KAMA KAANDIKA YEYE , LEMA INABIDI AKUE.
Anaandika Mwana UKAWA Halisi.
Nimesoma waraka mmoja ulioandikwa kwa kukoseakosea ikidaiwa kwamba umeandikwa na Mbunge wa Arusha Ndugu Godbless Lema.
Kiini cha andiko lake ni malalamiko ya kwamba eti Mrisho Gambo alizuia yeye kuongea pale uwanjani wakati wa kuaga miili ya wanafunzi, walimu na dereva wa shule ya Lucky Vincent.
Kwanza kabisa sina hakika kama Lema ndio ameandika uozo ule. Yani Lema hajui hata kuandika umuhimu anaandika UMUJIMU? . Hilo ni kosa moja tu kati ya mengi kunifanya nidhani watu wanamsingizia Lema ili aonekane ngumbalo mbele ya wanaoelewa miiko ya na Itifaki katika Uongozi.
Lakini kama aliyeeandika ni Lema, yabidi Lema akue sasa ; na tena atafutiwe mshauri wa saikolojia pengine akili yake imevurugika kutokana na shida za mahabusu.
Ule msiba HAUKUWA MSIBA WA JIMBO LA ARUSHA. Japo ulikuwa wa Taifa zima , pengine tungehusisha Mkoa mzima wa Arusha moja kwa moja ( Kiongozi wa juu katika Mkoa ni Mrisho Gambo ambaye aliongoza zoezi zima ). Kwanini Lema alazimishe kwamba yeye ndio ana uwakilishi wa wafiwa kuliko hata wazazi wa marehemu ?
Kwenye lile andiko lililoitwa la Lema, kuna mstari anadai kwamba " CHADEMA hawatakiwi kuongea ". Yani Lema alianza ubaguzi kabla ya siku ya tukio kusema Chadema hawaongei ( kaleta ubaguzi wa vyama, alipokuta Mbowe anaongea akaendeleza Ubaguzi wa kumbagua M/Kiti wetu Mbowe kwamba yeye hakustahili kuongea). Kama ni hivyo mbona MBOWE alipewa nafasi ya kuongea? Au Mbowe ni CCM?. Yaani Lema ameanza kumbagua M/kiti wetu Mbowe kwa kuona kwamba hakuwa na haki ya kuongea kwenye hadhara ile na yeye ndo alistahili?
Mbowe alizungumza kwa niaba ya CHADEMA na KAMBI YA UPINZANI. Kuzingatia itifaki ilikuwa lazima iwe hivyo. Ukisema azungumze Mbowe halafu azungumze Lema kwa sababu yeye ni Mbunge, baadae tungesema baasi aongee na Meya, na pia waongee madiwani wa kata zote zenye msiba, tushuke tena waongee wenyeviti mpaka wajumbe wa mitaa na baadae waongee wazazi ( Aongee kila mtu kwa sababu Ule msiba uliwahusu wengi moja kwa moja ).
Lema inabidi akue ( kama yeye ndio aliandika vile ) na afundishwe somo la Itifaki. HUWEZI KUTOA NAFASI KWA KILA MTU WANAPOKUWA VIONGOZI WENGI VILE.
Uongo mwingine ni kusema jina lake lilikuwepo kwenye Ratiba ; Ratiba ipi?. Anataka kusema Gambo kabadili ratiba pale jukwaani?. Kubadili vipengele vichache inawezekana kwa sababu ya muda na sababu nyingine ndogondogo. Lakini Lema aache siasa za kutafuta huruma ya wananchi kwa sababu siku zote inafahamika Gambo ni mbabe wake. Gambo ni mbabe kwa Lema lakini sio katika jambo kama lile na asingweza kufanya ujinga huo mbele ya Makamu wa Rais. Tulimuona Mbowe akiteta jambo na Makamu wa Rais, kama ishu ingekuwa kushtaki kwamba Gambo anabadili ratiba ni hakika Makamu wa Rais asingekubali ujinga huu ( hilo hata Lema analifahamu ).
MWISHO : Kama Lema ndio kaandika uozo ule, yabidi akue na kuacha tabia ya kulalamika na kutafuta kiki hata kwenye misiba. Afundishwe somo la itifaki na kama anataka kuuza sura kuongea kwenye maeneo kama yale, agombee Uenyekiti wa CHADEMA au amuambie Mbowe asiwe anahudhuria maana anamzibia shavu la 'Kuuza Sura '.
Ameandika MWANA UKAWA HALISI.