Namhurumia mwenye nalo. Sijui hapo kazika bilioni ngapi, na sijui kama huwa kuna utaratibu wa kuwa na bima kabla ya kuanza kulijenga ghorofa kama hilo. Na zaidi ya yote sijui kama mkandarasi wa hilo jengo alisaini mkataba gani na mwenye nalo? Je mkandaraasi atakuwa na uwezo wa kulipa gharama zote za hilo ghorofa?
Je ni nani aliyefanya uhuni hapa, ni mwenye ghorofa alikuwa anajaribu kubana matumizi au ni mkandarasi alikuwa anaiba cement na nondo? Kwa kweli nikiliangalia hili jambo hapa, naona lina msululu mrefu wa watu wanaotakiwa kuishi selo.
yawezekana sana .....moja ya changamoto ambayo wakandarasi wanakautana nazo ni hizo.....mmiliki anataka kitu kizuri na kikubwa lakini budget finyu ila anataka wewe utumie ujuzi wako apate anachotaka.....Umenena vyema.....yawezekana mmiliki alimwambia mkandarasi atumie elimu na ujuzi wake sababu budget yake iko finyu......au mkandarasi kaiba malighafi mana tanzania magumashi mengi.......[/QUOTE sister kweli mkandarasi anaweza kushauriwa na mwenye jengo kupunguzakubadilisha vipimo vya matilio...!?
Lakini kwa mkandarasi anaefata taaluma yake kuna kiwango ikifikia inabidi uikatae kazi..yawezekana sana .....moja ya changamoto ambayo wakandarasi wanakautana nazo ni hizo.....mmiliki anataka kitu kizuri na kikubwa lakini budget finyu ila anataka wewe utumie ujuzi wako apate anachotaka.....
anapaswa sana mana tanzania magumashi mengi.......document zote ziangaliwe vizuri.....kama yeye analipa pesa alipaswa afwatilie kwa karibu kupitia consultancy wake kama mkandarasi anaweka malighafi zinazohitajika......binafsi sidhani kama mwenye ghorofa anapaswa kushitakiwa, maana kaajiri maengenia na washauri juu, kama hiyo haitoshi kuna wakaguzi wa majengo wapo wanalipwa hela na serikali
ni wachache wenye huo ujasiri......wengi wanafanya ili apate pesa na kumridhisha mmiliki na kuipanua CV yake kuwa ameshawahi kujenga jengo fulani.....yawezekana pia engineer estimation ilikuwa ndogo compare to actual cost na mmiliki alikuwa amejiandaa kwa kupitia engineer estimation tu na akutaka kusitisha project yake.Lakini kwa mkandarasi anaefata taaluma yake kuna kiwango ikifikia inabidi uikatae kazi..
Ndicho ninachokifikiria pia. Inafaa asaidie polisi. Angalau na yeye atuambie ni nini kilichopelekea huko tulikofikia. Hadi kupoteza uhai wa watanzania zaidi ya 30 wasio na hatia na pia disturbance aliyoisababisha pale mahali. Though katika hali ya kawaida si ajabu huyo mwenye ghorofa, yupo hospitali hadi hivi sasa. Maana haya mambo sometimes ni mazuri kuyasikia kwa wenzako tu, yasikupate mwenyewe.anapaswa sana mana tanzania magumashi mengi.......document zote ziangaliwe vizuri.....kama yeye analipa pesa alipaswa afwatilie kwa karibu kupitia consultancy wake kama mkandarasi anaweka malighafi zinazohitajika......
Hakika sisi Watanzania ufisadi utatuangamiza. Tumezowea kushuhudia wa asasi kubwa kubwa lakini huu wa kukabidhiwa simenti ya kuchanganyia zege kisha ukaiuza na kukoroga zege la tope Na kupanda juu yake na kuporomoka nalo ndiyo kiboko zaidi.Mungu mkubwa, lingekuwa limekamilika na kuanza kutumika. Sijui hali ing'ekuwa vipi.
View attachment 88906
Namhurumia mwenye nalo. Sijui hapo kazika bilioni ngapi, na sijui kama huwa kuna utaratibu wa kuwa na bima kabla ya kuanza kulijenga ghorofa kama hilo. Na zaidi ya yote sijui kama mkandarasi wa hilo jengo alisaini mkataba gani na mwenye nalo? Je mkandaraasi atakuwa na uwezo wa kulipa gharama zote za hilo ghorofa?
Je ni nani aliyefanya uhuni hapa, ni mwenye ghorofa alikuwa anajaribu kubana matumizi au ni mkandarasi alikuwa anaiba cement na nondo? Kwa kweli nikiliangalia hili jambo hapa, naona lina msululu mrefu wa watu wanaotakiwa kuishi selo.
