Ndio ni kweli kabisaa! Nadhani hii ni matokeo ya utandawazi na katika mikakati ya wazungu kuanzisha utandawazi ili kushare majanga kama haya baada ya kuona yanatokea kwao Tu!
Kuna member mwenzetu humu ameeleza vizuri kuhusu majanga km haya ya Corona kuwahi kutokea huko nyuma na Athari hazikuoneka kwa kiasi kikubwa huku kwetu yaliishia hukohuko kwao na baadhi ya nchi huku Afrika hatukujua lolote hata mpaka maradhi yanaisha hatukuwa na Updates zozote km tunazosomewa kila siku mitandaoni.
Nadiriki kusema Utandawazi huu unaofanya Dunia kuwa kijiji ndio unasababisha yote haya maana lazima tukubali kuna mataifa makubwa yana uwezo wa kutangaza chochote ili mradi wanajua maslahi yake...Naamini kabisa utandawazi usingekuwepo Corona isingetufikisha hapa Tulipo leo Afrika!!
Waafrika Tuzinduke safari bado ni Ndefu japo basi hata wajukuu zetu wapate pa kuanzia sie tushachelewa.
Hata JF unayotumia ni sehemu ya utandawazi.
Kuna mambo kadhaa hapa yanayochochea maambukizi kuonekana sana.
1. Ongezeko la watu.
2. Watu kuingilia makazi ya wanyama kulima na kufanya shughuli nyingine.
3. Watu kula vitu ambavyo hawakuwahi kula awali.Hususan nyama.
4. Watu kusafiri sana, kwa haraka, sehemu nyingi za dunia.
5.Watu kutozingatia masharti ya usafi na afya bora.
Utandawazi ni kama moto. Unaweza kuutumia moto kupika chakula, unaweza kuutumia moto kuunguza nyumba.
Ingawa utandawazi unachangia kuongeza maambukizi, utandawazi huo huo unachangia kuelimisha watu kunawa mikono, watu wamefanya tafiti kwa urahisi kupitia utandawazi etc.
Tusilaumu utandawazi, tulaumu utandawazi unavyotumika.
By the way, pandemics za 1918 na hata kabla zilitokea bila utandawazi.
Sent using
Jamii Forums mobile app