Giza ni nini?

KENZY

JF-Expert Member
Dec 27, 2015
30,261
69,467
Habari zenu wana JF,

Ningependa kwa wanaojua maana ya giza ni nini wanijuze nilisha tafakari nikakosa majibu na hata nilishawauliza baadhi ya watu waliishia kuguna tu.

Inavyoonekana kuna vitu tunaviona kila siku mfano giza lkn mtu ukimuuliza hicho ni nini anashindwa kukujibu au hakujibu kiufasaha.

Na lingine la ziada ni je giza huzalishwa kama mwanga unavyozalishwa na jua? Na kama giza linazalishwa, je linazalishwa na nini au linafanyikaje?

Ni hayo tu wadau naomba kuwasilisha..
 
Giza ni matokeo ya dunia kujizungusha kwenye mhimili wake kutoka magharibi kwenda mashariki na wakati inazunguka ndio inasababisha day and night yaani inapokuwa upande wa jua inakuwa mchana isipokuwa upande wa jua inakuwa usiku hence inasababisha giza

so kwa ufupi giza ni matokeo ya uso wa dunia kutopata mwanga wa jua
 
Kwanza tuanze hapa dunia ni duara na jua lipo katika System ya sayari zetu tisa hivo lenyewe lina shine all the time sasa kama jua linawaka muda wote kwanini pana usiku na mchana? Dunia ni Duara jua haliwezi mulika duara lote kwa wakati mmoja hivo kutokana na dunia kujizungusha katka muhimili wake Yani dunia inapozunguka kuna upande unapata mwanga mwingine unakuwa na giza ndo mana leo hii unaona hapa inaweza kuwa mchana mahala pengine usiku, lakin tunayo satellite nyingine ambayo ina rotate respectively na dunia hii ni mwezi(Moon) wenyewe una akisi mwanga wa jua na kutoa illumination katika dunia , Upo hata mchana ni ivo huuoni kwa ajili ya miale mikale ya jua
 
Giza ni matokeo ya dunia kujizungusha kwenye mhimili wake kutoka magharibi kwenda mashariki na wakati inazunguka ndio inasababisha day and night yaani inapokuwa upande wa jua inakuwa mchana isipokuwa upande wa jua inakuwa usiku hence inasababisha giza

so kwa ufupi giza ni matokeo ya uso wa dunia kutopata mwanga wa jua

Unachanganya usiku, mchana, Giza na Mwanga. Usiku kunaweza kuwa na Mwanga vile vile mchana kunaweza kuwa na giza.
 
sijachanganya mkuu ila nimemjibu kama mtoa mada alivyouliza swali kama ulimwelewa mtoa mada kuna hii sentesi aliandika "
Inavyoonekana kuna vitu tunaviona kila siku mfano giza lkn mtu ukimuuliza hicho ni nini anashindwa kukujibu au hakujibu kiufasaha." maana yake anataka kujua kwanini Giza linatokea hence usiku
 
giza linaweza kuwa:
-kutokuwepo kwa mwanga
-kutokuelewa, kutokuamini
-mji ktk nchi ya misri penye mapiramidi maarufu
 
sijachanganya mkuu ila nimemjibu kama mtoa mada alivyouliza swali kama ulimwelewa mtoa mada kuna hii sentesi aliandika "
Inavyoonekana kuna vitu tunaviona kila siku mfano giza lkn mtu ukimuuliza hicho ni nini anashindwa kukujibu au hakujibu kiufasaha." maana yake anataka kujua kwanini Giza linatokea hence usiku
[/

Giza linatokea pale Mwanga unapokosekana iwe mchana au usiku. Sio kwamba eti usiku ndio Giza na wala sio kwamba mchana ndio Mwanga. Usikariri
 
Habari zenu wana JF,

Ningependa kwa wanaojua maana ya giza ni nini wanijuze nilisha tafakari nikakosa majibu na hata nilishawauliza baadhi ya watu waliishia kuguna tu.

Inavyoonekana kuna vitu tunaviona kila siku mfano giza lkn mtu ukimuuliza hicho ni nini anashindwa kukujibu au hakujibu kiufasaha.

Na lingine la ziada ni je giza huzalishwa kama mwanga unavyozalishwa na jua? Na kama giza linazalishwa, je linazalishwa na nini au linafanyikaje?

Ni hayo tu wadau naomba kuwasilisha..

Giza ni aina fulani ya mirungi inayolimwa kwa wingi huko Meru Kenya, mimi huitumia kila jumamosi kuanzia jioni, huwa inanipa mzuka ku party from dusk till dawn.
 
Back
Top Bottom