Nchi Kavu
JF-Expert Member
- Sep 11, 2010
- 4,271
- 2,401
Inaonekana miaka inavyosogea ndivyo mambo yanavyokuwa hovyo. Hili linathibitishwa na kila mmoja ukimkumbusha miaka ya '80 na early '90. Kikweli miaka ile life ilikuwa tam ukichanganya na uyanki wa primary na sec. Nakumbuka miaka hiyo tukiwinda sana kware kipindi cha masika Moshi huko. Nakumbuka na bar moja ikiitwa kwa soka pale Soweto ilikuwa ikipiga sana vibao vya mbilia beli kama nakei nairobi na tuombe Mungu baba... Sie wakati huo tukicheza kila aina ya mchezo kwenye jengo moja la vigae maarufu kama wailes lililo jirani na bar hiyo. Nikisikia nyimbo hizo nawakumbuka rafiki zangu wote wa utotoni, mambo tuliyofanya, raha iliyokuwepo...machozi yananilengalenga