Ghasia: Serikali Awamu ya Nne imeboresha maslahi

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
266
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Hawa Ghasia, amesema Serikali ya Awamu ya Nne imeboresha kwa kiwango kikubwa maslahi ya watumishi wa umma, lakini ndicho kipindi ambacho watumishi hao wameongoza kwa kulalamika.

Alisema tangu Awamu ya Nne iingie madarakani Desemba 2005, maslahi ya watumishi wa umma yameboreshwa kwa kiwango kikubwa kuliko wakati mwingine wowote katika uongozi wa nchi.

Waziri Ghasia alisema hayo juzi mjini hapa wakati alipozungumza kwenye mafunzo ya viongozi mbalimbali wa wilaya hiyo kuhusu Programu ya Mabadiliko katika Utumishi wa Awamu ya Pili.

“Serikali hii ya Awamu ya Nne imefanya mambo mengi kuboresha maslahi ya watumishi wa umma. Kwa mfano, imeongeza mishahara ya wakuu wa Idara, Mfuko wa LAPF ambao ulikuwa ukitoa kiinua mgongo sasa unatoa malipo ya pensheni kwa watumishi wa umma.

“Watumishi waliokuwa wamelundikana katika cheo kimoja kwa miaka mingi, zaidi ya 58,000 walipandishwa vyeo wakiwamo walimu 38,000. Tumejitahidi sana kuboresha maslahi ya watumishi, lakini ndicho kipindi ambacho wameongoza kwa kulalamika,” alisema Ghasia.

Alisema Serikali itaendelea kuboresha maslahi kwa watumishi hao wa umma, lakini akawataka nao waongeze tija na ufanisi katika kuwatumikia wananchi.

Aliwataka watumishi kutumia sheria, kanuni na taratibu za utumishi wa umma katika kutafuta suluhu ya matatizo yanapojitokeza, badala ya kuibuka na kuendesha migomo na maandamano, bila kukamilisha taratibu za majadiliano.

Kuhusu malimbikizo ya malipo kwa watumishi mbalimbali, alisema Utumishi ilishakamilisha taratibu za uhakiki wa malipo hayo na kabla hayajalipwa, yatakuwa yAnafanyiwa kazi na maofisa wa Hazina.
 
Ukiongeza elfu kumi kwenye laki na ishirini then ukokotoe kwa matumizi ya kila siku na huu mfumuko wa bei wa asilimia mia na unusu anao ubavu wa kusema haya kweli? Akawadanganye kwao kwa kuwa bado wamelala fofofo.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom