Godbless Lema: Kuna siku mtavililia vyama vya Upinzani viwasemee hamtavipata.

Quinine

JF-Expert Member
Jul 26, 2010
18,667
2,000
Anaandika GODBLESS J. LEMA (MB) Arusha

Vuta Picha Vyama vyote vikafutwa katika kipindi hiki kikabaki CCM tu chama ulichonacho wewe.

Then hao uliokua unawaona hawafai akina Mbowe, Mdee, Heche, Nassary, Lema n.k wakaona ni UJINGA KUFA unatetea watu wasiojua kujisaidia wenyewe. Wakajiuliza Kwani tunakwama wapi? Acha na sisi tukaungane na CCM mtesi wao na sisi tuishi vizuri tu.

Then Wabunge wote katika Majimbo yote wakatokea CCM kila kitu kikaamuliwa ndani ya Chama.

Mbowe akasaidiwa kujenga Bilcanas mpya maisha yakaendelea kama tunavyoona watu wanasamehewa kubomolewa nyumba zao wakijiunga na CCM.

Mbowe, Mnyika, Lijualikali tayari wanatambulika na system ya Uongozi hapa nchini. Kama DC wa Dodoma anaejitambua kama karai amepata vipi hawa wenye makarai yao watakosa?

Then fikiria wewe Mtanzania wa kawaida utaishije na atakusaidia nani tena kuhoja kuhusu pesa yako?

Kama walipokuwepo watu wa kuhoji pesa yako bado walikua watu wanakula kwa kujificha japo kweli zinaliwa. Vipi wakikosekana?

Hivi mshawahi kufikiria madhara ya hizi Juhudi za Kudhoofisha Upinzani au huwa mnashangilia tu?

Mtaishi kama "Mbwa Koko" na hutatambulika tena kama mfuasi wa CCM watatambuana viongozi kwa viongozi. Who is going to deal with you?

Leo Viongozi wa CCM wanawanyenyekea kidogo wananchi ni kwa sababu wanajua kuna Uchaguzi awamu ijayo.... Na Pengine Jimbo likaenda Upinzani. Ikibaki CCM pekeake nani atakunyenyekea wewe? Nani atakuja kujua hata unaishije?

Mshafikiria?

Hamtamuona Polepole tena! Anakuja kueneza nini? Watakua ofisini tu wakilipana mishahara. Watawachagulia kila kitu na hakuna cha kuwafanya.

Mshafikiria?

Ni ngumu kuelewa kwa kuwa haijatokea na mnaangalia leo tu.

Huwa natamani hii hali itokee hata kwa muda wa mwezi mmoja tu.

Mtakopwa hadi mishahara mtasema wapi? Nani atawapigania kipindi hicho hata kina Lissu wanakula mema ya nchi tu.

Hicho ndo kipindi hata ajira mpya kuna zingine itabidi wapate kwanza watoto wa viongozi na wengine mtapata zitakazobakia.

Hicho ndo kipindi mtapigwa hadi fimbo makazini, nadhani Dalili za Makofi zimeanza na hakuna wa kuwatetea.... Ukienda kushtaki makahamani unawakuta wale wale. Unapeleka kesi na unafungwa wewe. Wa kupiga kelele itakua ni familia yako tu wengine wote wanaogopa.

Akina Mbowe kipindi hicho watakua wanakula kuku kwa mirija tu.

Mtawaita na hawataitika tena. Ipo sababu kubwa sana ya Kuilinda Demokrasia na vyama Vya Upinzani. Walioianzisha na Kuitetea kwa Damu hawakua wajinga they focused on their future.

Hatubembelezani hapa kuilinda demokrasia ya kweli maana kesho ni yetu sote.

Kila Unachotaka kukishabikia kipime kwanza madhara yake ya baadae.

Watu mnatamani vyama vya Upinzani vyote vife au vifutwe ila ipo siku mtavililia na hamtavipata.

Tafakari

Siku njema
 
Ibumalo

Senior Member
Mar 19, 2017
153
250

Maneno yaliyojaa tafakuri.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sigara Kali

JF-Expert Member
May 28, 2017
3,047
2,000
Hii hali itokee tu hata kesho manake watz vichwa vibovu mtanzania akila ugali,akashiba na kwenda kunya chooni basi ndo keshamaliza hapo anaona maisha ameyapatia,Watz wa sasa ni wabinafsi ila ipo siku makaburi yetu yatakuja kuchapwa fimbo na kutemewa mate na vitukuu vyetu,Leo tunawaheshimu kina mkwawa,kinjekitile ngwale,isike na mirambo,Nduna Songea kwa sababu walijitoa kwa ajili ya sisi wajukuu zao tuje kuishi vizuri nje ya mikono ya mkoloni mweupe kutoka bara Ulaya,lakini leo hii watz wenyewe tunabaguana pale tunapopinga mtanzania mwenzetu ambaye kaja kama mkoloni mweusi kutunyanyasa,tuna safari ndefu sana nchi hii

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom