Godbless Lema: Mkijua jinsi Mungu alivyonibadilisha kupitia gereza mtatamani muende gerezani

Francis12

JF-Expert Member
Sep 30, 2016
7,533
22,278
Mbunge wa Arusha na mjumbe wa Kamati Kuu Chadema Godbless Lema leo akiongozana na mkewe na wanae ametoa sadaka ya shukrani kwa Mungu ndani ya kanisa la Winners Arusha.

Lema ametoa sadaka hiyo ya shukrani ikiwa ni siku mbili tu tangu aachiwe kwa dhamana baada ya kuzuiliwa gerezani kwa miezi minne.

Akizungumza mbele ya umati wa waumini mbunge huyo amesema hana kinyongo na yeyote aliyekusudia mabaya dhidi yake.Amesema wakati maadui zake wakikusudia mabaya dhidi yake kwa upande mwingine Mungu alikusudia mema kwake.

Mbunge huyo ambaye alilakiwa kama mfalme na wananchi alipotoka gerezani kwa kutandikiwa kanga ili apite juu yake amesema akiwa gerezani kila siku alikuwa anasali masaa manne mfululizo bila kuchoka.

Amesema katika maombi yake alikuwa anaombea Taifa,wabunge,viongozi na Rais John Pombe Magufuli.Lema amesema alichofundishwa na Mungu akiwa gerezani ni kuwapenda maadui na kuwaombea mema wale wanaomtakia mabaya.

Amesema anamshukuru sana Mungu kwani amembadilisha mno akiwa gerezani na yeye siyo yule Lema wa zamani.

Mbunge huyo maarufu kama Mandela wa Tanzania alikuwa akishangiliwa sana na waamini huku wengine wakibubujikwa na machozi ya furaha huku wakimtukuza Mungu.

Mbunge huyo mara baada ya Ibada amerejea nyumbani huku akitarajiwa kukutana na kada mpya na maarufu wa chama hicho Wema Sepetu kwa majadiliano maalum
 

Attachments

  • tmp_14243-VID-20170305-WA0061-651355862.mp4
    13.9 MB · Views: 55
Duh!
Wakapate utakaso kwa kupitia "tanuri la moto"?
...1:tunasubiri ona hayo mabadiliko
...2:tunamuonya Lusinde, mara hii ukileta tafitafi ya yaliyojiri "mazabe" kama ulivyoimwaya hadharani mwaka ule, kwenye kampeni za uchaguzi uliomuingiza Nassari mjengoni kwa mara ya kwanza, utatuudhi....na "hatutakusikiliza"...
 
Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini Godbless Jonathan Lema akitoa neno la shukrani kanisani leo jumapili amesema Mkijua jinsi Mungu alivyonibadilisha kupitia gereza mtatamani muende gerezani.


Nimeipenda.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
msomaji wa biblia utamjua tu kwa jinsi anavyotafuta sura huyu lema ni mmoja wapo ukiitazama hii video utagundua.
"kumcha mungu ni chanzo cha maarifa" mungu aendelee kukulinda kamanda
 
msomaji wa biblia utamjua tu kwa jinsi anavyotafuta sura huyu lema ni mmoja wapo ukiitazama hii video utagundua.
"kumcha mungu ni chanzo cha maarifa" mungu aendelee kukulinda kamanda
Lema ni mtumishi wa Mungu .magu anatakiwa kujirekebisha
 
Akizungumza mbele ya umati wa waumini mbunge huyo amesema hana kinyongo na yeyote aliyekusudia mabaya dhidi yake.Amesema wakati maadui zake wakikusudia mabaya dhidi yake kwa upande mwingine Mungu alikusudia mema kwake.
[/MEDIA]

Hili kanisa nalo tuliunganishe na KKKT la Kimara au hili halifanyi siasa?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom