Ghorofa kwa kingereza linaitwaje?

Samahani kwa usumbufu wakubwa naomba kujua kwa lugha ya kingereza ghorofa linaitwaje?

Mimi nadhani tafsiri ya kiingereza itategemea zaidi context ya kile unachotaka kuzungumza kwa sababu neno ghorofa lina maana zaidi ya moja kwa matumizi ya kawaida.

Mfano:
- SMU anakaa mtaa wa Tandamti karibu na lile ghorofa la benki kuu [hapa neno ghorofa lina maana inayokaribiana na 'jengo' ambayo kwa kiingereza ingeweza kuwa na maana ya "building" or "structure"]
- Ofisi ya SMU ipo ghorofa ya saba katika jengo la benki kuu [hapa kwa kiingereza neno ghorofa inabeba maana ya "floor", au "level")
- Benki kuu inajenga jengo jipya la ghorofa mtaa wa Tandamti - [hapa neno ghorofa linaweza kubeba maana ya "multi-storey"]
- Benki kuu inajenga jengo jipya la ghorofa kumi mtaa wa Tandamti - [hapa neno ghorofa linaweza kubeba maana ya "storey" au "floor"]

Jioni njema.
 
Samahani kwa usumbufu wakubwa naomba kujua kwa lugha ya kingereza ghorofa linaitwaje?

Mimi nafahamu ghorofa kwa kiingereza ni Storey na Jengo ni Building na kama ni ghorofa zinaongezeka zitakuwa "two, three four storey building".

Kwahio jengo la ghorofa 12 litakuwa ni "12 storey building" iwe ni makazi au ofisi.

Pia ni sawa kuita multi storey/ story ikimaanisha jengo lenye ghorofa nyingi iwe ni kwa kuegesha magari Multi storey car park au shopping mall.

Majengo mengine zaidi ya haya yanaitwa Skyscrapers au Towers maana yanakuwa yanaelekea angani.
 
si mshikaji kaeka hapo juu kuwa story kwa american english kutoka wikipedia
 
Ghorofa tunaiita Upstairs Sijawahi kusikia jina jingine ( hapa ninapokaa tupo watu wa kutoka mataifa mbalimbali na wengine wanakaa ghorofani na wanatumia neno hilohilo) Nitauliza kama kuna jina jingine
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…