Godbless Lema: Nimeambiwa na Mungu

Godbless Lema: Nimeambiwa na Mungu

Mtu mwenye historia ya kuchukua viisyo vyake kwa nguvu, hasa vifaa vya moto, anapoanza kuongea na Mung bila kutubu hadharani , ujue ndo wakati wa kuchunga mzigo wako!!!
Toba ni mambo binafsi kati ya mwanadamu na Mungu wake! Ulitaka mtu anayeomba toba aitishe mkutano wa hadhara?
 
Namku
Mh Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema akihutubia kwenye mkutano wa hadhara kata ya Elerai.

Mh Lema alianza kwa kusema meya na madiwani wa jiji wataendelea na shughuli za kuimarisha upatikanaji wa huduma za jamii kama hospitali, shule, maji na mikopo kwa wnawake na vijana.

Aliendelea kusema kuwa huduma za jamii sio hisani ni haki ya binaadamu hivyo watu wa Arusha msidhani tunapoboresha miundombinu, maji, huduma za afya n.k ni kwaajili ya kampeni in wajibu wetu kufanya hivyo. Wananchi haya tunayoyafanya sio hisani ni wajibu wetu kwenu, alisema Mh Lema.

Hatahivyo mh Lema alisisitiza kazi kubwa iliyombele yake ni kusababisha wananchi kuwa jasiri kudai haki yao na kutoonewa wala kudhalilishwa utu wao. Ungeniuliza mimi nini nafanya kwa sasa, ningesema kubwa ni kusababisha wananchi wangu kudai haki yao na kulinda utu wao na madiwani wangu fanyehivyo pia alisema mh Lema

Pia amewaagiza madiwani kuendelea kuwajenga wananchi kujua haki zao na kulinda utu wao kwa garama yeyote. Ndugu wananchi kwasasa mambo ni kupangua hoja papo kwa hapo (tit for tat) madiwani msidhalilishwe mkaogopa kukemea uovu kwasababu eti ni mheshimiwa na utaonekanaje, sema kweli alisisitiza mh Lema

Katika kuhitimisha mh Mbunge alishangazwa na ukimya wa viongozi wadini katika mambo yanayoendelea nchini mfano kuzuiwa kwa mikutano ya hadhara, maaskofu, masheikh msisubiri maafa yatokee ndio mkemee uovu, leo wanaona kukatazwa mikutano ya hadhara ni ya wanasiasa, lakini iko siku viongozi wadini watatakiwa kwenda kueleza wanaenda kuhubiri nini madhabahuni nadhani hapo ndipo watutuelewa alisema mh Lema
View attachment 422261
Namkubali sana Mh. Lema.
Angalau anafanya kazi inayoonekana Jimboni kwake tofauti na wenzake.
Hongera sana Mh. Lema, kwa sasa jaribu kumwomba Mwenyezi Mungu akupunguzie hasira na kuwa na moyo wa kiasi katika kushirikiana na viongozi serikalini.
 
Arusha walikuamini, wanakuamini hakuna wa kutubabaisha piga kazi kelele muachie GAMBO anaedandia gari kwa mbele.
 
inichome nini sasa, kama kweli ni mtu wa Mungu ya nini kupayuka hadharani kisa hujatajwa kwenye orodha ya wafanikishaji wa mradi? lip anahofia kama yeye ni mtu wa Mungu
Na Mimi namshangaa analitaja jina la MUngu bure ndio maana nuksi na mikosi kwenye ubunge wake haiishi yeye afanye siasa viongozi wa dini awAACHE NA KAZI ZAO ZA KIDINI ASIWAINGILIE
 
Viongozi wa dini wamkemee grand mopao? Haitatokea,thus why mimi hua nasema ni wanafiki sana
 
Hapa ndo naamini kua mtu hawezi kukudanganya mpaka awe amekudharau.....Lema amekwisha wadharau watu wa arusha ndio maana haoni shida wala ajabu kuwadanganya.
 
Lema anasafiria nyota ya Gambo! Bila kulia lia siku ile mkutano ungekua na watu wawili yaani yeye na mkewe! Hapo watu walikwenda kusikiliza umbea tu wa siku ile ya mtifuano wakawasimulie wengine na sio kwakua analo la maana la kuwaambia!
 
Lema anasafiria nyota ya Gambo! Bila kulia lia siku ile mkutano ungekua na watu wawili yaani yeye na mkewe! Hapo watu walikwenda kusikiliza umbea tu wa siku ile ya mtifuano wakawasimulie wengine na sio kwakua analo la maana la kuwaambia!
Haya tuma salamu kwa fisi wenzako 20.
 
Kabadilishe taratibu za ibada kwanza, na huyo jambazi kwanini hammpeleki mahakamani huoni kama unadhalilisha serikali yetu pendwa?
Taratibu za Ibada haziwezi kubadilishwa kukidhi matakwa ya jambazi asiyetubu.
 
Viongozi wa dini walishawaona chadema wanafiki tu,huo udikteta mbona hatuuoni au ni kitu cha kufikirika.endeleeni na movement yenu ya UKUTA isiyo na kichwa wala miguu. Lema ana tabia za ushari (tabia za watoto wa mitaani).Mbona Pro.J anapiga kazi kimya jimboni kwake tena anapata sapoti kubwa toka kwa madiwani wa CCM ambao ndo wengi jimboni kwake na kaamua kuachana na wale wa upande wa pili baada ya kuwabaini ni wazushi tu wapika majungu
 
Back
Top Bottom