Wateule
JF-Expert Member
- Sep 17, 2010
- 390
- 368
Akiwa kwenye harakati zake za kampeni kata ya Kibena, jimboni Kalenga, Mgombea Ubunge wa jimbo hilo kwa karata ya CCM, Ndg. Godfrey Mgimwa alisema anajua sheria na kanuni za muajiriwa na yupo pale kibena kuomba wananchi ajira. Sijui wewe unaichukulia vipi kauli hii, binafsi kauli hii imenisikitisha na kunihuzunisha.
Nasema nimesikitika na kuhuzunika, kwasababu kijana Mgimwa anaweka wazi kwamba anatafuta ajira, na si kuwatumikia wananchi katika suala zima la kuwaletea maendeleo, ikiwemo na ajira zao. Wengi mnaweza mkaitafsiri kauli hii tofauti, lakini kikubwa kinachoonekana katika kauli hii ni ubinafsi, ambao ndio kinachoturudisha nyuma mpaka sasa, kwani wanasiasa wengi wamekuwa wanatafuta nafasi za kisiasa kwa lengo la kupata ajira na kujinufaisha na si kwa lengo la kutumikia watu. Najua kwamba unapochagulia katika nafasi fulani ya kiuongozi, tafsiri nyingine ni kwamba umepata ajira,lakini kiongozi bora ni yule anayeomba "kuwatumikia wananchi" wake, na si "kuwaomba ajira". Tofauti ya kuomba "kutumikia wananchi" na "kuomba ajira" ni kwamba ya kwanza inaonyesha ubinafsi na ya pili, inaonyesha kujali na kuthamini wengine. Kwakuwa hatujui haswa lililo moyoni kwa mtu, sheria ya Saikolojia inatutaka tuwe makini na kauli hizi mbili.
Kama mimi ningekuwa ni mpiga kura wa Kalenga(muajiri) leo hii, basi mgombea huyu (muajiriwa) angekuwa ameshindwa usaili(interview), kwani katika Saikolojia ya kutahini waomba kazi, muajiri anakuwa makini sana na kauli za muomba kazi katika kung'amua kwamba muombaji ameweka maslahi ya pesa mbele(mshahara/ajira) au majukumu yaliyo mbele yake? Kama muomba kazi anaonekana ameweka mshahara mbele, basi huyo atakuwa muajiriwa, ambaye ni mzigo, kwani siku zote atakuwa anapigania maslahi yake, badala ya kampuni(wananchi/matatizo yao).
Naomba kuwasilisha,