Godbless Lema: Kuna siku mtavililia vyama vya Upinzani viwasemee hamtavipata

Leo hii CCM inaoomba CDM ipelekee wabunge wa viti maalum! Kweli anayecheka mwishoni ndio anafurahia kicheko..
 
Anaandika GODBLESS J. LEMA (MB) Arusha

Vuta Picha Vyama vyote vikafutwa katika kipindi hiki kikabaki CCM tu chama ulichonacho wewe.

Then hao uliokua unawaona hawafai akina Mbowe, Mdee, Heche, Nassary, Lema n.k wakaona ni UJINGA KUFA unatetea watu wasiojua kujisaidia wenyewe. Wakajiuliza Kwani tunakwama wapi? Acha na sisi tukaungane na CCM mtesi wao na sisi tuishi vizuri tu.

Then Wabunge wote katika Majimbo yote wakatokea CCM kila kitu kikaamuliwa ndani ya Chama.

Mbowe akasaidiwa kujenga Bilcanas mpya maisha yakaendelea kama tunavyoona watu wanasamehewa kubomolewa nyumba zao wakijiunga na CCM.

Mbowe, Mnyika, Lijualikali tayari wanatambulika na system ya Uongozi hapa nchini. Kama DC wa Dodoma anaejitambua kama karai amepata vipi hawa wenye makarai yao watakosa?

Then fikiria wewe Mtanzania wa kawaida utaishije na atakusaidia nani tena kuhoja kuhusu pesa yako?

Kama walipokuwepo watu wa kuhoji pesa yako bado walikua watu wanakula kwa kujificha japo kweli zinaliwa. Vipi wakikosekana?

Hivi mshawahi kufikiria madhara ya hizi Juhudi za Kudhoofisha Upinzani au huwa mnashangilia tu?

Mtaishi kama "Mbwa Koko" na hutatambulika tena kama mfuasi wa CCM watatambuana viongozi kwa viongozi. Who is going to deal with you?

Leo Viongozi wa CCM wanawanyenyekea kidogo wananchi ni kwa sababu wanajua kuna Uchaguzi awamu ijayo.... Na Pengine Jimbo likaenda Upinzani. Ikibaki CCM pekeake nani atakunyenyekea wewe? Nani atakuja kujua hata unaishije?

Mshafikiria?

Hamtamuona Polepole tena! Anakuja kueneza nini? Watakua ofisini tu wakilipana mishahara. Watawachagulia kila kitu na hakuna cha kuwafanya.

Mshafikiria?

Ni ngumu kuelewa kwa kuwa haijatokea na mnaangalia leo tu.

Huwa natamani hii hali itokee hata kwa muda wa mwezi mmoja tu.

Mtakopwa hadi mishahara mtasema wapi? Nani atawapigania kipindi hicho hata kina Lissu wanakula mema ya nchi tu.

Hicho ndo kipindi hata ajira mpya kuna zingine itabidi wapate kwanza watoto wa viongozi na wengine mtapata zitakazobakia.

Hicho ndo kipindi mtapigwa hadi fimbo makazini, nadhani Dalili za Makofi zimeanza na hakuna wa kuwatetea.... Ukienda kushtaki makahamani unawakuta wale wale. Unapeleka kesi na unafungwa wewe. Wa kupiga kelele itakua ni familia yako tu wengine wote wanaogopa.

Akina Mbowe kipindi hicho watakua wanakula kuku kwa mirija tu.

Mtawaita na hawataitika tena. Ipo sababu kubwa sana ya Kuilinda Demokrasia na vyama Vya Upinzani. Walioianzisha na Kuitetea kwa Damu hawakua wajinga they focused on their future.

Hatubembelezani hapa kuilinda demokrasia ya kweli maana kesho ni yetu sote.

Kila Unachotaka kukishabikia kipime kwanza madhara yake ya baadae.

Watu mnatamani vyama vya Upinzani vyote vife au vifutwe ila ipo siku mtavililia na hamtavipata.

Tafakari

Siku njema
Kukimbia nchi ni ishara kwamba vita vimekushinda...kama angekuwa mwanaharakati wa kweli basi angebaki hapa nchini apiganie anachokitaka siyo kusingizia kuwa wanataka wamuue kumbe amekimbia madeni.
 
Kukimbia nchi ni ishara kwamba vita vimekushinda...kama angekuwa mwanaharakati wa kweli basi angebaki hapa nchini apiganie anachokitaka siyo kusingizia kuwa wanataka wamuue kumbe amekimbia madeni.
Ulikuwa kwenye mfumo kila siku mahabusu na mahakamani sasa ukiwa nje ya mfumo si kunyongwa hivyo vita utavipigania kaburini au ahera????
 
Ulikuwa kwenye mfumo kila siku mahabusu na mahakamani sasa ukiwa nje ya mfumo si kunyongwa hivyo vita utavipigania kaburini au ahera????

Wapinzani wote ni waongeaji wazuri tu wa hoja...kwa hiyo kama ni hivo basi wapinzani wote wangekimbia nchi....walishindwa kukuua ukiwa kwenye mfumo leo hii wahangaike na roho yako ya nini wakati hauko kwenye mfumo tena so utawasumbua kwa lipi
 
Mlichokua mnakitaka kimewashinda sasa mnatafuta pakutokea komaeni na hao covid 19 mwonekane mnawajali wapinzani taifa lililo sahau ustaarabu wa kanuni na taratibu za nchi kwa kisingizio cha uzalendo wa kumwabudu mtu mmoja CHATO EMPIRE.
 
Uliishia darasa la ngapi mkuu shule !!! 🤔🤔🤔

Mungu akuhurumie bure
 
Uliishia darasa la ngapi mkuu shule !!! 🤔🤔🤔

Mungu akuhurumie bure
Shule au elimu yangu inakuhusu?? Mbona unashindwa kujibu hoja unaanza upumbavu wa kuhoji elimu kuandika na kusoma kunaonyesha nimesoma sema lingine kama huna akili.
 
Huyu naye wanajiona kama ndo wanajua kuwaamulia watanzania wanachotaka. Hayo yakitokea tutaingia roads bila msukumo kijana. Mbona ulisema Uko tayari kwa lolote afu ukakimbiilia Nairobi. Unitumie mtaji Wa watanzania ili kujinufaisha.kwani viti maalumu Mbowe hakuwekaga Dada zake wote ama bado wengine hawajasoma mpaka Leo hii.
 
Back
Top Bottom