"Graduates" karibuni sana mtaani

wiseman734

Senior Member
Apr 29, 2018
136
250
Graduates jamani karibuni sana mtaani, mmetoka chuoni, mambo yanabadilika na kuwa tofauti, huku mtaani hakuna bumu, huku hakuna atakayekupa pocket money! Wengi wenu mna matumaini makubwa ya kupata kazi nzuri zenye mishahara minono

Lakn amini usiamini kuna kipindi itafika utatafuta tu sehemu ya kujitolea hautapata! Ni wakati ambao ndugu watakukwepa na kukukimbia kwa kukuona msumbufu, zile couple za chuoni mlizoahidiana ndoa zitavunjika, hakuna atakayekuthamini.

Utazunguka maeneo mengi saana ukatafuta kazi na hautapata. Wapo watakaoenda kwa waganga wa jadi kutafuta maisha mema!

Wadada watajibidiisha kutafuta wachumba na waume za watu, wengine watashikwa mikono na kupelekwa maofisini!
Wapo wazee ambao wako maofisini waajiriwa wa serikali wataambia mjiajiri.

Lakini niwaase ni kipindi cha kumtegemea MUNGU sana.
 

dong yi

JF-Expert Member
Jan 31, 2016
3,249
2,000
Siwatishi nimewaeleza ukweli, mwaka 2011, tulipograduate tulipanga kufungua NGO's tujiajiri, tukaanza kujipa vyeo Sijui CEO, sijui Marketing Manager asee usipime
Nakumbuka wakati nipo CoET tulikuwa tunadanganyana eti tukimaliza kazi zinatusubiri.

Basi tukawa tunaambizana gari ya engineers ni surf, yaani tukitoka hapo tunawaza kwenda kupata ajira take home 1.5 ndio minimum. Tunawaza kwenda kuwa maboss. Ajira ya kwanza nikalipwa hata laki 5 haifiki kazi nafanya za standard 7
 

dong yi

JF-Expert Member
Jan 31, 2016
3,249
2,000
Be positive mkuu usitumie njia yako uliyo pitia kujudge njia za wengine kama wewe ume hustle kitaa ni wewe mkuu pambana na hali yako hahah
Mtoa uzi kaongea ukweli. Kitaa bora ufike ukiwa na low expectation ukaona mambo mswano, kuliko ufike na high expectation utajuta
 

Omusolopogasi

JF-Expert Member
Aug 31, 2017
3,166
2,000
Ukweli ndio huu. Tena umemalizia kwa msitari wenye busara - kumtegemea Mungu. Mambo yamebadilika sana. Tatizo lingine ni kwamba Wabongo hatutafuti kazi nje ya nchi. Wote tunabanana humo humo. Zamani form IV walipata kazi direct from school. Enzi hizo zilikwishapita. Kama ulivyosema sasa hivi hata ukitaka u-volunteer haupati!

wiseman734
 

gilldenu

JF-Expert Member
Mar 25, 2015
2,665
2,000
Kufeli kwako baada ya ku graduate miaka hiyo sio guarantee ya kufeli kwa graduates wa mwaka 2018 katika maisha.
Watanzania wenzangu ni lazima tubadilike.

Mindset za umaskini tusipoziacha tutakuwa tunaenda shule kusoma badala ya kuelimika.
Sema wewe mkuu labda watakuelewa.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom