Graduates: Maeneo/Miji ndani ya Tanzania ambayo unaweza kuanza maisha baada ya kumaliza chuo na ukifanikiwa

spleen

JF-Expert Member
Apr 24, 2013
3,224
4,663
Mada hii ni maalum kwa wale waliomaliza chuo, na hii inatokana na upungufu wa ajira, si tu Tanzania bali dunia nzima.

Sasa ukizingatia wengi baada ya kumaliza vyuo hukimbilia mijini sana sana Dar es salama kuanza maisha, kiukweli kwa asili ya Dar es salaam ya sasa kuanza mwanzo na kufanikiwa ni ngumu sana, ingawa kupata tu hela ya kula, usafiri, maradhi na makazi ni rahisi mno kuliko mji wowote ule.

Dar es Salaam kuna unafuu labda kama unaishi kwenu kidogo wanajiweza na wewe ukawa ni mtu wa kuhangaika.

Kuna maeneo ndani ya hii nchi yenye wa kazi kati ya elfu 50 hadi laki 1,ni labda vijijini, miji ama tuseme maeneo ambayo si maarufu masikioni mwa watu wengi ambayo unaweza kwenda kuanza maisha chini kabisa na ndani ya miaka 3 hadi 5,ukajikuta una mali za kutosha na umeweza kuwekeza na kuendelea kwa kiasi fulani.

Lengo la hii mada ni kushirikiana kuyataja hayo maeneo na fursa zilizopo ili tuweze kuona namna ya kuzitumia rasilimali za nchi vizuri.

Basi kwa kupitia huu uzi iwe sehemu ya wanachuo na wale waliomaliza kuona jinsi gani tunaweza kusaidiana na kufunguana akili.
Naanza na maeneo mchache .

1.Mbingu/Mngeta Ifakara.
Hayo maeneo yana fursa kubwa ya kilimo cha ndizi na biashara za ndizi, kuku, nguo kutoka mbeya(Tazara reli imepita hapo)..... Pia kuna biashara za mchele zinafanyaika.... Laki 2 unaweza Pata chumba mwaka mzima ukalipa na umeme Safi tu..... Hio ni Miji inayo kua kwa kasi sana...... Kwa mtaji mdogo unaweza anza na hayo maeneo, kama ni nguo unachukua Mbeya mtumba ni rahisi kidogo unakuja kuuzia wasukuma hapo,mchele hadi kilo 400 ukiwa mjanja unaweza uuza Dar, Moro ukapata chochote.... Hayo maeneo kuna uwekezaji mkubwa wa miti ya mitiki unaweza ishi huku ukipata shamba la heka hata moja ukapanda zako hio miti, heka moja ya mtiki baada ya miaka 20,unaweza fanya mahesabu mwenyewe.

2.Kisiwa cha Mafia.
Huku watu wengi wa bara wanapaogopa sana.
Ukiwa chuo jitahidi ujifunze hata lugha 2-3,yaani maeneo hayo ukiweza kujua mfano kiitaliano basics, kihispaniola basics huwezi kosa hata dola 500 yaani kwenye utalii.

Kuna biashara ya samaki, pweza bweni pweza kilo wanauzwa elfu 3 ukija Dar unauza hata elfu 8.
Hizo biashara watu hawana hata certificates ila wanapiga hela daily.

Kuna biashara za nazi, mtaji nisamrt phone yako tu ukiuza ukirudi Dar unanunua kama hio mpya, kikubwa ni kujilipua tu kwa wenyeji na kuonesha nini unataka kufanya.

3.Njombe/Mafinga etc.
Huko ni mji unakua kwa kasi sana. Yaani hata duka la mangi tu unaweza anza nalo huku ukiangalia fursa zaidi za kilimo.
Unaweza nunua hata heka 2 za ardhi ukaanza na miti, baada ya miaka kadhaa ukiuza unaweza nunua hata nyumba charambe, chanika na sio kulipa kodi huku ukizunguka na bahasha kila leo.

4.Kanda ya ziwa, maeneo ya Simiyu, Bunda, Bariadi.
Hii kanda watu wanazaliiana ka utitili,kuna upungufu mkubwa wa huduma za afya, umesoma pharmacy,CO etc zamia huku kodi fremu hata ya elfu 20....dawa za laki 2 ukianza nazo huko mwezi hukosi laki 8 etc......ukiritimba wa leseni sijui nini mini inayokua hamna kivile, unaweza kuanza na duka lako na baadhi ya vipimo unapima mimba, malaria etc si haba.

5.Maeneo ya Ruangwa, Nachingwea.
Majira ya miezi ya kilimo cha ufuta na korosho hizo sehemu kuna pesa zaidi ya Dubai... Unaweza kujiingiza kwa namna moja ama nyingine, dalali, msambaza viloba ilimradi tu uweze kuzoea game.

6.Mwambao wa kuzunguka ziwa Victoria.
Huwezi amini wachina wanapiga pesa mno kwenye uvunaji wa samaki kitaalamu, unaweza anza kilocal tu ukaweka kambi moja ya kijiji na kuanza ufugaji, watu wakiona upo serious wanaweza kuweka hela ukakuza mtaji wako

Nitarudi.
 
