Unajua kuna some things watu wanakosea... naomba nijaribu kufafanua kimoja kimoja ili mjue vizuri jinsi mambo yanavofanya kazi..
Kwa aliyeuliza kuhusu 3D rendering, kuna technique mbili tofauti kwenye 3D rendering, ya kwanza na ambayo inatoa very accurate renders ni ya kutumia CPU, inahitaji CPU kubwa hapa kama unataka speed kweli tunaongelea high end CPUs za i7, kwa nini CPU inatoa very accurate renders na ndio inatumika kwenye industry kubwa duniani kutengeneza 3D animated movies, sababu ni kuna kitu kinaitwa Ray tracing, hii ni technique ya kurender ambayo light ray (virtual) inakua inapita across 3D objects na kusimulate real light effect, hii hairun in parallel ndo sababu kubwa its done kwenye CPU peke yake na it takes a long time sababu CPU unlike GPU haina cores nyingi. Wamejaribu kutengeneza GPU ray tracing techniques lakini still hazitoi very good image compared to a CPU ray tracing technique.
Technique ya pili ni kwa kutumia GPU, render ambayo ingekuchukua saa moja kwenye CPU inaweza kukuchukua sekunde 20 kwenye GPU, tatizo ni hutopata quality nzuri sana ya renders kama ambayo ungepata kwenye CPU, sababu ni kama nlivosema hapo juu, GPU techiniques hizi zinajaribu tu kusimulate mwanga kwa technique mbalimbali ambazo sio very accurate, sema utapata a good overview ya render yako itakavyokua very quickly..
Sasa hapo ni kuchagua mwenyewe, kama unataka realistic looking graphics, kama movie animations etc itakulazimu kwenda na CPU rendering, kama unataka good looking graphics ila sio lazima ziwe na very high accuracy then nenda na GPU rendering.
Umesema una dual core, hiyo processor inabidi upige chini tu utafute a better processor, kwa 3D graphics hapo huchomoki, na hata kwa games the max you could run ni 30fps ukiwa na graphics card nzuri, sasa hata kama una pesa ndefu usijisumbue kununua very high end GPU sababu itakua bottleneck, GPU iko very fast ila processor inashindwa kucatch up na GPU, mwisho wa siku unakua umepoteza pesa kununua more graphics perfomance than your processor can handle.. kwa ushauri tu nenda na mid range GPUs kama Radeon R7 260X, au GT 730, dunia iko mbali sasa ununue hata online tu wafanye delivery kama bongo hutopata.. Usinunue GPU kama GTX 970, 980 CPU yako haitoweza kuhandle.
Kuongezea tu kama unataka a cheap build kabisa lakini ambayo ni fast consider kununua CPU moja Intel Pentium G3258, ni haswell CPU unaweza overclock kama una motherboard nzuri, ila kabla ya kununua motherboard yako hakikisha inaingiliana, hiyo ndo processor cheapest you can find ambayo ukiiweka na GPU kama 970 inaweza kupa 1080p 60fps kwenye magemu mengi tu. Fanya research zaidi ujue vitu kama hivi ubuild your own machine