Godbless Lema ukimbizi: Kaingia jela ya kufikirika

Jidu La Mabambasi

JF-Expert Member
Oct 20, 2014
15,312
24,171
Namhurumia sana Godbless Lema.
Kaingia jela ya kufikirika, jela ambayo ni yeye mwenyewe atajua ni kifungo cha miaka mingapi na atatokaje kwa msamaha wake mwenyewe.

Mbaya zaidi familia nzima imemsindikiza jela hiyo ya kufikirika.

Lema ata enjoy miezi michache ya kwanza huko Canada, pamoja na familia.
Baada ya hapo ndipo ataelewa uzuri na utamu wa Tanzania, maji ya kunywa bure, hewa bure, shule karo za watoto karibu na bure, chakula unarudi kutoka Moshi na mikungu miwili ya ndizi bure!
Mbge ndo usiseme!

Tuliokaa nje muda kidogo tunaelewa jinsi matatizo tuliyo nayo, yalivyotukomaza na kuishi nayo kama ndugu.

Nampa pole Lema maana alisema wanataka kumuua.
Bado angeweza kubaki na kutatua hilo fumbo na shinikizo.

Tanzania ni nzuri!
 
Kama kwenda kuishi Canada ni jela, hebu Canada wakosee waje waseme watu waliochoka kukaa Tanzania waende jela Canada.

Ndani ya mwezi watanzania watakaokuwa wamebaki ni wale wanaotembelea maVX ya umma, na wafanyabishara wachache wenye vipato vikubwa.

Kisha baada ya mwaka wawaulize watanzania walioko jela huko Canada, wangapi wanataka kutoka kifungoni Canada kurudi Tanzania, uone kama kuna mtu atakubali kurudi.
 
True, yet the choice between landing on a rock or in its stead, a hardplace remains neither. As to how credible "his case" REALLY is, the two ASYLUM GIVERS are more INFORMED than narratives richer in fiction propagated by the purported enemy as opposed to FACTS.

IN his place, I would opt for personal SECURITY, and that of my loved ones OVER fantasies and exaggerated harmony of living among watu WANAFKI, WAONGO, WAOGA etc and for that, Machame bananas and mbege notwithstanding!
 
True, yet the choice between landing on a rock or in its stead, a hardplace remains neither. As to how credible "his case" REALLY is, the two ASYLUM GIVERS are more INFORMED than narratives richer in fiction propagated by the purported enemy as opposed to FACTS. IN his place, I would opt for personal SECURITY, and that of my loved ones OVER fantasies and exaggerated harmony of living among watu WANAFKI, WAONGO, WAOGA etc and for that, Machame bananas and mbege notwithstanding!
Case ya Tundu Lissu kupigwa risasi inawapa credibility viongozi wengi wa CHADEMA watakaosema wanatafuta ukimbizi nje.

Sio kama kisingizio tu, kama an actual possibility of political assasination.
 
Namhurumia sana Godbless Lema. Kaingia jela ya kufikirika, jela ambayo ni yeye mwenyewe atajua ni kifungo cha miaka mingapi na atatokaje kwa msamaha wake mwenyewe.

Mbaya zaidi familia nzima imemsindikkza jela hiyo ya kufikirika.

Lema ata enjoy miezi michache ya kwanza huko Canada, pamoja na familia. Baada ya hapo ndipo ataelewa uzuri na utamu wa Tanzania, maji ya kunywa bure, hewa bure, shule karo za watoto karibu na bure, chakula unarudi kutoka Moshi na mikungu miwili ya ndizi bure!

Tuliokaa nje muda kidogo tunaelewa jinsi matatizo tuliyo nayo, yalivyotukomaza na kuishi nayo kama ndugu.

Nampa pole Lema maana alisema wanataka kumuua!

Bado angeweza kubaki na kutatua hilo fumbo na shinikizo.

Tanzania ni nzuri!
We umetoka kwenye nyumba za tembe utakuwa na akili ya kuishi nje kweli? angalia wachaga walivyojazana Ulaya na Marekani
 
Namhurumia sana Godbless Lema.
Kaingia jela ya kufikirika, jela ambayo ni yeye mwenyewe atajua ni kifungo cha miaka mingapi na atatokaje kwa msamaha wake mwenyewe.

Mbaya zaidi familia nzima imemsindikkza jela hiyo ya kufikirika.

Lema ata enjoy miezi michache ya kwanza huko Canada, pamoja na familia.
Baada ya hapo ndipo ataelewa uzuri na utamu wa Tanzania, maji ya kunywa bure, hewa bure, shule karo za watoto karibu na bure, chakula unarudi kutoka Moshi na mikungu miwili ya ndizi bure!

Tuliokaa nja muda kidogo tunaelewa jinsi matatizo tuliyo nayo yalivyotukomaza na kuishi nayo kama ndugu.

Nampa pole Lema maana alisema wanataka kumuua!
Bado abgeweza kubaki na kutatua hilo fumbo na shinikizo.
Tanzania ni nzuri!
Eeenh, 'Jidu'?

Wewe hujakaa nje. Na kama umekaa nje, basi ulijiweka jela wewe mwenyewe, bila ya kulazimishwa na yeyote.

Hivi unazungumzia jela? Kuna jela zaidi ya uliyomo sasa? Hata kama wewe ni waziri, au mkuu wa mkoa fulani; hivi kweli unajihisi kwamba upo HURU; unajuwa maana ya kuwa huru kweli!

"Maji ya bure, mikungu ya ndizi..." hivi kweli hivyo vitu ndiyo thamani ya utu wako?

Nijuavyo elimu ya Canada haina wasiwasi kwa watoto, sijui utaanzia wapi kuwahurumia watoto wale kwa kukosa elimu inayotambulika dunia nzima. Ungekuwa ni mmojawapo wa mazezeta wengi wanaofahamika hapa ukumbini, nisingehangaika kujibu upotofu huu ulioweka hapa. Lakini najua wewe ni mtu mwenye fikra nzuri.

Umenisikitisha sana na mada yako hii, kwa sababu ninakutambua kuwa mtu mwenye uelewa wa kutosha, hata kama ni mpenzi tu wa hilo lichama lililopoteza mwelekeo kabisa.

Kuna watu wanafurahia kuwa 'mateka' kwa kupewa vitu tu, a,mbavyo ni haki yao? POLE SANA.

Kabla hujaanza kumhurumia Lema na familia yake, jaribu kujihurumia wewe na waTanzania kwa ujumla kwa hii jela ya umateka tuliyojaliwa kuwa nayo. Hatujui kikomo chake ni lini.
 
Back
Top Bottom