Gharama za matibabu Muhimbili zapanda maradufu

Gharama za matibabu Muhimbili zapanda maradufu

Mkuu pale Muhimbili kama huna kitu panaudhi waweza jipotezea maisha hivi hivi unajiona. Wadau hebu fnyenyi kutembelea siku moja pale Muhimbili na muingie huko walikolazwa wagonjwa mjionee wenyewe. Mtu unaumwa na uko taabani unapewa panadol kisa huna hela ya vipimo sasa wanasubiria mpaka utakapopata fedha ya vipimo ndio mambo mengine yafuate. Bungeni tuliowaweka kila siku wanagombana nakutetea maslahi yao na si ya mtz. Hao tuliowapa migodi yetu hivi hatuwezi kuwalazimisha kutoa %%% Fulani kwa ajili ya hizi hospt ili gharama ziweze kuwa chini. tunaambiwa wanaenda nje ili kutuletea wawekezaji sasa hao wawekezaji wanatusaidia nini kama tunakufa kwa kushindwa kulipia matibabu yetu .
Ablessed, bado tuna safari ndefu sana katika kujikwamua toka hapa tulipo, lakini kwa nguvu ya pamoja tutafika tu!
 
Last edited by a moderator:
Acha us...ng wewe hiyo sio sababu ya watu wenye kipato cha chini kufa, au mwanaCCM nini wewe?

Mkuu kwani CCM ndiyo inayoua watu;?? si Mungu amewapenda zaidi??? au si ni siku za ahadi zao zimefika?????
 
GHARAMA ZA MATIBABU MUHIMBILI ZAPANDA MARADUFU.....SASA KUMWONA DAKTARI NI SHILINGI 30,000/=



Muhimbili(1).jpg

Gharama za huduma za kulipia matibabu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili zimepanda maradufu.
Hatua hiyo inayotekelezwa bila kuwashirikisha wadau na watoa huduma ilianza Septemba mosi mwaka huu na kulalamikiwa na wagonjwa na wafanyakazi.

Kwa mujibu wa tangazo la Mkurugenzi wa MNH, lililobandikwa kwenye ubao wa matangazo wa jengo la mateniti la kulipia huduma IPPM, inaonyesha kuwa gharama zilipanda kuanzia Septemba 2, wakati notisi hiyo iliyosainiwa na Mkurugenzi ilitolewa Septemba 4.

Wagonjwa wanaolipia matibabu binafsi Muhimbili waliliambia gazeti hili kuwa wateja wanaotumia ‘ast truck' na huduma ya uzazi inayotolewa na kitengo cha mateniti- IPPM ndizo zilizoongezeka.

Kuanzia sasa upasuaji wazazi unalipiwa Sh. 500,000 badala ya 350,000 za awali. Uzazi wa kawaida ni Sh. 250,000 badala ya Sh. 150,000 zilizokuwa zikitozwa mwanzo.

Walisema kulala kunagharimu Sh. 20,000 badala ya 15,000 wakati tozo la kumuona daktari kwa mara ya kwanza ni Sh. 30,000 badala ya Sh. 20,000 za awali.

Kumuona daktari kwa ajili ya kufuatilia huduma na matibabu zimepanda hadi Sh. 20,000 kutoka Sh. 10,000.


Huduma nyingine kama dawa na uchunguzi wa maabara
zimepanda japo bei zake hazikutangazwa kwenye ubao wa matangazo.

Kwa wagonjwa wa kujifungua kawaida ambao hawalipii gharama watatozwa gharama ambazo hazikafafanuliwa ingawaje serikali inataka watibiwe bure.

"Mfano mjamzito akipata uchungu ghafla na kufika Muhimbili bila rufaa atatakiwa kalipia gharama" alisema mjamzito jina tunalo.

Msemaji wa MNH Aminieli Aligaesha, alikiri kuongezeka gharama hizo ziliongezeka na kuongeza kuwa sababu ya ongezeko hilo ni gharama kubwa za uendeshaji.

Hata hivyo alikataa kutoa maelezo zaidi na kutaka mwandishi wetu kwenda ofisini kwake kwa maelezo zaidi.

Hospitali ya Muhimbili inatoa huduma kwa utaratibu wa aina mbili kuchangia matibabu kunakofanywa na mgonjwa wa rufani pamoja na serikali.

Njia nyingine ni wagonjwa kulipia gharama zote za tiba kama ambavyo wanafanya kwenye hospitali za binafsi.

Hata hivyo gharama za tiba kwa wale wanaochangia matibabu na wale wa rufaa hazijaongezeka.



CC: #TeamBK7
 
Wakati Wanapandisha Gharama za Maisha kwa Kasi ya Kutisha,Wafanakazi waliowengi wamepata Nyongeza wa wastani wa Tshs.40,000/ kwa Mwezi.Shime Watanzania,CCM ni Janga Tushirikiane Kuitokomeza.
 
JF especially jukwaa la siasa ni mahala pazuri sana kwa wanafunzi wa social sciences, aspiring social reformers and politicians of every level. Watu wanaweza toka na mengi sana kupitia jukwaa hili kwenye kulielewa taifa letu na changamoto zake zinazotukabili. Tungekuwa na mfumo wa elimu kama wa ulaya ambapo social sciences demand students to apply their theories on current issues nadhani tungetotoa wanafunzi wengi sana ambao wangetoa thesis zenye kuelezea matatizo yetu na tulipo kwa sasa kwenye ulingo wa siasa, uchumi na matatizo mengine ya kijamii.

