Nimekuwa nafuatailia siasa za hiki Chama takribani miaka ishirini iliyopita. Kama sikosei hiki chama nafasi ya Mwenyekiti imewahi kuwa na wenyeviti watatu ambao wawili kati yao ni mtu na Mkwe wake yaani Freeman Mbowe na Mzee Edwin Mtei.
Kutokana na kelele nyingi saana toka ndani ya chama kutaka awepo mwenyekiti mwingine asietokana na uridhi wa kindugu, Mwenyekiti ambaye kwa sasa yupo mahabusu amekuwa na mawasiliano ya karibu saana na baadhi ya viongozi wa kanda wa chama kwa nia ya kuhakikisha ya kwamba mrithi wake anatokana na safu wa viongozi wa kanda waliopo. Msingi haswa wa kutaka viongozi wa kanda ni kutaka kuhakikisha ya kuwa mheshimiwa Lissu ambae ni Makamu Mwenyekiti hataweza kumrithi Mheshimiwa Mbowe kwenye uachaguzi ujao wa chama.
Wadadisi wa maswala ya uchaguzi wanaamini ya kwamba kwa viongozi wa Kanda waliopo kwa sasa, Mrithi halisi na ambae aataweza kuendeleza dhana ya chama (chgga kwanza) ni Mheshimiwa Godbless ambae amekuwa active saana kwenye mitandao ya kijamii kwa nia ya kuhakikisha ya kwamba anaonekana na vijana wa chama kuwa ni jasiri na SHUPAVU hivyo anaweza kuwa mtu sahihi kumrithi kaka mheshimwa Mbowe ambae ni binadmu yake LEMA.
Nawasilisha wakuu