Global fighting against cyber attack 2017

MLINGANO

Member
Joined
Nov 26, 2013
Messages
15
Points
20

MLINGANO

Member
Joined Nov 26, 2013
15 20
Udukuzi wa mifumo ya kompyuta na simu uliyotokea Jana.
Jana usiku kumetokea udukuzi wa kimtandao takribani nchi zaidi ya 150 duniani kwa siku ya juzi tu. Nchi kubwa zenye wataalamu wa kutosha kama [HASHTAG]#GermanAsiachinarusiauingereza[/HASHTAG] zimeathirika sana na Afrika. Ujangingili huu wa kimtandao unaendeshwa na watu wenye utaalamu wa kutosha jamani. Lengo la udukuzi wa Juzi ulikuwa ni kujipatia fedha kwa aina yoyote ile na utaendelea wiki nzima . Walivamia baadhi ya computer na kuzifunga files zote kwa kufanya [HASHTAG]#encryption[/HASHTAG] method. Unapotaka kufungua computer yako unakutana na message isemayo [HASHTAG]#Please[/HASHTAG] pay $300 (£230) payments to restore access”. Ili Computer yako irudi kwako salama ni lazima ulipe dola 300 za kimarekani na inaongezeka kadri unapochelewa kulipa huo mpunga wao” Mfano wamekupa siku moja ulipe hiyo hela lakini wewe ukapitisha siku mbili basi kiwango kinafikia dola 400. Uvamizi huu wa kimtandao unaitwa Ransomware” sababu lengo lake ni kujipatia fedha tu na kirusi kinachofanya mashambulizi kinaitwa WannaCry”. Kimeshasambaa duniani kote hiki kirusi jamani even Tandale . WannaCry anaingia kwenye computer yako na kuicontrol kwa kila kitu na kukuwekea password. WannaCry akishaingia uwezi kumtoa jaman mpaka ulipe mpunga wao ndio unapewa uhuru wa kutumia computer yako. Mwaka Huu Mamlaka ya Usalama wa Taifa ya Marekani (National Security Agency – NSA) . ni taasisi yenye nguvu kubwa kuliko zote duniani katika masuala ya Technolojia na wana wataalamu wakubwa duniani lakini walivamiwa kimtandao na HACKERS na kuibiwa taarifa zao pamoja na software yao iliyokuwa inatumika kuiba taarifa za watumiaji wa mtandao kama mimi au wewe. Hii Software ya NSA ambayo ndio iliyoibiwa na HACKERS inaitwa Eternal _blue. Yani NSA waliitengeneza kwa ajiri ya kutuchunguza sisi tunafanya nini mtandaoni. Hii Ndio Tabia ya NSA Wana taarifa ya kila mtu duniani aliye kwenye mtandao. Baada ya HACKERS kuiona hii software ina uwezo wa kuingia kwenye computer za watu bila wao kujua, ndipo wakatengeneza virus aitwaye WANNACRY ambaye ndiye anaitesa dunia kwa sasa. Kwahiyo bila Software kuibiwa NSA huu uhuni usingetokea !
"A statement from Microsoft president and chief legal officer BradSmith on Sunday criticised the way governments store up information about security flaws in computer systems. "We have seen vulnerabilities stored by the CIA show up on WikiLeaks, and now this vulnerability stolen from the NSA has affected customers around the world," he wrote. The organisation also said that many organisations had failed to keep their systems up to date, allowing the virus to spread. Microsoft said it had released a Windows security update in March to tackle the problem involved in the latest attack, but many users were yet to run it."
NJIA YA KUJIKINGA NA HUU UVAMIZI WA KIMATAIFA NA VIRUS [HASHTAG]#WANNACRY[/HASHTAG] KWA SASA 2017
1.Hakikisha computer yako ina antvirus ambayo ipo active ndugu zangu. Sio unatumia internet na hauna ant-virus au imexpire.
2.Usifungue Email ambayo huitambui kabisa au kwa lugha nyingine spam Email ambazo huzielewi.Humjui mtu aliyekutumia wala ujumbe .
3.Hakikisha Operating system umefanya Window Updates! Please Updates Window Yako kwa ajiri ya kupokea Window security policy mpya na za kisasa iliyotolewa na Microsoft Wiki hii.
4.Kwa wale wanaotumia sana browser kwa sana “ kuna kitu kinaitwa pop-ups—Small Window or display that suddenly appears ("pops up") in the foreground of the visual interface. Pop-ups can be initiated by a single or double mouse click” Hapa jaman usiruhusu Pops ups zikitokea [HASHTAG]#Block[/HASHTAG] them kwenye browser yako. Kiruhusi kinaingia pia kwa njia hii.
5.Ukiona computer yako inadalili kuhakiwa na mtu please [HASHTAG]#itoe[/HASHTAG] haraka kwenye mtandao au chomoa modem.
6.Hakikisha data zako kwenye computer ama simu umezifanyia backup kwenye external files ama flash
7.Punguza kufungua websites ambazo hazina Tija kwako kama Websites za ngono ,gaming na bets.
8. Tumieni Vifaa vya kisasa vinavyotumika kwa ajiri ya kulinda network yako kama FIREWALL n.k
Ushauri!
Serikali na Taasisi zake zote ikiwemo usalama wa Taifa , Polisi na TCRA pamoja COSTECH watoe Elimu ya kutosha kwenye matumizi bora ya mtandao ili watu wachuke taadhari mapema. Tukio Hili limetokea Tokea ijumaa ya 12/5/ 2017 na kuendelea mpka wiki hii kwahiyo kuna umuhimu sana wataalamu wengi wa ICT Kuendelea kutoa elimu ya kutosha kwenye private sectors. All the Best.
IT Techinian!
Kurwa B Kandoro
0653203508.
hkandoro@tangafresh.com
 

Attachments:

Thread starter Similar threads Forum Replies Date
akida peter Tech, Gadgets & Science Forum 0
simplemind Tech, Gadgets & Science Forum 0

Forum statistics

Threads 1,382,637
Members 526,405
Posts 33,832,426
Top