Card ya Lottery inayojulikana kwa jina la DV-1 haijafutwa bado ipo.Lakini hatima ya utaratibu huu wa watu 50,000 kuingia Marekani kwa ushindi wa Lottery hiyo utafutwa mara Muswada mkubwa wa mabadiliko ya sheria ya Uhamiaji itakapopitishwa na Bunge la Marekani.Katika Muswada huo miongoni mwa mambo yaliyopendekezwa ni kufutwa kwa DV-1 na kuongezwa viza kwa watu wenye vipaji maalumu.Pindi muswada huo utakapopita jumla ya watu 11.4milioni waliokuwa wanaishi kinyume cha sheria Nchini Marekani watapata Makazi ya kudumu (Permanent Residence) na baada ya miaka 13 kama mienendo yao ni mizuri watapewa uraia.Katika kundi hilo la watu milioni 11.4 wapo Watanzania wengi.