Global publishers - utapeli ??

Global publishers - utapeli ??

Mpucha

JF-Expert Member
Joined
Jun 11, 2012
Posts
1,268
Reaction score
1,647
Ndugu wapendwa,inawezekana hapa sio jukwaa sahihi lakini napost huku kwa kuwa wasomaji ni wengi.
Juzi nilituma sh 500 via 0757400600 kwa m-pesa ili nisome gazeti la globalpublishers online, nikatumiwa PIN number.
Cha ajabu naingiza PIn[accurately] inakataa, inasema invalid PIN, nawapigia via the same number, simu inaita tu haipokelewe, nikawatumia email via info@globalpublishers.info, no response, nikapiga simu namba 255659176842 ambayo ipo kwenye tangazo lao, no response, Je huu ni utapeli ? naomba msaada kwa mwenye taarifa,thanks.
 
Gazeti gani ulitaka kusoma? Kwanini? Umeanza lini? Nani alikufundisha? Ili iweje? Samahani,mwenzio mimi mwanasheria....nimezoea maswali. Mkuu,ipotezee tu hiyo jero lakini siku nyingine kuwa makini
 
Gazeti gani ulitaka kusoma? Kwanini? Umeanza lini? Nani alikufundisha? Ili iweje? Samahani,mwenzio mimi mwanasheria....nimezoea maswali. Mkuu,ipotezee tu hiyo jero lakini siku nyingine kuwa makini

Gazeti ni risasi.
Nimeiweka hapa makusudi, ili kama kuna mamlaka husika ifuatilie hilo kwani yawezekana ni watanzania wengi "wameshatapeliwa" hili ni jukwaa la kuelimishana/experience sharing
 
Hembu Mkuu post vitu vya maana, magazeti ya udaku peleka malalamiko yako kwa mamlaka ya udaku na wala si hapa JF.
 
lakini nafikir mtoa mada ana point ya muhimu sana. kwamba inawezekana watu wengi wanatapeliwa kwa staili hiyo. binafsi kama ni kweli inabidi kwanza kabisa uwashataki manake wanaiba hata kama ni mia 5
 
Hembu Mkuu post vitu vya maana, magazeti ya udaku peleka malalamiko yako kwa mamlaka ya udaku na wala si hapa JF.

Vitu vya maana ni vipi ? naomba ufafanuzi. Hili suala haliathiri maisha ya watanzania ?
 
Kama wewe ni JF Member na bado unasoma MAGAZETI YA UDAKU basi ujue
"YOUR RUBISH IN A RUBISH PIT"
Hiyo hela katoe SADAKA
 
Kama wewe ni JF Member na bado unasoma MAGAZETI YA UDAKU basi ujue
"YOUR RUBISH IN A RUBISH PIT"
Hiyo hela katoe SADAKA
I see, next time jitahidi kuwa na staha katika kauli zako mkuu. Kuna watu wanasoma magazeti ya udaku na ni wastaarabu sana na wasomi kuliko wewe unayewadharau wenzako kwa kiingereza chako kibovu.

Kama kwako magazeti ya udaku ni rubish na wasomaji wake ni rubish, basi kuna wengine ambao wanasoma hayo kwa ajili tu ya kupotezea mawazo, sawa sawa na vile wewe ambavyo huwa unaamua kujipumzisha kwa kukaa baa au kusoma comic books au kusikiliza nyimbo za kanisani au bongo flava. Hakuna tofauti. Ni vizuri kujifunza kuheshimu hisia za watu wengine.
 
Na yale magazeti yanavyopendwa na watu wengi wakifanya hivyo kwa watu 100 kwa siku, mmmmmh plus Dar live,
Hiyo ndo STREET UNIVERSITY.
 
ukweli global publishers ni matapeli. Mm pia nashuhudia nilishatapeliwa sh.500 kwa mtindo huohuo. Nilifata maelekezo ya kutuma vocha kwenye no. iliyotolewa pale. Sikujibiwa mpaka leo miezi 2. Wezi hao, siwaamini tena na address yao nilishafuta kwenye browser yangu. Pfuu...
 
Kama wewe ni JF Member na bado unasoma MAGAZETI YA UDAKU basi ujue
"YOUR RUBISH IN A RUBISH PIT"
Hiyo hela katoe SADAKA

Mkuu magazeti ya Udaku hata akina Bill gate na OBAMA, David Cameron etc wanasoma. Ukiwa too fomal huwezi kujua yanayopita nyuma yako...UDAKU una umuhimu sana katika maisha. Jirekebishe anza kusoma hayo siku moja utajua kwa nini!!
 
Hii biashara ya kulipia na usome hayo magazeti, GP imewashinda, News Int'l ya magazeti ya "The Sun" iliwashinda ndio itakua GP?
Kwanza watu wenye uwezo wa kusoma hayo magazeti ya GP kila mara ni wachache na mtu akiingia kwenye mtandao, sidhani atakua yuko tayari tena alipie kusoma gazeti la udaki, hata ingekua sh. 100..!
Ila ni wazo zuri, baadae nafikiri, wanaweza rudisha hii taratibu ya kulipia, hasa watumiaji wa mtandao wakiongezeka...
 
Usimwambie maana asiyejua maana! Wengi wanaangamia kwa kukosa maarifa kisa kikiwa ni kutanguliza ujuaji, dharau na kashfa kwa itikadi za wengine! Usikashif magazet ya udaku kwani statistics zinaonesha ndiyo yanayopendwa zaidi Tanzania! Hata ndugu zako wanasoma, kama siyo mkeo basi mwanao!
 
Gazeti ni risasi.
Nimeiweka hapa makusudi, ili kama kuna mamlaka husika ifuatilie hilo kwani yawezekana ni watanzania wengi "wameshatapeliwa"
Risasi? imekupata ya kichwa au? na bado unapumua!
 
Back
Top Bottom