GNU Baada ya Uchaguzi Mdogo wa Bububu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

GNU Baada ya Uchaguzi Mdogo wa Bububu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by jamesbond007, Sep 17, 2012.

 1. jamesbond007

  jamesbond007 Member

  #1
  Sep 17, 2012
  Joined: Jun 27, 2012
  Messages: 36
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hakuna anayeweza kubisha kwamba sasa Serikali ya Umoja wa Kitaifa imejaribiwa na imefeli majaribu hayo. Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Bububu ulikuwa ni mtihani uliokuwa ndani ya mtihani. Mtihani wa kwanza ni kwamba ulitakiwa upime kiwango cha ukubalifu wa Ajenda ya Zanzibar.
  Mtihani wa pili ulikuwa upime kiwango cha utendaji na ufanyaji kazi wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa ya Zanzibar; na kwa hili la pili suala kubwa lilikuwa ni je kwa kiasi gani serikali hiyo ni moja panapohusika dhana ya Maridhiano na Mustakabali wa Zanzibar.
  Kwangu, na naamini kwa wengine wengi, suala kamwe halikuwa kushinda na kushindwa kwa CUF ama CCM. Njia za kila mmoja wao kufikia kwenye ushindi huo, zilipaswa kuakisi kwenye majibu ya masuali mawili ya juu, ambayo nayaita kuwa ni mtihani ndani ya mtihani.
  Sichukulii, kwa hivyo, matokeo yaliyotangazwa na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar kuwa ndio kipimo cha kushinda na kushindwa kwa vyama vilivyoingia kwenye uchaguzi. Nachukulia suala zima kwenye mizani ya Umoja ndani ya Serikali ya Umoja wa Kitaifa na Mustakabali wa Ajenda ya Zanzibar.
  Je, ndio tuseme kuwa tumefeli na wahafidhina wakisaidiwa pakubwa na mabwana zao wa Tanganyika ndio walioshinda? Hapana. Natamani jawabu isiwe ndiyo. Natamani jawabu “TUNASONGA MBELE, NA KURUDI NYUMA MWIKO.”
   
Loading...