Ghorofa wanaloishi Watanzania Afrika Kusini, hufanya uhalifu na kujificha humo

Isanga family

JF-Expert Member
Feb 25, 2015
14,590
25,690
Hilo jengo ndio wanaloishi vijana wengi wa kitanzania Johannesburg lipo mtaa Nugget/jeepe hilo jengo wao hulitambua kwa Chaka lao halina umeme, maji wala choo vijana wengi wa Kitanzania wanaoishi humo hufanya biashara ya unga, bangi na shughuli nyingi haramu hupatikana hapo pia kuna bar na wadada poa pia ndani ya huo mjengo.

Matukio ya kuuana humo ni kawaida tu, juzi tuu hapo katolewa Mtanzania humo kakatwa kichwa. Pia ni chimbo la bunduki zao wanazozitumia kukaba ndani ya mitaa ya jozi. Panya road pia walifikia hapo miezi michache iliyopita baada ya kufanya ukabaji mitaa ya Jozi na walikuwa wanakaba mpaka Watanzania wenzao kuzunguka hilo jengo ila baada ya kudhibitiwa aliyepona ni kama watatu tuu hao ndio mmoja yupo hosptali, mwingine anaugulia maumivu ya kutolewa jicho na kuvunjwa miguu yupo Soweto na wengine wamekimbilia Pretoria na Durban kuwa mabaharia wa Nchi kavu.

Ila waliopo Pretoria dawa yao inachemshwa kama wale waliovamia Jozi, kwa sasa kila kona ya mwisho wa mtaa kuna walinzi wa jiji na redio call zao imewafanya vijana wengi raia na wageni waliokuwa wanakaba kushindwa kwa mida ya kawaida labda usiku ila ujambazi wa magari kwa mitaa kama Troy, kerk, bree, president na pritchard ni kama kawaida hiyo ndio Johannesburg Town..

tmp-cam-1589607162.jpg


tmp-cam--1476898712.jpg
 
Aiseeh assnte kwa taarifa, kuna siku nilikuwa nimevaa mavazi yaliyoashiria kuwa mie ni mtanzania. Nikakutana na jamaa mmoja wakati natoka lunch akajitambulisha yeye ni mtized. Sijui kwanini roho ilisita kumuelezea uhalisia wangu nikamwambia nimeingia Joberg leo asubuhi (siku hiyo) na naondoka kesho yake. Akanishawishi niende kumtembelea anakoishi na akataja huo mtaa.... Nimewaza hapa jinsi ambavyo labda saa hii ningekuwa marehemu au washani massacre iwapo ningejipelekaa..... yeemweeeh.

Asante sana mtoa mada nimeongeza kuziba masikio hasa nikutanapo na nisiyemjua wala kumfahamu.

Ni hatari na inasikitisha.
 
Hiyo nugget street ni umbali wa Kama mita 100 ila hizi mita Mia moja ni bora ucross Amazon unaweza kusalimika ila mtaa huo ni noma unapigwa roba SAA 7 mchana kweupe na hakuna atakayekusaidia
Sio kwamba gvt ya SA haijui wanajua na wanaona na hapo panajulikana ila hakuna hatua zinazochukuliwa
Hayo majengo ni Kama yametelekezwa vile ndio maana yamekatiwa maji na hayana umeme
 
weed waharifu wakubwa South ni wazimbabwe ndio wanaoongoza kwa kuteka maroli na kubomoa godown na wanunuzi wakubwa ni Waethipia mtaa huo huo mbele kuna maduka yapo vizuri Joburg mall na mengineyo yaliyopo bree Waethiopia wanauza nguo bei chini ya Mchina anaejumlisha China mall..
 
Back
Top Bottom