Ghorofa lililojengwa Dodoma kwa pesa za walipa kodi kupitia wakala wa majengo Tanzania TBA

saimon111

JF-Expert Member
Apr 5, 2012
1,736
1,355
Habari za mida wakuu...? Kabla yakuandika mengi sana naomba niende moja kwa moja kwenye point. Leo nazungumzia ghorofa la serikali lililojengwa kwa pesa za walipa kodi kupitia wakala wa majengo Tanzania (TBA).

Hili ghorofa ni miongoni mwa majengo yaliyokua na mvuto sana kwa mji wa Dodoma lilipojengwa, cha ajabu na kweli kinatokea ni kwamba aliyekua waziri wa ujenzi ambaye sasa ndio mfalme alipiga marufuku ghorofa hili kutumika mpaka liwekwe lift.

MY TAKE:
hili jengo wakati linajengwa lilikua lishafanyiwa upembuzi yakinifu na wasanifu majengo na michoro ikapita likajengwa bila lift, na palikua panafanyika site meeting kila baada ya muda, na mtendaji mkuu wa wakala alikwisha likagua mara nyingi, muhandisi wa mkoani kakagua. Sasa nashangaa jengo hili limekamilika huu sasa miaka zaidi ya minne na halijapangishwa kutokana na kukosa lift tu.

JE HAYA SIO MATUMIZI MABAYA YA MALI ZA SERIKALI MAANA WAKALA WA MAJENGO WANAYO HALI MBAYA KIUCHUMI NA HILI JENGO NDIO LILIKUA LIWE KITEGA UCHUMI CHAO...??????
63aca256b63d681bd1096161fc14246d.jpg
492be035784f2425df645631e8b4d596.jpg
 
Waliwekee tu elevator ili ndugu zetu wenye Ulemavu na wazee waweze kufika Floor ya 5 kwa urahisi..
Wakala hana hela ya elevator lakini walimuomba waziri walipangishe then wakipata pesa hiyo waliwekee elevator akakataa mpaka waweke elevator kabisa ndio lipangishwe.
 
Naomba kwa anaejua anifahamishe, hivi Magufuli alishawahi soma Diplomasia kwenye kile chuo cha Kurasini ?? Mbona maamuzi yake yanakua yakiniacha njia panda.
 
kwa nini halina lift? hao wataalamu ni MAJIPU......Ghorofa zaidi ya nne hakuna Lift???????
Mkuu mbona mjini ramani nyingi tu za maghorofa hazina elevator lakini yanatumika. Hili ghorofa lilikaguliwa michoro wakakubaliana lijengwe bila lift na waziri JPM wakati huo alikubali na mpaka akawa anakuja kukagua akija dodoma. But katika hali yakushangaza akabadilika ghafla na kusema lisitumike mpaka liwekwe lift.
 
Back
Top Bottom