Maana everything in relation to social information is available in JF, hata walimu wangeweza kuweka nakala za magazeti zenye angle fulani ya somo na kupata opinion za kisiasa, pumba za wachangiaji wengine (asilimia kubwa ya watu wetu) na angle za waelevu wa mambo to understand the social, wanapokuwa huko kwenye lecture theater discussions in relation to a theory wanayosoma au research mtu anayofanya.

Jana kulikuwa na thread ya Mkutano wa wapinzani ambayo mpaka dakika hii imefikia page 38, na picha zimewekwa za umati mkubwa wa watu walioudhuria na ushabiki wa kupindukia ndani ya thread. On the outlook it appears democracy has grown and people are informed about the political party choices which are available in the country.

That is until you discover the union of that meeting was fueled by what the opposition call a deprivation of democracy in the process of writing a new constitution. But then ask them what is their political demand in the new constitution CDM will most certainly point at the problems of Tanzanian union in their perspective. As for the other political parties we dont even know of their demands in the new constitution apart from disagreeing on the new government bill how the constitution should be written.

As for the people they do pose another conundrum of their purpose for being there nor what they demand in the new constitution considering most of human rights acts have been implemented in the existing constitution, better still there are elements of 'socialism ideals' in the current constitution that demand people are treated equally in politics and governments organs, therefore their problems lies with their representatives, with whom they are responsible for electing.

Sasa basi mtu unajiuliza hawa jamaa wa-muhimbili pengine na hospitali zingine za serikali zimeweka criteria ya malipo katika sehemu ya services zake, moja kwa moja unajua fees comes with a little bit more care from the service provider. On the other hand katiba inasema katika kutoa huduma za jamii kusiwe na criteria yoyote ambayo itamfanya mwengine abaguliwe katika kupata huduma yenye usawa kutoka kwenye vyombo vya serikali.

Hili ni tatizo kubwa sana kwenye jamii katika sector nyingi sana. Hivi ni nani alitakiwa kulisemea hili swala kama si vyama vya upinzani, taasisi huru za kusimamia haki za binadamu na raia wenyewe wenye kujua haki zao kisheria pengine na kuishitaki muhimbili kwa kuvunja sheria za haki ya mtanzania kwenye public services.

Kwa maana hiyo ule umma uliokwenda pale na kila siku ndio unaoumia na matatizo ya jamii, hivi katiba kweli ni matatizo yao au poor governance (simply ignorance from those people) and truth be said opposition parties are shying away from debates of those nature kwa sababu serikali inaweza kuja na changamoto za gharama na huwezo wake ndio maana imebidi kwenda na taratibu zingine na wao huwezo huo wa kuonyesha huwezakano bado hupo kwa kutumia facts za budget and running organisation at cheap all year long hawana, sana sana watasema kata posho and blah blah lakini kwenda na sera na kwa kuangalia gharama halisi za kuendesha mahospitali huwezo huo hawana. Kinachoendelea sasa ni ku-further their political ambitions hilihali matatizo yako palepale na hata wakishinda itabidi wayatatue kibaya ni pale ambapo hawayaongelei kwa jinsi watakavyo yamudu, ndio maana wengine wanaona hata kama CCM imeoza where is the realistic alternative.

Kweli ujinga wa mtanzania ndio mtaji wa wanasiasa kwa sasa.
 
MNH ni hospitali ya Taifa. Inaendeshwa kwa kodi za watanzania. Kuna mambo mengi ambayo si sahihi kufanyika katika hospitali hii. Naamini kabisa kuwa hakukuwa na haja ya kuwa na madaraja kama IPPM na kawaida. Pia ingewezekana huduma kutolewa bila malipo endapo kam referrals zingekuwa zinafanyika kama inavyotakiwa.
 
MNH ni hospitali ya Taifa. Inaendeshwa kwa kodi za watanzania. Kuna mambo mengi ambayo si sahihi kufanyika katika hospitali hii. Naamini kabisa kuwa hakukuwa na haja ya kuwa na madaraja kama IPPM na kawaida. Pia ingewezekana huduma kutolewa bila malipo endapo kam referrals zingekuwa zinafanyika kama inavyotakiwa.
Tatizo ni CCM imekuwa na utaratibu wa kuteua watu wasiokuwa na ufahamu wa sehemu wanazopewa na kuacha kufuata utaratibu wa sheria katika muonogozo wao hili waweze kuwa more creative ni common sense mtu mmoja awezi kujua direct problems of every sector, region and vast social problems so why should he be given the authority to select people everywhere. Huu utaratibu inabidi ubadilishwe na kuwe na mchakato mpya wa kutoa viongozi especially makatibu wa wizara.

Watanzania wakawaida ilitakiwa tuongelewe na wanasiasa wote wa upinzani na ambao wanaunda serikali kwa sasa, tatizo ni watanzania hao hao ndio wanachagua hawa watu kwenda kuwa represent, amini nikikwambia amna katiba ambayo inamlinda raia kama ya sasa kama matatizo yapo baasi ni kwenye taasisi ya uraisi.

Huko mbele watanzania ndio wanaenda kuondolewa haki zao zote kisa ushabiki waliouanzisha akina Mwanakijiji, bila ya kuwashauri watu jinsi gani taratibu za sasa ambazo jamaa wanafanya kinyume na mkataba wa uongozi kama katiba inavyo amuru na ni maswala ambayo yanaweza kuwa challenged at court au sheria inapotaka kupitishwa bungeni ambayo hipo kinyume na governance guidance wabunge wanatakiwa waikatae.
 
Back
Top Bottom