Godbless Lema: Nimeambiwa na Mungu

Godbless Lema: Nimeambiwa na Mungu

Ccm na wafuasi wao wote wanamwogopa mheshimiwa Lema kiasi kwamba kila kukicha wanatafuta ni mtu gani ndani ya chama chao anaweza kumshinda Lema na kuirudisha Ccm madarakani? Lakini kila wafanyalo haliswihi.
 
Mh Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema akihutubia kwenye mkutano wa hadhara kata ya Elerai.

Mh Lema alianza kwa kusema meya na madiwani wa jiji wataendelea na shughuli za kuimarisha upatikanaji wa huduma za jamii kama hospitali, shule, maji na mikopo kwa wnawake na vijana.

Aliendelea kusema kuwa huduma za jamii sio hisani ni haki ya binaadamu hivyo watu wa Arusha msidhani tunapoboresha miundombinu, maji, huduma za afya n.k ni kwaajili ya kampeni in wajibu wetu kufanya hivyo. Wananchi haya tunayoyafanya sio hisani ni wajibu wetu kwenu, alisema Mh Lema.

Hatahivyo mh Lema alisisitiza kazi kubwa iliyombele yake ni kusababisha wananchi kuwa jasiri kudai haki yao na kutoonewa wala kudhalilishwa utu wao. Ungeniuliza mimi nini nafanya kwa sasa, ningesema kubwa ni kusababisha wananchi wangu kudai haki yao na kulinda utu wao na madiwani wangu fanyehivyo pia alisema mh Lema

Pia amewaagiza madiwani kuendelea kuwajenga wananchi kujua haki zao na kulinda utu wao kwa garama yeyote. Ndugu wananchi kwasasa mambo ni kupangua hoja papo kwa hapo (tit for tat) madiwani msidhalilishwe mkaogopa kukemea uovu kwasababu eti ni mheshimiwa na utaonekanaje, sema kweli alisisitiza mh Lema

Katika kuhitimisha mh Mbunge alishangazwa na ukimya wa viongozi wadini katika mambo yanayoendelea nchini mfano kuzuiwa kwa mikutano ya hadhara, maaskofu, masheikh msisubiri maafa yatokee ndio mkemee uovu, leo wanaona kukatazwa mikutano ya hadhara ni ya wanasiasa, lakini iko siku viongozi wadini watatakiwa kwenda kueleza wanaenda kuhubiri nini madhabahuni nadhani hapo ndipo watutuelewa alisema mh Lema
View attachment 422261
Mbona sijaona alipoambiwa na Mungu?
 
Lema dini waachie wengine wewe usihubiri kabisa kwasababu ulishatuambia Mungu kakueleza ni ruksa kumzomea Lowasa baadae ukasahau uliagizwa na Mungu ukatuambia Lowasa ni malaika sasa hivi watakao kuelewa ni wale vipofu , hawa wakazi wapo wenye nguo ya rangi ya kijani ama wale wenye magwanda ya khaki sisi tusio amini watu kama ninyi hatutakuelewa hata kidogo.....
Mkuu kumbuka kuna Mungu na miungu! Yeye huenda anaambiwa na miungu.
 
Luther King Jr.
"Ni maoni yangu kwamba yeyote anayevunja sheria ambayo nafsi yake inamtuma kuwa ni dhalimu, na ambaye yu tayari kukabiliana na adhabu yeyote kwa kitendo hicho chenye lengo la kuamsha hisia za watu juu ya sheria dhalimu,anaonyesha utiifu wa hali ya juu kwa sheria"Maneno haya yalitamkwa Aprili 16, 1963 na mwanaharakati maarufu wa zamani wa haki za weusi katika Marekani.Dk.Martin Luther King Jr.
 
inichome nini sasa, kama kweli ni mtu wa Mungu ya nini kupayuka hadharani kisa hujatajwa kwenye orodha ya wafanikishaji wa mradi? lip anahofia kama yeye ni mtu wa Mungu
Mkuu kwa mwana siasa kutajwa ina maana kubwa sana, huyo aliye kataa kumtaja alikuwa na lengo la kuharibu mahana hiyo. Na kama hakukuwa na umuhimu wa kutajwa kwanini wengine walitajwa?
 
inichome nini sasa, kama kweli ni mtu wa Mungu ya nini kupayuka hadharani kisa hujatajwa kwenye orodha ya wafanikishaji wa mradi? lip anahofia kama yeye ni mtu wa Mungu
wewe unaona kutokutajwa ni ishu ndogo sababu hujui impact yake
 
Mtakaa sana! Na miungu MTU wenu Lemas aliyekunywa tope la bangi miaka ya 1982 ndo linaendelea kumsumbua hadi sasa!
 
uzuri wa lema pamoja na mapungufu yake toka mwaka 2010 hajabadilika. ni yuleyule....
 
Uchaguzi wa Mayor Kinondoni uliokua ufanyike ukumbi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni umevurugika kutokana na kasoro kadhaa zilizojitokeza kama ifuatavyo:

1. CCM walikua wanazidiwa madiwani na UKAWA, kwahiyo wakaamua kuleta wabunge wanne walioteuliwa na Rais kupiga kura kama madiwani wa Kinondoni kinyume na utaratibu. Wabunge hao ni Dr.Tulia Akson, Prof.Joyce Ndalichako, Balozi Augustine Mahiga, na Prof.Makame Mbarawa.

Madiwani wa UKAWA wamepinga ushiriki wa wabunge hawa kwa sababu Sheria ya vyama vya siasa ya mwaka 1992, na sheria ya serikali za mitaa ya mwaka 1982 kwa pamoja haziruhusu wabunge zaidi ya watatu walioteuliwa na Rais kupiga kura kwenye Halmashauri moja. Kwahiyo kitendo cha CCM kuleta wabunge wanne, wakati maximum ni watatu ni kinyume cha sheria.

2. Wabunge wawili Prof.Joyce Ndalichako na Balozi Dr.Augustino Mahiga walishaapa kama madiwani wa Halmashauri ya manispaa ya Ilala, sasa iweje wapige kura Kinondoni wakati waliapia Ilala?

3. Mbunge wa Viti Maalumu Kinondoni (CHADEMA) Mhe.Suzan Lyimo ameondolewa kwenye kikao kinyume na utaratibu ili asiweze kupiga kura.

4. Mkutano mkuu wa uchaguzi uliitishwa chini ya saa 24 kinyume na sheria za serikali za mitaa zinazotaka mkutano mkuu kuitishwa angalau masaa 72 kabla. Barua ya mkutano wa leo iliandikwa jana na Mkurugenzi wa Manispaa hiyo ikieleza kuwa kikao ni leo (less than 24 hours hours).

KILICHOTOKEA:
1. Madiwani wa UKAWA wametoka nje na kuungana na wafuasi na wanachama waliokua nje ya ukumbi huo kuelekea Makao makuu ya CHADEMA (Kinondoni) ambapo Mwenyekiti wa Taifa Mhe.Freeman Mbowe atafanya mkutano na vyombo vya habari.

2. Madiwani wa CCM wamebaki ndani lakini wameshindwa kuendelea na mkutano huo maana akidi haijatimia. Kanuni zinataka angalau 2/3 ya wajumbe kuwepo ili kikao kiwe halali. Na 2/3 ya wajumbe wa leo ni angalau madiwani 24. Lakini madiwani wote wa CCM (including wabunge wanne wateule wa Rais) wapo 18 tu, jambo ambalo limewafanya kushindwa kuendelea na mkutano huo
 
Ni heshima kwa Mungu kumzomea fisadi Lowasa --------@ Lema
 
Back
Top Bottom