Viwanda vya ndani vinawaza kupiga hela tu, vinawanyonya wakulima wa miwa na wananchi wanao nunua sukari pia, ni wavivu wa kubuni njia za kuongeza uzalishaji na kupunguza gharama za uendeshaji. Hawana tofauti na viwanda vya saruji nchini. Haiingii akili sukari (au saruji) iliyotengenezwa nje, imeingizwa nchini na ikalipiwa kodi zote bila kusahau shiping costs halafu inauzwa nafuu kuliko hiyo ya ndani. Inahitaji mwenye mamlaka awe anakunywa viroba ili aweze kuzuia sukari (au saruji) isiingie toka nje, kwanza inaongeza ushindani katika ubora wa bidhaa na unafuu wa bei hivyo mwananchi wa chini anafaidika zaidi.