Mariam Ditopile amlipua Lema, amtaka ajitokeze kuomba radhi

JUMA JUMA

JF-Expert Member
Jan 5, 2013
666
835
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Dodoma Mhe Mariam Ditopile amemtaka aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Godbless Lema ajitokeze aombe radhi kutokana na kauli yake aliyoitoa kuhusu Vicoba ambayo ni yakuwadhihaki wanawake.

Katiba hotuba yake Lema alikaririwa akisema Vicoba ni umasiki na ndio maana alimwondoa mkewe kwenye benki hizo.

Ditopile ametoa wito huo alipo kuwa mgeni rasmi katika kongamoano la Vicoba na kumpongeza Rais Dk.Samia Suluhu Hassan kwa kutimiza miaka miwili madarakani liloandaliwa na Shirika la Msaada wa Kisheria (JUST).

“Kama kweli tunataka kurekebisha pale ambapo serikali imekosea basi tuwe na lugha nzuri,kama kuna mtu anaona vikoba havifai basi aje na hoja zake sio kudharau kwasababu wapo wanawake wengi wanaendesha shughuli zao kupitia fedha hizo kidogo."

Amesema “Ndugu yangu huyu Godbless Lema kiukweli ametumia lugha ambayo imetudhihaki sisi wanawake na inawezekana hata mama yake alikuwa ni miongoni na kama anahoja aishauri serikali."

"Mimi namuomba ashuke chini akafuatilie vikoba hivi ni kwa namna gani vimeinua maisha ya watanzania ajifunze na kama anaona kuna sehemu ya kujirekebisha aseme, ikiwezekana atoke na afute kauli yake kwasababu ametukosea sana, asitumie uhuru vibaya aliopewa na Rais Dkt. Samia."

Ditopile amesisitiza kuwa uanzishwaji wa huduma ndogo za fedha upo kwa mujibu wa sheria ambayo ilitungwa wakati Godbless Lema akiwa Mbunge.

Alisema wizara ya fedha ilitunga sheria ya huduma ndogo za fedha mwaka 2017 lengo ni kuhakikisha huduma hiyo inaleta tija kwa wananchi.

IMG-20230313-WA0985.jpg
IMG-20230313-WA0979.jpg
IMG-20230313-WA0978.jpg
IMG-20230313-WA0976.jpg
 
Kwa wasiomjua huyu maria ditopile, ni mtoto wa kada mkubwa wa CCM, aliyewahi kuwa mkuu wa mkoa wa Dar, Ukiwaona Ditopile Mzuzuri, kwa sasa ni marehemu, akiwa mkuu wa mkoa mstaafu, daradara lilimchomekea akashuka akampiga dereva risasi ya kichwa akafa hapo hapo na yeye alikuja kufia gest akiwa na mchepuko,
Huyu maria, hajuhi shida, hajasomeshwa na vicoba, vicoba ni katika hari ya kutapatapa tu maisha.
 
Waanze wao familia nzima kuomba Msamaha kwa baba yake kumpiga risasi dereva bajaji amabaye hakuwa na hatia pale Kawe. Hata kama alikuwa nayo haikuwa sahihi kumpiga risasi hadi kufa wakati sheria iko wazi.
Dereva bajaji tena????

Ova
 
Huyu mtu hajui kuwa vicoba ni katika hali ya kuganga ganga njaa kama ilivyo bodaboda.........shughuli za kuganga ganga ambao hazina tija kubwa kwenye maendeleo ya watu na nchi haziwezi kuchukuliwa kama kipaumbele cha nchi. Hawa watu wanajaribu kutafuta sympathy kwa haya makundi badala ya ku-address hoja za Lemma, hopeless!!​
 
Ila Lema angetumia kauli nzuri, huenda ana tatizo la akili, alianza na "bodaboda ni laana", ugali unadumaza akili. Akili za wazazi wake zingedumaa basi Lema hangekuwepo.
 
Ulipomuita Mh. Ditopile moto wa muuaji positivity energy ilikuwa inakuimarisha Ili nikupe hongera! Pumbavu!!!
[/QUOTE
Aliyeita Vicoba umaskini na aliyetaka watu waombwe radhi wote wapo sehemu wanajiandaa na ajenda zao. Nikutakie kazi njema mkuu katika ujenzi wa taifa.
 
Back
Top Bottom