Inapendeza kwamba na wewe shabiki namba moja wa CCM leo umeamua kuacha unafiki na kusema ukweli. Ni nini tatizo sasa? Angalia vitu feki vingi vilivyowahi kukamatwa au dhuluma kubwa zilizowahi kufanywa nchini uone kama hutakuta wahusika wake wakubwa ni CCM. Hizi feki nyingi zinaendeshwa na CCM kwa kuwa hawawezi kukamatwa wala kushitakiwa kutokana na uenzetu plus michango yao kwa chama. Hapa ndipo ambapo CCM imetufikisha kwa sasa. Tuna wakati mgumu sana kusema ukweli, hadi CCM ije itoke madarakani tutakuwa tushapoteza uhai wa watanzania wengi sana.
Nakuomba radhi kwa kuchanganya majina. Lakini ninakushukuru pia kwamba umeshanisamehe.Samahani mkuu nadhani umenifananisha.
Sijawahi hata siku moja kuwa shabiki wa ccm, una uhuru wa kucheki posts zangu kadhaa humu jamvini.
Ninakusamehe ingawa kauli yako kwangu mimi ni sawa na tusi la nguoni!
Mara nyingi sana nimekuwa nikiona kwenye blogi mbalimbali kama Michuzi, magazetini na kwenye matangazo na picha binafsi zinazoonyeshwa kwenye mitandao ya kijamii. Kwa sifa nyingi sana watu wamekuwa wakinadi 'vikwangua anga' vinavyochipuka kila kona ya jiji la Dar na miji mingine ya Tanzania. Baada ya kuangalia picha ya lile jengo lililobomoka juzi na kuangalia jinsi kile kifusi kilivyokuwa, ninaogopa hata kufikiria kuhusu ubora wa hivyo 'vikwangua anga' vinavyosifiwa sana kila kukicha. Ukweli ni kwamba suala zima la viwango nchini kwetu halipo. Madawa feki yamezagaa, hospitali ziko chini ya viwango, shule ziko chini ya viwango, barabara chini ya viwango n.k. Hivi vyote ni viashiria dhahiri vya mahali ambapo ccm ambayo imekuwa madarakani tangu ilipoanzishwa 1977 na kupokea kijiti kama kwenye mbio za vijiti kutoka TANU ambayo ilikuwa madarakani tangu 1961. Ninachojaribu kusema ni kwamba, tumepotea njia. Sasa hatuna budi kukaa chini na kufikiri ili tubadilishe kabisa mwelekeo. Tufanye maamuzi magumu leo ili kesho tuweze kuipata dira yetu ambayo itatuonyesha njia ya kuelekea huko tunakokutaka.
Mwalimu alituasa, maendeleo siyo vitu, maendeleo ni lazima yawe ya watu. Tulipoanza kushabikia vikwangua anga wakati hatuna udhibiti juu ya wajenzi, makandarasi, vifaa vya ujenzi vya uhakika ikiwemo sementi, vibali vya ujenzi vinavyotolewa kwa misingi ya rushwa na udanganyifu tulishafikiria ya kuwa vikwangua anga ndiyo maendeleo. Tujiandae kwa matukio mengi tu kama haya.
Mungu Ibariki Tanzania!
Namhurumia mwenye nalo. Sijui hapo kazika bilioni ngapi, na sijui kama huwa kuna utaratibu wa kuwa na bima kabla ya kuanza kulijenga ghorofa kama hilo. Na zaidi ya yote sijui kama mkandarasi wa hilo jengo alisaini mkataba gani na mwenye nalo? Je mkandaraasi atakuwa na uwezo wa kulipa gharama zote za hilo ghorofa?
Je ni nani aliyefanya uhuni hapa, ni mwenye ghorofa alikuwa anajaribu kubana matumizi au ni mkandarasi alikuwa anaiba cement na nondo? Kwa kweli nikiliangalia hili jambo hapa, naona lina msululu mrefu wa watu wanaotakiwa kuishi selo.
Umenena vyema.....yawezekana mmiliki alimwambia mkandarasi atumie elimu na ujuzi wake sababu budget yake iko finyu......au mkandarasi kaiba malighafi mana tanzania magumashi mengi.......
yawezekana sana.....yani kila kitu kinapunguzwa.kweli, inasikitisha sana... hapo sasa jengo la ghorofa 16 linajengwa kwa kufanya maarifa zaidi kuliko nondo na sementi,
dah limejipiga mtama pwa kwa sasa tanzania hakuna tunaloliweza.