Good, intellectual and acceptable funeral speech aired out by the pontiff office

Good, intellectual and acceptable funeral speech aired out by the pontiff office

deblabant

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2022
Posts
3,011
Reaction score
4,500
Kardinali Kevin Farrell, Camerlengo wa Chumba cha Kitume, ametangaza kifo cha Papa Francis kutoka Casa Santa Marta kwa maneno haya:

“Ndugu wapendwa, kwa huzuni kubwa ninapaswa kutangaza kifo cha Baba Mtakatifu Francis kilichotokea Saa 1:35 asubuhi hii, Askofu wa Roma, Francis, amerudi kwa nyumba ya Baba. Maisha yake yote yaliwekwa wakfu kwa huduma ya Bwana na Kanisa lake. Alitufundisha kuishi maadili ya Injili kwa uaminifu, ujasiri, na upendo wa wote, hasa kwa ajili ya maskini na waliotengwa. Kwa shukrani kubwa kwa mfano wake kama mwanafunzi wa kweli wa Bwana Yesu, tunakabidhi roho ya Papa Francis kwa upendo wa huruma usio na mipaka wa Mungu mmoja wa Utatu Mtakatifu.”

Papa alilazwa katika Hospitali ya Agostino Gemelli Polyclinic siku ya Ijumaa, Februari 14, 2025, baada ya kuugua bronchitis kwa siku kadhaa.

Hali ya kiafya ya Papa Francis iliendelea kudhoofika, na madaktari wake waligundua kuwa alikuwa na nimonia ya pande zote mbili siku ya Jumanne, Februari 18.

Baada ya siku 38 hospitalini, Marehemu Papa alirudi katika makazi yake ya Vatican huko Casa Santa Marta kuendelea kupata nafuu.

Mnamo mwaka wa 1957, akiwa na miaka ya ishirini mapema, alipata upasuaji nchini Argentina alikozaliwa, ili kuondoa sehemu ya pafu lake iliyokuwa imeathiriwa na maambukizi makali ya kupumua.

Kadri alivyozeeka, Papa Francis alikuwa akipatwa mara kwa mara na magonjwa ya kupumua, hata kufuta ziara iliyopangwa kwenda Umoja wa Falme za Kiarabu mwezi Novemba 2023 kutokana na mafua na kuvimba kwa mapafu.

Mnamo Aprili 2024, Marehemu Papa Francis alikubali toleo jipya la kitabu cha liturujia kwa ajili ya ibada za mazishi ya mapapa, ambacho kitakuwa mwongozo wa Misa ya mazishi ambayo haijatangazwa rasmi bado.

Toleo la pili la Ordo Exsequiarum Romani Pontificis linajumuisha vipengele vipya kadhaa, ikiwa ni pamoja na jinsi ya kushughulikia mabaki ya mwili wa Papa baada ya kifo.

Uhakiki wa kifo hufanyika katika kanisa dogo (chapel), badala ya chumba alichofia, na mwili wake huwekwa mara moja ndani ya jeneza.

Kulingana na Askofu Mkuu Diego Ravelli, Mwalimu wa Ibada za Kitume, Marehemu Papa Francis aliomba ibada za mazishi zirahisishwe na zijikite katika kuonesha imani ya Kanisa katika Mwili wa Kristo Aliyefufuka.

“Ibada mpya,” alisema Askofu Mkuu Ravelli, “inalenga kuangazia zaidi kwamba mazishi ya Papa wa Roma ni ya mchungaji na mwanafunzi wa Kristo, si ya mtu mwenye mamlaka duniani.”

#greenfmUpdates
 
Back
Top Bottom