Gorofa kabla na baada kuporomoka

Namhurumia mwenye nalo. Sijui hapo kazika bilioni ngapi, na sijui kama huwa kuna utaratibu wa kuwa na bima kabla ya kuanza kulijenga ghorofa kama hilo. Na zaidi ya yote sijui kama mkandarasi wa hilo jengo alisaini mkataba gani na mwenye nalo? Je mkandaraasi atakuwa na uwezo wa kulipa gharama zote za hilo ghorofa?

Je ni nani aliyefanya uhuni hapa, ni mwenye ghorofa alikuwa anajaribu kubana matumizi au ni mkandarasi alikuwa anaiba cement na nondo? Kwa kweli nikiliangalia hili jambo hapa, naona lina msululu mrefu wa watu wanaotakiwa kuishi selo.
 
Hii ni sinema nyingine tena kwani hakuna lolote watakalofanyiwa hao mnaowaita wahusika. Sio mara ya kwanza ghorofa kuporomoka; hapo hapo mjina liliporomoka ghorofa karibu na mtaa wa bibi titi , wahusika wakatiwa ndani na mpaka leo kesi ilipelekwa mahakamani na haijasikika tena!! Hata lile la Chang'me lilipoporomoka wakaishia kuunda tume enzi za Lowassa akiwa waziri mkuu lakini hakuna aliyewajibishwa, hivyo basi msitegemee lolote jipya kuhusu uwajibikaji ni sanaa kwa kwenda mbele!
 
haya majanga ya majengo sijui yataisha lini........MUNGU ATUNUSURU.
 
Umenena vyema.....yawezekana mmiliki alimwambia mkandarasi atumie elimu na ujuzi wake sababu budget yake iko finyu......au mkandarasi kaiba malighafi mana tanzania magumashi mengi.......
 

Umewezaje kukimbilia kumhurumia mwenye ghorofa kabla ya wahanga? Kumbe hata hujui ni uzembe wa nani still unamhurumia.

Iko hivi, ALIOMBA PERMIT YA GHOROFA 13 badala yake kajenga 16 endelea kumuonea huruma
 
Jamaa kala hasara sana ghorofa 17 zimeteketea!
 
haya mambo ni magumu sana........consultancy wa mradi naye anahusika mana kwenye ujenzi ilibidi awe bega kwa bega kwa kila stage ambaye mkandarasi anapitia ili ajue kama vitu vinavyotumika viliorodheshwa kwenye tender document na bill of quantity (BOQ).......na kama mkandarasi anafwata specification kwenye ujenzi wake.......
 
Hili jengo mbona hata kwa kuliangalia tu kwa macho kama limelalia upande vile
Kabla ya kuchukuliwa hatua mkandalasi kwanza vyeti vyake vichuguzwe
itakuwa ndo walewale ambao siku za paper hawapo darasani,alafu matokeo
yakitoka ana AAAAAAAAAAAAAAA COZ ZOTE











 
...wakaishia kuunda tume enzi za Lowassa akiwa waziri mkuu lakini hakuna aliyewajibishwa....
Naamini hakuna atakayewajibishwa, kwa kuwa kama wataruhusiwa kujitetea, kila upande utakuwa sahihi. Kwanza angalia viwango vya nondo na viwango vya simenti, utakuta simenti ina mhuri wa tbs, wakati huohuo haiko kwenye kiwango. Vifaa vingi vya ujenzi vitumikavyo hapa nchini ni fake. Hivyo wahusika hawawezi kuwajibika iwapo serikali imeruhusu kutumia vifaa visivyo na ubora usio kidhi viwango vya kimataifa.
 
Mara nyingi sana nimekuwa nikiona kwenye blogi mbalimbali kama Michuzi, magazetini na kwenye matangazo na picha binafsi zinazoonyeshwa kwenye mitandao ya kijamii. Kwa sifa nyingi sana watu wamekuwa wakinadi 'vikwangua anga' vinavyochipuka kila kona ya jiji la Dar na miji mingine ya Tanzania. Baada ya kuangalia picha ya lile jengo lililobomoka juzi na kuangalia jinsi kile kifusi kilivyokuwa, ninaogopa hata kufikiria kuhusu ubora wa hivyo 'vikwangua anga' vinavyosifiwa sana kila kukicha. Ukweli ni kwamba suala zima la viwango nchini kwetu halipo. Madawa feki yamezagaa, hospitali ziko chini ya viwango, shule ziko chini ya viwango, barabara chini ya viwango n.k. Hivi vyote ni viashiria dhahiri vya mahali ambapo ccm ambayo imekuwa madarakani tangu ilipoanzishwa 1977 na kupokea kijiti kama kwenye mbio za vijiti kutoka TANU ambayo ilikuwa madarakani tangu 1961. Ninachojaribu kusema ni kwamba, tumepotea njia. Sasa hatuna budi kukaa chini na kufikiri ili tubadilishe kabisa mwelekeo. Tufanye maamuzi magumu leo ili kesho tuweze kuipata dira yetu ambayo itatuonyesha njia ya kuelekea huko tunakokutaka.

