Gration Mukoba anatishia nyau

The Phylosopher

JF-Expert Member
Mar 11, 2015
1,911
2,890
Leo rais wa chama cha waalimu tanzania mwalim mkoba ameitaka serikali iwalipe waalim madai yao yote kabla ya mei mosi kwani serikali isipofanya hivyo waalimu watagoma kushiriki sherehe za meimos mwaka huu na kutanganza mgogoro na serikali.

Mkoba ameyasema hayo akiwa kwenye ziara ya siku tatu ya kutembelea waalim mkoani Shinyanga ninacho jiuliza ni kuwa walishindwa kugoma siku zote za mkwere watawezaje sasa!

Asiwarubuni waalim awe mkweli kua hicho chama hakina ubavu mbele ya watawala ikibidi kivunje kiundwe kingine!!
 
Huyu jamaa anamatatizo
Pombe ndo kwanza ameingia madarakani, siwampe walau mwaka mmoja iliajipange... ....
Vipaumbele nivingi sana...fedha haiwezi tosha mambo yote kwampigo.
Huku ndo kutafuta umaarufu kusiko natija yoyote.
 
huyu jamaa mzima kweli?? walishindwa kugoma enzi za mkwere ndio ataweza sasa

mzee ameshasema " mtu asimletee fyoko fyoko"
shauri zake
 
Wamesharubuniwa hao.Mkoba alikuwa zamani na Mgaya.Kwa sasa wote ni toothless old dogs
 
Sijui unamzungumzia nani maana ninayemfaham anaitwa gratian mkoba. Sa sijui ni mimi au wewe unayekosea.
 
Halafu wakati mwingine huwa napata hisia kwamba huyo Mukoba huwa anatishia ili akatiwe chochote na serekali. Hajawahi kusimamia chochote kikafaninikiwa na haya madeni yote yamejilimbikiza yeye akiwa kiongozi mkuu wa hicho chama. Hana lolote atafanya zaidi ya kuwapumbaza waalimu. Ni bahati nzuri tu walimu wana uvumilivu wa kondoo.
 
Walimu wanahitaji Professional board, Trade Unions zimekaa kisiasa zaidi. Hapo Mukoba anatafuta kiki ili apoozwe, mwishoni utasikia, mgomo umezuiwa na mahakama.
 
Mgomo una taratibu zake. Ni hatua ya mwisho kabisa baada ya hatua za mazungumzo na reconciliation kushindikana. After all, bwana Mukoba alikuwa wapi siku zote! Walimu wana madai yaliyolimbikizwa kwa muda mrefu sasa takribani miaka 5! Ilikuwa bora awaeleze walimu kipindi chote hicho alikuwa wapi asiweze zungumzia suala hilo nyeti yeye akiwa kiongozi mkuu wa TTU (CWT) As they identify themselves, a pressure group, which ought to be real, what kind of pressure do the TTU, which is all over Tanzania(at every school, teachers' college,in every district and region)exerts to employers i.e district executive directors kwa upande wa walimu wa elimu ya primary na sec?
Maana bwana Mukoba hakupaswa kufika hatua hiyo k.m kweli madai ya walimu hasa salary arrears yangekuwa yanawasilishwa kwa wakati. Na hii ingetokana na follow up ya makatibu na wenyeviti wa TTU ngazi ya wilaya na mikoa km wangewajibika ipasavyo.
Madai huwa yanahakikiwa na kubaki ktk halmashauri kwa muda mrefu kutokana na uzembe wa maafisa utumishi na kutokuwepo kwa ufatiliaji wa viongozi wa TTU niliowataja. Matokeo yake ni malalamiko ya serikali haiwalipi walimu wakati madai hayafikishwi hazina kwa wakati. Maafisa utumishi wa halmashauri, Mukoba na watendaji wa TTU badilikeni. Timiza wajibu wenu.
Naomba kuwasilisha.
 
Tumeshamzoea. By the way Serikali ya Magufuli inajali sana watumishi wake
Anatishia nyau usiogope. Hata mimi najua anatishia nyau. Walishindwa kumgomea rais dhaifu kabisa aliyepita watamuweza jabali huyu . Huku si kutaka kuchezea testicles za baba badala ya mother's breast. Wajaribu waone. Usiwe na wasiwasi mngoni.
 
Anatishia nyau usiogope. Hata mimi najua anatishia nyau. Walishindwa kumgomea rais dhaifu kabisa aliyepita watamuweza jabali huyu . Huku si kutaka kuchezea testicles za baba badala ya mother's breast. Wajaribu waone. Usiwe na wasiwasi mngoni.
 
Leo rais wa chama cha waalimu tanzania mwalim mkoba ameitaka serikali iwalipe waalim madai yao yote kabla ya mei mosi kwani serikali isipofanya hivyo waalimu watagoma kushiriki sherehe za meimos mwaka huu na kutanganza mgogoro na serikali.

Mkoba ameyasema hayo akiwa kwenye ziara ya siku tatu ya kutembelea waalim mkoani Shinyanga ninacho jiuliza ni kuwa walishindwa kugoma siku zote za mkwere watawezaje sasa!

Asiwarubuni waalim awe mkweli kua hicho chama hakina ubavu mbele ya watawala ikibidi kivunje kiundwe kingine!!
Sawa kabisa mkuu unachosema.Halafu jamaa akikurupuka tu anaita mgomo kipindi cha likizo au sikukuu kama hivyo mei mosi.Kama kweli anauchungu na walimu wenzie mbona hahamasishi mgomo kipindi muhimu kama cha MITIHANI ya MIHULA au TAIFA?
 
Back
Top Bottom