Ghorofa la Mbunge labomolewa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ghorofa la Mbunge labomolewa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Nov 11, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Nov 11, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  [h=2][/h]THURSDAY, 10 NOVEMBER 2011 13:53 UHURUNEWSROOM
  [​IMG][​IMG][​IMG]


  MAMLAKA ya Mji Mkongwe, Zanzibar, imebomoa ghorofa la kigogo katika eneo la Malindi, baada ya kukiuka maelekezo yaliyotolewa katika kibali cha ujenzi.


  Jengo la ghorofa tatu lililobomolewa linamilikiwa na mwakilishi wa Muyuni, ambaye pia ni mbunge wa kuteuliwa na Baraza la Wawakilishi, Jaku Hashim Ayuob.

  Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mji Mkongwe, Issa Sarboko Makarani, akizungumzia ubomoaji huo, alisema wamelazimika kuchukua hatua kwa kuwa kibali kinaruhusu ujenzi wa ghorofa moja, hivyo inashangaza kuona kumejengwa ghorofa tatu na ujenzi unaendelea.


  Issa alisema awali, baada ya kuona ujenzi wa nyumba hiyo unakiuka kibali cha ujenzi, mamlaka ilitoa agizo la kusitisha ujenzi lakini lilipingwa na mafundi waliendelea na ujenzi.


  Mkurugenzi huyo alisema kinachoendelea sasa ni ubomoaji wa ghorofa ambazo hazikuwemo katika kibali na ramani ya ujenzi wa nyumba hiyo.


  Alisema mamlaka imekuwa ikieleza na kuweka wazi kuhusu ujenzi katika eneo la Mji Mkongwe, lakini kesi kadhaa zimefunguliwa kupinga taratibu hizo.


  Issa aliwataka wananchi watambue Mji Mkongwe wa Zanzibar ni mmoja kati ya urithi wa kimataifa, hivyo hawana budi kudumisha yote yanayoupa hadhi, ikiwemo kuendeleza makazi kama itakavyoelekezwa na mamlaka husika.


  Mkurugenzi huyo pia aliwataka wananchi waache ubishi katika kutekeleza taratibu zinazotolewa na taasisi husika katika kuuenzi Mji Mkongwe.


  Alisema endapo wananchi wataendelea kujenga na kupuuza maagizo ya mamlaka husika, hasara wanazoweza kuzipata ni kubwa, ikiwemo kubomolewa nyumba zao.


  Katika kufikia utunzaji bora wa Mji Mkongwe, alisema mamlaka ipo tayari kutoa elimu na maelekezo kwa wananchi au taasisi yoyote kuhusu namna ya utunzaji wake.


  Hatua ya mamlaka hiyo imechukuliwa siku chache baada ya Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohammed Sheni, kusema tatizo la ardhi ni kubwa na lenye mambo mazito.


  Alisema baada ya muda wananchi watasikia matokeo yake kwa suala la ardhi, kwani ndiyo jambo la pili kwa umuhimu katika ufuatiliaji wake.   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Nov 11, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Nguvu nani anazo?
   
 3. Nani Kasema

  Nani Kasema Senior Member

  #3
  Nov 11, 2011
  Joined: May 31, 2011
  Messages: 148
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Safi sana, atakomaje sasa?
   
 4. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #4
  Nov 12, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Stori hii haieleweki.
   
Loading...