Mwalimu alituasa, maendeleo siyo vitu, maendeleo ni lazima yawe ya watu. Tulipoanza kushabikia vikwangua anga wakati hatuna udhibiti juu ya wajenzi, makandarasi, vifaa vya ujenzi vya uhakika ikiwemo sementi, vibali vya ujenzi vinavyotolewa kwa misingi ya rushwa na udanganyifu tulishafikiria ya kuwa vikwangua anga ndiyo maendeleo. Tujiandae kwa matukio mengi tu kama haya.

Mungu Ibariki Tanzania!
 

Hee.. Makubwa..!!! Unamhurumia mwenye gorofa kwa kupata hasara..!! Na hao binadamu 34 waliopoteza maisha???
 
Umewezaje kukimbilia kumhurumia mwenye ghorofa kabla ya wahanga? Kumbe hata hujui ni uzembe wa nani still unamhurumia.

Iko hivi, ALIOMBA PERMIT YA GHOROFA 13 badala yake kajenga 16 endelea kumuonea huruma
Ili usimhurumie mwenye ghorofa ni lazima uwe kwanza unajua kilicho nyuma ya pazia. Kama mimi nilikuwa sijui kama aliomba kibali cha ghorofa kumi na tatu akajenga kumi na sita. Lakini hilo pia halitoshi kusema kwamba alipunguza ratios za mchanga na cement au ubora wa nondo ili aongeze urefu hadi ghorofa hizo zote. Siamini. Sidhani kama wewe ndo unajenga nyumba yako utathubutu japo kuongeza mchanga kwenye cement ili upate tofali nyingi zaidi. Naamini utakuwa tayari nyumba ichelewe kuisha lakini ujenge nyumba iliyo bora. Anyway, kikubwa tuwaombee pumziko la amani marehemu, na mwenye ghorofa awahishwe mahakamani mapema iwezekanavyo.
 
Inapendeza kwamba na wewe shabiki namba moja wa CCM leo umeamua kuacha unafiki na kusema ukweli. Ni nini tatizo sasa? Angalia vitu feki vingi vilivyowahi kukamatwa au dhuluma kubwa zilizowahi kufanywa nchini uone kama hutakuta wahusika wake wakubwa ni CCM. Hizi feki nyingi zinaendeshwa na CCM kwa kuwa hawawezi kukamatwa wala kushitakiwa kutokana na uenzetu plus michango yao kwa chama. Hapa ndipo ambapo CCM imetufikisha kwa sasa. Tuna wakati mgumu sana kusema ukweli, hadi CCM ije itoke madarakani tutakuwa tushapoteza uhai wa watanzania wengi sana.
 
Huyu jamaa hata kama anazo pesa ila ujenzi wake ulikuwa ni wa kimaskini. Alafu inaonekana alikuwa hajali masuala ya usalama wa wafanya kazi. Kuna ghorofa lingine mkabala na lile lililoanguka, nasiki yote mmiliki ni mmoja na Mkandalasi ni huyo huyo wa lile lililoanguka.

Haiwezekani unajenja ghorofa 16 alafu unatunia mbao badala ya chuma B/PIPES kutengeneza ule mzunguko wa nje ya jengo sehemu wanapokanyaga mafundi wakati wa kufanya kazi.
 
Mungu mkubwa, lingekuwa limekamilika na kuanza kutumika. Sijui hali ing'ekuwa vipi.
View attachment 88906

Wahanga wengine niwaoneao huruma ni wapangaji ambao tayari walikuwa wamekwisha toa sehemu ya malipo ya pangp (deposit). Japo huwa kuna mikataba inayowezesha marudisho ya malipo yaliyofanywa kabla ya kuhamia katika sehemu iliyolipiwa iwapo kuna badiliko lolote; nina WASIWASIi na MIAKATABA YA NCHI HII (kama ilvyokuwa mingi tuijuayo-kuanzia serikalini hadi kwetu mitaani)
 
Umewezaje kukimbilia kumhurumia mwenye ghorofa kabla ya wahanga? Kumbe hata hujui ni uzembe wa nani still unamhurumia.

Iko hivi, ALIOMBA PERMIT YA GHOROFA 13 badala yake kajenga 16 endelea kumuonea huruma

Kuna watu wanashangaza sana hapa.

Mwingine jana kasema kiurahisi kabisa "watalipwa na bima" kama yeye ndiye case manager wa NIC vile, halafu bila kujali kwamba kuna vitu kama uhai wa binadamu ambavyo havirudishiki kwa bima.
 

binafsi sidhani kama mwenye ghorofa anapaswa kushitakiwa, maana kaajiri maengenia na washauri juu, kama hiyo haitoshi kuna wakaguzi wa majengo wapo wanalipwa hela na serikali
 
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…