Graduates na kukosa ajira tz ........

nziriye

JF-Expert Member
Jan 23, 2011
1,051
360
Tanzania nakupenda kwa moyo wote,nchi yangu tz,jina lako ni tamu saaaana....ni wimbo ambao nilikuwa nauimba miaka hiyo nikiwa sekondari lakini sikutambua kama nauimba kinafiki ,nina andika haya nikiwa na machungu na kubwa la leo ni kuhusu graduates wa vyuo tofauti hapa tz na nje ya nchi,na hasa nataka kuuliza kuhusu enrollment wanazofanya vyuo ina mana hawajui kuwa hapo baadaye watu watakosa ajila,graduate wa vyuo hawana kazi,wenye kazi wanafanya kazi wasizomea angalia nchi inavyochangia kupoteza ujuzi wa graduates,lakini kinachovunja nguvu wengine wanaingia ktk ajira ya ualimu ambao hawajausomea ,je watoto wakifail inakuaje aje hapo?msaada members hv tatizo la kukosa ajira kwa graduates ni kuwa hawana ujuzi,experience au elimu waliyopata haiwaqualify kupata ajira?kumbukeni elimu yetu haiwaandai graduates kuwa job creatorz ila job seekers.
 
Labda mkuu ungeanza kwa kutoa pendekezo la kuinusuru nchi kutokana na hali hii.
 
Pendekezo ni kuwa wazawa wapewe upendeleo katika ajira. Hii nchi imekuwa ni kimbilio la mataifa mbambali na hata makampuni ya nje hayaji kuleta ajira bali wanakuja na wafanyakazi wao. Sheria zipo zinazowabana lakini Uhamiaji wamejaa rushwa pamoja na Wizara ya kazi. Lada tuanze kuwataja.

Pale kampuni ya Total kuna watu wafeni wamekaa miaka mingi na kila baada ya miaka mitatu wanaenda kuhonga Uhamiji na kazi wanazofanya ni za kawaida tu. Na wengine endeleeni..........
 
Tatizo hili ni pana sana kuliko mtu anavyoweza kudhani!
Lilianza taratibu hapa kwetu enzi za Mwalimu(refer..."Mpe kazi yoyote bwana, atafanya chochote, ni mtoto wa binamu yangu")
Matokeo yake ni kuwa hii hali ime' reverberate, na kuwa mbaya zaidi enzi hizi za usomi...
Ishu nyingine kwa enzi za sas ni hii ya soko huria...Uhuru wa kuingiza finished goods nchini unasababisha kifo cha asilia kwa ujuzi wa wataalamu wetu...Tumeua viwanda na idara mbalimbali za uzalishaji, badala yake tunanunua bidhaa zilizotengenezwa za nchi za Uchina na Malaysia!
 
Pendekezo ni kuwa wazawa wapewe upendeleo katika ajira. Hii nchi imekuwa ni kimbilio la mataifa mbambali na hata makampuni ya nje hayaji kuleta ajira bali wanakuja na wafanyakazi wao. Sheria zipo zinazowabana lakini Uhamiaji wamejaa rushwa pamoja na Wizara ya kazi. Lada tuanze kuwataja.

Pale kampuni ya Total kuna watu wafeni wamekaa miaka mingi na kila baada ya miaka mitatu wanaenda kuhonga Uhamiji na kazi wanazofanya ni za kawaida tu. Na wengine endeleeni..........

Mams,
Unafikiri tatizo ni rushwa tu?
Kwenye private sector ambazo ziko profit-oriented, hawahitaji suala la uzawa tu. Wanahitaji na suala la ufanisi na nidhamu ya kazi. Watz bwana hawana nidhamu ya kazi. Mtu yupo tayari kusafiri wiki nzima kuhudhuria sendoff ya rafiki yake. Kuchelewa kazini na kuwahi kutoka ndio utaratibu wenyewe. Kuiba kazini ndio ujanja wetu. Malalamiko na majungu na kudai maslahi makubwa kuliko kazi, ndicho utaratibu wetu. Customer scaring badala ya customer care ndio jadi. Naturally, nitapendelea zaidi wafanyakazi wa nchi kama Kenya wawepo kwenye kampuni yangu badala ya waswahili.
Kwenye kazi za serikali, huko hakuna jinsi, lazima waajiriwa wawe watanzania. Kama kuna raia wa nje basi wanatakiwa wawe na uraia wa tz. Hapo ndipo hasa pa kukemea rushwa kwa watu wa uhamiaji, kama tutaona Mkenya au mganda anafanya kazi kwenye utumishi wa umma.
 
Na hivi tunavyokwenda kuunganisha soko la Afrika Mashariki yawezekana hali ikawa mbaya zaidi - maana haiyumkini wenzetu watachukua kazi katika nchi yetu zaidi ya sisi tutakavyochukua kazi katika nchi zao.
 
Mi nadhani tatizo liko kwetu watz wenyewe.
1. Watu wengi ambao hawana kazi, hawahangaiki vya kutosha kutafuta. Mtu akishatuma application mbili hajajibiwa anajikunyata na kuanza kulalamika kazi hamna
2. Wengi tunachagua kazi na tunataka tuanzie kwn senior positions, mshahara mnono wakati experience hatuna.
3. Wamiliki wengi wa makampuni wako radhi kuajiri wakenya, wageni na kuwalipa ghali kwasababu watanzania tumezidi uvivu, majungu badala ya kufanya kazi! Nenda kwenye hoteli zinazoongozwa na watz uone tofauti na zenye, mf, wakenya.
 
Matatizo ni mengi
  1. Infrastructure mbovu, ni vigumu business cooperate bila umeme, internet ya maana, usafiri na kunasa masaa kwenye traffic. Na ndo maana hatuwezi kushindana hata siku moja na bidhaa kutoka nje, cost of production iko juu.
  2. Rushwa imezidi hii inasupress biashara mpya na inaleta gharama sizizo na mpango.
  3. Elimu ni ya kitabu sana, real world skills chache sana zinafundishwa.
  4. Na mengine mengi.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom