God is real

God is real

Issue nyingi Sana zimeshindwa kuthibitishwa kuhusu uumbaji wake kisayansi, kwa maana hiy, uumbaji wa dunia na ulimwenguni Kwa ujumla haujaweza kuelezewa Kwa mapana yake na sayansi Tu, kuna nguvu isiyoonekana imefanya yote haya tena Kwa usahihi mkubwa Sana pasipo kukosea chochote. Kila kitu kimepangwa kikapangika Kwa mahesabu makali, hiyo nguvu naiita Mungu mwenyezi mwenye enzi na mamlaka yote katika vyote vinavyoonekana na visivyoonekana Kwa macho ya nyama.a Aimidiwe milele, Amina.
Sent using Jamii Forums mobile app
Kuna watu wanashindwa kuufaham ukweli huu mdogo
 
Nina imani hata Kiranga anapinga uwepo kamili wa huyu Mungu wa kuambiwa, ila akilini mwake anakataa katakata kwamba ulimwengu na vyote viujazao vilijileta vyenyewe tu
Hata huyo Kiranga anaamini Mungu Yupo tatizo hajui Ni Mungu yupi
 
Hivi tunatumiaje nguvu nyingi/Muda kiasi hiki kuthibitisha uwepo wa Mungu??

Hii si kazi yetu, Mungu anajidhihirisha.

Maandiko husema mpumbavu husema hakuna Mungu, kwanini tuangaike na wapumbavu??

Si kazi yetu kumthibitisha Mungu!!
 
Kuna Mungu, yaaaani Mungu is there na haletwi na kanisa wala msikiti
Just chukulia tu yale ma process ya glycolysis na Krebs cycle, hiv Kuna kemikali ambazo zinaweza kujidirect zenyewe vile bila kuwepo na mtu alie unda mfumo mzima wa mambo kama hayo,

kikubwa kabisa cha kudhihirisha Mungu ni kifo, waulize hao wapinga Mungu, roho inatoka mwili kwa sababu mwili umekufa au mwili unakufa kwa sababu roho inatoka, kwa nini wasi initiate tena process za mwili mtu arudi kuwa hai...

Hata kama Bible na vitabu vingine vikifeli bado Mungu anabaki kuwepo, haizuii Mungu kuwepo
Mm najua Mungu yupo, hizo nyingine kama dini ni fantasy tu cha muhimu ni kutambua kuwa kuna Mungu mmoja, tuishi kwa kadiri ya matakwa yake maana yupo kabisa
 
Mi naamini yupo ila Jina Lake tumefichwa maan kila nikiitafakari ile Amri ya "Usilitaje Bure Jina La Bwana Mungu Wako"
Nagundua ni Jina lenye nguvu kubwa na unapolitaja lazima Aje kwa ishara ambazo si za mchezomchezo.
Hivyo basi jina Mungu nadhani ni la Cheo tuu kama ilivyo Raisi... yani ni sawa tuseme usilitaje bure jina la raisi wako. huku yeye mwenyewe akiitwa John.

Yote Yatokeayo Ni Kwa Mapenzi Yake So Kutoa Ushuhuda Ni Kwa Kila Sekunde Ya Mtu Anashuhudia Uwepo Wake.
 
Nikisoma 2Wafalme 6:5~7 huwa naona tofauti ya science na imani hasa mstari wa 6,,,kuhusu shape ya kitu cha kuelea..kwa hata ukitaka kutafuta volume ya water displaced hutoipata,,,mass ya water displaced hutoipata au density ya kile chuma hutoipata labda density ya hayo maji tu maana iko constant.

Ila ni science ipi iliokifanya hiki chuma kielee??

Je! Kwa hili tusikubali kwamba Imani ya kumwamini Mungu ni inversely proportional na Science ambayo ni falsafa ilioanzishwa na watu ambao ni viumbe wa Mwenyezi??

Kama science imeweza kuextract asilimia 10%ya uumbaji wa Mungu,,tena hii iko kwenye percentage ya kibinadamu,,Mungu mwenyewe akitupa percentage ya kile tulichogundua kwenye hio science si itakuwa asilimia 0,,0%??

Japo kwa kuwa binadamu Anaendelea kuchunguza yapo mengi atayajua.
 
Mimi nipo na MUNGU ALIYE HAI kila siku inayoitwa leo.
 
Issue nyingi Sana zimeshindwa kuthibitishwa kuhusu uumbaji wake kisayansi, kwa maana hiy, uumbaji wa dunia na ulimwenguni Kwa ujumla haujaweza kuelezewa Kwa mapana yake na sayansi Tu, kuna nguvu isiyoonekana imefanya yote haya tena Kwa usahihi mkubwa Sana pasipo kukosea chochote. Kila kitu kimepangwa kikapangika Kwa mahesabu makali, hiyo nguvu naiita Mungu mwenyezi mwenye enzi na mamlaka yote katika vyote vinavyoonekana na visivyoonekana Kwa macho ya nyama.a Aimidiwe milele, Amina.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu usipoteze muda kufikiria mambo ya
Mungu huyu jamaa hayupo kabisa
 
Back
Top Bottom