Godbless Lema akiuka maagizo ya Rais wake

Godbless Lema akiuka maagizo ya Rais wake

Mazaya

JF-Expert Member
Joined
Apr 9, 2015
Posts
875
Reaction score
771
Habari wana Janvi.

Kwa wana UKAWA wote na Watanzania kwa ujumla wanao fuatilia siasa za nchi yetu bila kujali itikadi za kisiasa mtakuwa mnakumbuka jambo hili.

Hivi karibuni wakati UKAWA wanamtambulisha mgombea wao Mikoani, mgombea wa UKAWA Mh Edward Ngoyi Lowasa alitoa tamko au agizo ambalo wana UKAWA wanaliita "Tamko Zito" alimuagiza anaejiita/kuitwa Rais wa Arusha Mh Godbless Lema aende kwa Mkurugenzi wa TANESCO Arusha akafuatilie suala la tatizo la kukatika kwa umeme kwa lugha nyingine amwambie Mkurugenzi akome kukata umeme Arusha na kama Mkurugenzi hatamsikiliza Lema, basi Lema amtwangie Mh Lowasa.

Kinachonishangaza tangu tamko hili litolewe umeme bado unakatika na maeneo mengine umezidi tofauti na ilivyokuwa mwanzo, Je? Mh Lema alikaidi maagizo ya Mh Lowasa? au Mkurugenzi amekaidimaagizo ya Mh Lema?

Au Mh Lowasa aliongea haya ili apate huruma ya wananchi? Yaani ilikuwa ni kauli aliyoitoa bila kujua kama hana uwezo wa kumfanya chochote Mkurugenzi wa TANESCO?

N.B naomba ufafanuzi wa maswali yangu hayo wanajamvi.
 
Nakumbuka tu ule uchaguzi wa 2010...kuna hadithi ndefu sana...imekula kwa lema
 
mkuu inavyosemekana mh. lowasa ana parknosis huu ugonjwa unafanya mtu kusahau mara kwa mara ye alijua anaitoa hiyo kauli km alivyokuwa waziri mkuu kipindi kile kashasahau kumbe si waziri mkuu tena.. dooh
 
Habari wana Janvi.

Kwa wana Ukawa wote na Watanzania kwa ujumla wanao fuatilia siasa za nchi yetu bila kujali itikadi za kisiasa mtakuwa mnakumbuka jambo hili.

Hivi karibuni wakati Ukawa wanamtambulisha mgombea wao Mikoani, mgombea wa Ukawa Mh Edward Ngoyi Lowasa alitoa tamko au agizo ambalo wana Ukawa wanaliita "Tamko Zito" alimuagiza anaejiita/kuitwa Rais wa Arusha Mh Godbless Lema aende kwa Mkurugenzi wa TANESCO Arusha akafuatilie suala la tatizo la kukatika kwa umeme kwa lugha nyingine amwambie Mkurugenzi akome kukata umeme Arusha, na kama Mkurugenzi hatamsikiliza Lema,basi Lema amtwangie Mh Lowasa.

Kinachonishangaza tangu tamko hili litolewe umeme bado unakatika na maeneo mengine umezidi tofauti na ilivyokuwa mwanzo, Je? Mh Lema alikaidi maagizo ya Mh Lowasa? au Mkurugenzi amekaidimaagizo ya Mh Lema?

au Mh Lowasa aliongea haya ili apate huruma ya wananchi? yaani ilikuwa ni kauli aliyoitoa bila kujua kama hana uwezo wa kumfanya chochote Mkurugenzi wa TANESCO?

N.B naomba ufafanuzi wa maswali yangu hayo wanajamvi.

Upuuzi mtupu na kwa taarifa yako alitoa maagizo kwa Wenje wakati akiwa Mwanza.
 
Mwambie aliekutuma ukawa hatudanganyikii, aliambiwa wenje na tayari Mwanza umeme si tatizo tena
 
Yaani mleta mada kiazi kweli, maisha bora mliyo ahidiwa na Ccm yako wapi??
 
Yote kwa yote umeme imekuwa kero mno na si tu Arusha ni TZ yote na hakuna tamko rasmi ni nini kinaendelea...Kweli WATZ tuna nidhamu ya woga mno...
 
Acha ufalaaaa wewe....aliyeambiwa ni Wenje wa Mwanza....Ndorooooobo wewe...

Usimtukane mwenzio , alieambiwa ni lema pale Arusha. Pengine yalirudiwa MWANZA, fanya utafiti kabla ya kukurupuka na kutumia lugha chafu. Chama chako hakihitaji wahuni wasiotumia kipao Chao na uwezo wao wakutumia akili walizopewa na Mungu.
 
Acha kuwa na akili finyu. Lowassa ni Rais wa Lema kivipi? Kila jambo si la kuliletea propaganda na siasa. Bure kabisa
 
Back
Top Bottom