Mmhh! Ukiikacha Dar es salaam sababu ya gharama ya maisha mbona kuna miji mikubwa ina gharama za maisha za chini kidogo na biashara zinatembea sana.
Kujiingiza kwenye kilimo kwa pupa hivyo bila uzoefu ukianguka ukakosa backup je? Maana naona wengine wanasema ukianguka mara ya kwanza kwenye kilimo ni kujifunza,hivyo inabidi uwekeze tena.
Mimi naona sahihi ni kukomaa mijini mijini tu hadi kieleweke.Ukifeli mji huu unahamia ule.
Maoni yangu tu lakini.
 
Mmhh! Ukiikacha Dar es salaam sababu ya gharama ya maisha mbona kuna miji mikubwa ina gharama za maisha za chini kidogo na biashara zinatembea sana.
Kujiingiza kwenye kilimo kwa pupa hivyo bila uzoefu ukianguka ukakosa backup je? Maana naona wengine wanasema ukianguka mara ya kwanza kwenye kilimo ni kujifunza,hivyo inabidi uwekeze tena.
Mimi naona sahihi ni kukomaa mijini mijini tu hadi kieleweke.Ukifeli mji huu unahamia ule.Wazazi wangu walitoka kijijini kuja mjini kutafuta life,nikazaliwa mjini,mimi nirudi kijijini tena!
Maoni yangu tu lakini.
Sawa mkuu ni maoni yako, shida ya mjini napo kulianza kama kijiji, mwaka 1980 Mbagala Tandika, boko kulikua mapori ya sungura...... Ndio mapori ya sungura ya kiberege, nanjilinji ya sasa.... Wekeza sasa wanao wamiliki masaki ya miaka hiyo ya Singida
 
Mmhh! Ukiikacha Dar es salaam sababu ya gharama ya maisha mbona kuna miji mikubwa ina gharama za maisha za chini kidogo na biashara zinatembea sana.
Kujiingiza kwenye kilimo kwa pupa hivyo bila uzoefu ukianguka ukakosa backup je? Maana naona wengine wanasema ukianguka mara ya kwanza kwenye kilimo ni kujifunza,hivyo inabidi uwekeze tena.
Mimi naona sahihi ni kukomaa mijini mijini tu hadi kieleweke.Ukifeli mji huu unahamia ule.Wazazi wangu walitoka kijijini kuja mjini kutafuta life,nikazaliwa mjini,mimi nirudi kijijini tena!
Maoni yangu tu lakini.
Mkuu!
Usipinge kila jambo
Mleta uzi amezungumzia biashara na fursa nyingi kwenye miji tofauti tofauti mfano biashara ya pweza na nazi kutoka kisiwa cha mafia, wewe umeshupalia kilimo pekee(hata kwenye kilimo kama zilivyo biashara nyingine zote kuna wanaofanikiwa na wanaopoteza)

Ishu ya kuzaliwa mjini ni sawa, kuna wengi wamezaliwa mjini na wanapiga pesa Mikoani na wengine wako mjini lakini hawajafanikiwa.

Ni mtazamo tu.
 
Mimi nimeona comments zote mawazo yameelekezwa pointi no.1,no.3 na no.5.Nami nimegusia hapo hapo.Sijapinga upo huru kuchukua wazo lolote hapo.Ndo maana nikasema ni mtazamo wangu.
 
Mkuu!
Usipinge kila jambo
Mleta uzi amezungumzia biashara na fursa nyingi kwenye miji tofauti tofauti mfano biashara ya pweza na nazi kutoka kisiwa cha mafia, wewe umeshupalia kilimo pekee(hata kwenye kilimo kama zilivyo biashara nyingine zote kuna wanaofanikiwa na wanaopoteza)

Ishu ya kuzaliwa mjini ni sawa, kuna wengi wamezaliwa mjini na wanapiga pesa Mikoani na wengine wako mjini lakini hawajafanikiwa.

Ni mtazamo tu.
Una uzoefu na hiyo biashara ya nazi mafia?
 
4.Kanda ya ziwa, maeneo ya Simiyu, Bunda, Bariadi.
Hii kanda watu wanazaliiana ka utitili,kuna upungufu mkubwa wa huduma za afya, umesoma pharmacy,CO etc zamia huku kodi fremu hata ya elfu 20....dawa za laki 2 ukianza nazo huko mwezi hukosi laki 8 etc......ukiritimba wa leseni sijui nini mini inayokua hamna kivile, unaweza kuanza na duka lako na baadhi ya vipimo unapima mimba, malaria etc si haba.
Hili wazo nimeliewa mkuu...maana nimemaliza diploma ya pharmacy nasota kupata hata pakujitolea nipate ujuzi eti mtu hakuamini anaona utamwibia dawa zake!

Je gharama za maisha huko zikoje?hawana ubaguzi kwa wafanyabiashara wageni au ambao sio wazawa?
 
Du hi ni hatari!. ..
 
  • Thanks
Reactions: PYD
Usafiri kwenda ifakara inakuwaje kuhusu gharama kutokea moro mjini na muda wa kufika
 
Back
Top Bottom