Katika mazingira mengi (most cases) wanadamu tumeumbwa kuitikia (respond) matukio mbali mbali kwa namna tofauti. Hata hivyo jambo hili linatofautiana kwa mwanadamu mmoja na mwingine.
Mfano ikitokea watu kadhaa wamepata taarifa za msiba. Kuna watakaochanganyikiwa na kuweza kupata au kupatwa na ajali kama watakuwa barabarani.
Au ikitokea mtu amepoteza ajira aliyokuwa akiitegemea sana kwa maisha yake kuna atakaye chukua hatua au maamuzi ambayo asingeyachukua kama asingepatwa na janga hilo.
Mara nyingi katika matukio kama haya au mengine tumekuwa tukishauriwa kutohamaki(panic) badala yake tumekuwa tukiambiwa “calm down”, “relax”, “ take it easy “ tukiaminishwa kuwa kwa kufanya hivyo tutaweza kuamua kwa busara na kuepuka ajali au matokeo hasi ya matendo yetu kutokana na kuhamaki(panic)
Swali linakuja.
- Je, haiwezekani kuwa kwa kujaribu ku-calm down tutakuwa tunakinzana na maumbile halisi ya kiuumbaji(nature)?
- Nauliza hili nikiamini mwili wa mwanadamu ulivyoumbwa kuitikia vichocheo (stimuli) uko sahihi na hauwezi kukosea. Kwa kuthibitisha hili angalia irisi (iris) ya jicho inavyoitikia mwanga mkali au mwanga hafifu, kinywa kinapoitikia kwa kutoa mate pale unapolitazama limao au ukwaju kwa kuutamani.
- Sasa iweje mtu akihamaki(panic) tunajaribu kumtuliza?
- Je, kwa kufanya hivyo hatukosei?
Naomba mawazo yenu watu wenye ufahamu juu ya jambo hili.
Asanteni sana.
Kuna maoni yanayochukua kukubalika kwa sana sasa katika nyanja za saikolojia kwamba, ni vizuri watu kuachia hisia zao.
Kwa mfano, habari za kwamba wanaume ni shupavu na hawatakiwi kulia, angalau hadharani, zinapingwa, na wanasaikolojia wanasemakwamba mtu akijisikia kulia, halafu akajizuia kulia, hilo linamfanya akosekutoa hisia zake na atazikusanya zikae ndanikwa namna ambayo inaweza kumletea madhara baadaye.Kuna ushahidi wa kisayansi ya kikemikali unaoonesha kwamba matendo kama kulia huwa yanaendana na kuachilia kemikali fulani ubongoni, mwilini, na hivyo, kama mtu anajisikia kulia na asipolia, anawezakuwa anazifungia kemikalihizi asizitoe.
Mimi binafsi hupenda kuangaliamambo kimantiki, na kwenye vitu kama misiba, nakuwa mgumu kulia. Kwa kitambo sasa, nimejifunza kutohuzunika sana mambo yanavyokwenda kinyume na ninavyotaka, na pia kutofurahia sana mambo yanavyokwenda vizuri sana, nafikiri falsafa za ki Buddha nilizosoma, zinazoelezea umuhimu wa kuwa na equanimity (kuchukulia mambo yote kwa usawa wa mawazobila kuhamanika au kufurahi sana) zimenisaidia sana kuwa hivyo.
Pia, mimihujiona kamamtu wa kusaidia, kwa mfano, sehemu kama msibani, mimi hujiona kama askari ambaye atadaka wale wanaolia na kuanguka, sasa askari mimi tena nikilia, watu wakilia na kuanguka nani atawadaka? Muda wote nakuwa busy kuangalia logistics,kuna chakula? kuna vinywaji? Kuna viti? Nini kinahitajikakufanyika? Mipango inaendaje? Nani anahitaji msaada? Watu muhimu wana habari? Wazee wanaohitaji kusaidiwa wamesaidiwa? Watoto wataendanaje na mazingira haya? Habari za usafiri zimetengemaa? Kuna hatari ya mifarakano? Kama zipo, usuluhishi na uzuizi unaweza kugfanyaje? Kuna wanaotaka kupiga picha? Hilohalitaleta mtafaruku? Kuna mgongano wa kitamaduni?Pombe itanyweka? Walokole watasemaje? Waislamu watakula chakula kilicho halal? Maji yakosalama?
Yani kwenye msiba akili inaenda spidi ya mwanga hivyo, hata kulia nasahau.
Nitakuja kulia peke yangu wiki mojabaadaye, mwaka mmoja baadaye, au hata miaka ishirini baadaye.
Nikimkumbuka mtu peke yangu.