Gharama za usafiri ndani ya jijini Dar es Salaam

Mhache

JF-Expert Member
Jun 20, 2008
345
25
Usafiri ndani ya Jiji la Dar es salaam lenye takribani watu milioni nne umekuwa ni mkuki mchungu kwa sisi makabwela. Mtu unayepanda magari mawili kwenda kazini au kwenye shuguli ya kujipatia rizik unalipa kiasi cha shilingi 800 kwenda na kurudi hizo hizo jumla 1,600 kwa siku. Hapo hujanywa hata maji achana na chakula cha mchana. Kwa mwezi nauli tu ni shilingi 32,000 ukitoa jumamosi na jumapili. Ukiweka nauli ya watoto, kodi ya chumba na kikitokea tena kaugonjwa utabakiwa na shilingi ngapi kuendesha familia? Kwa mtu anayelipwa mshahara wa shilingi 100,000 kwa mwezi atahimili maisha kweli?

Kwa mawazo yangu nauli itaendelea kwenda juu kwani gharama ya mafuta inanda kila kukicha.

Naomba mchango wenu, mnatumia mbinu gani kuendesha familia katika hali tata kama hiyo?
 
Back
Top Bottom