Gharama za wizi wa mapenzi

Gharama za wizi wa mapenzi

VERITE-NUE

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2019
Posts
1,481
Reaction score
1,450
GHARAMA ZA KUTOKA NA MCHEPUKO
1.Usafiri 10,000
2.Chumba Lodge 30,000
3.Chakula + Vinywaji 30,000
4.Asante Kwa Kuja 50,000

Jumla 120,000 Brother Unaongeza Umasikini Tu Nyumbani Mpe Mke Hii 120,00 Uone Utakavyo Ombewa Na Kupata Zaidi Na Zaidi.

Mchepuko ni mwizi anafurahia Kidogo anachopata; Unauona mchepuko wako haulalamiki sana kama mke wako, akikuomba pesa ya kusuka utakayompa anashukuru, usiponunua chakula ukalipa kodi anashukuru, usiponunua nguo ukampa pesa ya saluni anashukuru. Lakini mke wako yeye mara nyingi pamoja na kujaribu kutimiza majukumu yako lakini bado atalalamika kitu kidogo kama vile “chumvi hamna” mpaka unakasirika na kumuona kama hana shukurani, unaona kwanini hashukuru kama mchepuko.

Lakini kuna upande wa muda, ukichelewa kidogo tu nyumbani mke atalalamika mpaka basi, lakini kwa mchepuko hata usipoenda siku mbili bado ukipiga simu atakuchekea, atakuambia kakumiss na kuonekana kukujali sana. Hapo sasa unaona kua mwanamke si ndiyo huyu, mbona anashukuru, mbona hana kisirani kama mke wangu. Ndugu yangu hakuna kitu hapo, mchepuko unashukuru na unaridhika kwa kila kitu kwakua yeye ni “Mwizi!” anajua nafasi yake na anajua kua hatakiwi kulalamikia kitu cha wizi.

Tuanze katika matumizi, unapompa pesa kidogo na kuhudumia kwa baadhi ya mambo anafurahia kwasababu kuu mbili:
Kwanza si wajibu wako kumpa, hivyo ile ni kama msaada, hisani tu unatoa, si majukumu yako hivyo mtu ukimpa kidogo kama ni msaada lazima afurahi. Anajua anaiba hivyo hawezi kulalamika eti nimeiba kidogo, hii ni tofauti na mke wako, yeye ni haki yake, ni wajibu wako, wewe ndiyo mwanaume, anatakiwa kupata chote hivyo unapokua huhudumii lazima alalamike kwani ni chake anatakiwa kukipata chote.

Sababu ya pili ni kwakua kwa mchepuko hauko peke yako, kwamba hata kama unampa kila kitu mara nyingi anakua na mtu wake wa akiba, kuna mtu anahudumia vitu vingine, kwa hiyo kama ukitoa kodi kuna mwanaume mwingine atatoa hela ya saluni, mwingine atatoa ya ujenzi na vingine vingi. Kwa maana hiyo hana sababu ya kulalamika kwakua majukumu mengine yashatimizwa. Tofauti na mkeo, labda kama unataka nayeye achepuke lakini kama ni muaminifu basi nilazima akulalamikie wewe kwani hana mtu mwingine wa kumuambia matatizo yake kama mchepuko wako.

Katika suala la muda mchepuko haulalamiki kwakua unajua unaiba muda wa watu, kwamba hata kama ukienda kwake kwa wiki mara moja unajua kuna mke hivyo nilazima utulize makalio chini na uache kulalamika, lakini inawezekana ana mwanaume mwingine hivyo unapokua haupo basi huchukua nafasi yako na hana sababu tena ya kulalamika.

Tofauti na mke, unapomuoa anajua yuko peke yake, haibi hivyo unapokua unachelewa nilazima awaze mbona kama naibiwa. Hivyo huo mchepuko siku ukibadilika na kuwa mke nao utataka matumizi zaidi kama mkeo kwakua hakutakua na mtu mwingine wakutoa na utataka muda zaidi kama mkeo kwakua hakutakua na mwanaume mwingine wakuwa naye.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom