Gharama za matibabu Muhimbili zapanda maradufu

Gharama za matibabu Muhimbili zapanda maradufu

Dingswayo

JF-Expert Member
Joined
May 26, 2009
Posts
4,019
Reaction score
2,931
Gharama za huduma za kulipia matibabu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili zimepanda maradufu.
Hatua hiyo inayotekelezwa bila kuwashirikisha wadau na watoa huduma ilianza Septemba mosi mwaka huu na kulalamikiwa na wagonjwa na wafanyakazi.

Kwa mujibu wa tangazo la Mkurugenzi wa MNH, lililobandikwa kwenye ubao wa matangazo wa jengo la mateniti la kulipia huduma IPPM, inaonyesha kuwa gharama zilipanda kuanzia Septemba 2, wakati notisi hiyo iliyosainiwa na Mkurugenzi ilitolewa Septemba 4.

Wagonjwa wanaolipia matibabu binafsi Muhimbili waliliambia gazeti hili kuwa wateja wanaotumia ‘ast truck’ na huduma ya uzazi inayotolewa na kitengo cha mateniti- IPPM ndizo zilizoongezeka.

Kuanzia sasa upasuaji wazazi unalipiwa Sh. 500,000 badala ya 350,000 za awali. Uzazi wa kawaida ni Sh. 250,000 badala ya Sh. 150,000 zilizokuwa zikitozwa mwanzo.

Walisema kulala kunagharimu Sh. 20,000 badala ya 15,000 wakati tozo la kumuona daktari kwa mara ya kwanza ni Sh. 30,000 badala ya Sh. 20,000 za awali.

Kumuona daktari kwa ajili ya kufuatilia huduma na matibabu zimepanda hadi Sh. 20,000 kutoka Sh. 10,000.

Huduma nyingine kama dawa na uchunguzi wa maabara
zimepanda japo bei zake hazikutangazwa kwenye ubao wa matangazo.

Kwa wagonjwa wa kujifungua kawaida ambao hawalipii gharama watatozwa gharama ambazo hazikafafanuliwa ingawaje serikali inataka watibiwe bure.

“Mfano mjamzito akipata uchungu ghafla na kufika Muhimbili bila rufaa atatakiwa kalipia gharama” alisema mjamzito jina tunalo.

Msemaji wa MNH Aminieli Aligaesha, alikiri kuongezeka gharama hizo ziliongezeka na kuongeza kuwa sababu ya ongezeko hilo ni gharama kubwa za uendeshaji.

Hata hivyo alikataa kutoa maelezo zaidi na kutaka mwandishi wetu kwenda ofisini kwake kwa maelezo zaidi.

Hospitali ya Muhimbili inatoa huduma kwa utaratibu wa aina mbili kuchangia matibabu kunakofanywa na mgonjwa wa rufani pamoja na serikali.

Njia nyingine ni wagonjwa kulipia gharama zote za tiba kama ambavyo wanafanya kwenye hospitali za binafsi.

Hata hivyo gharama za tiba kwa wale wanaochangia matibabu na wale wa rufaa hazijaongezeka.

SOURCE: NIPASHE

  • Thanks
Reactions: BAK
Sasa naelewa kwa nini watu wanafia kwenye dispensary za mitaani. Hivi mwananchi wa kipato cha chini ataweza vipi kumudu ghrarama hizi za matibabu?
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Tufanye kazi kwa bidii. Tuache kukaa vijiweni na kupiga soga. Gharama za maisha zinazidi kupanda kila siku.
 
tukituma kufanya kazi kipato cha tifa kitaongezeka na gharama zitapungua huu utamaduni wa kulazimisha mandamano kila siku badala ya kazi ni hatari sana.
 
Tufanye kazi kwa bidii. Tuache kukaa vijiweni na kupiga soga. Gharama za maisha zinazidi kupanda kila siku.

Acha us...ng wewe hiyo sio sababu ya watu wenye kipato cha chini kufa, au mwanaCCM nini wewe?
 
Hizi gharama ni kubwa kwa kiasi fulani!

Toka 350,000 mpaka 500,000 Upasuaji. Angalau ingepanda mpaka 400,000 japokua bado ni kubwa pia!

Huyu anayepata dharura ya kujifungua bila rufaa wangemuweka kwenye kundi la wasiolipia ingependeza sana kuliko kumchaji!
 
Ni wazi kuwa gharama za maisha zinazidi kupanda kila siku. Hata hivyo gharama zipande kulingana na kipato cha wananchi na anayeweza kurekebisha hilo ni serikali. Pindi ikitokea kutokuwa na uwiano kati ya gharama na uwezo wa kulipia huduma, matokeo yake ni kupata jamii dhaifu iliyojawa na maradhi, vifo vingi ambavyo vingeweza kuzuilika na mwishowe jamii kukosa imani na serikali. Kutoa misemo myepesi kuwa gharama zinapanda kila siku ni kushindwa kuingalia hali hiyo kwa upana wake na madhara yake katika jamii na serikali iliyopo madarakani.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
wanasiasa wao wanajiweka katika mazingira mzuri ya maisha, wafanyabiashars kadhalika, serikali imesahau huduma muhimu, watendaji wa afya wakisema hali siyo shwari kwao n kwa jamii watu wanawabeza nakuwaona wabinafsi.

kila mtu anataka maaisha bora na unapobanwa wapaswa mbana unayemuweza so watendaji wa afya wamerudi kwa mwananchi wa kawaida wanakamua mpaka tone la mwisho, hospitali za binafsi nao watapandisha gharama.

mambo yatakwenda hivyo mpaka pale umma utakapochoka nakuamua kuchukua hatua ya makusudi kujirejeshea haki yetu!
 
Ni wazi kuwa gharama za maisha zinazidi kupanda kila siku. Hata hivyo gharama zipande kulingana na kipato cha wananchi na anayeweza kurekebisha hilo ni serikali. Pindi ikitokea kutokuwa na uwiano kati ya gharama na uwezo wa kulipia huduma, matokeo yake ni kupata jamii dhaifu iliyojawa na maradhi, vifo vingi ambavyo vingeweza kuzuilika na mwishowe jamii kukosa imani na serikali. Kutoa misemo myepesi kuwa gharama zinapanda kila siku ni kushindwa kuingalia hali hiyo kwa upana wake na madhara yake katika jamii na serikali iliyopo madarakani.
Hii ndio shida kwa maswali magumu kupewa majibu mepesi. Tumeona hata kabla gharama hizi hazijapanda bado mtz wa hali ya chini ambao ndio tuko wengi gharama za matibabu zilikua mtihani kwetu. Huko nyuma niliwahi tembelea ward Fulani na kukuta mgonjwa ameshindwa kulipia sh 3000 ya x-rays sasa leo hii gharama ndio hizoo zimezidi kupaa je tuta-survive kweli. Kila mara serikari yetu inalalama oooh haina pesa je hizi pesa zinazokwapuliwaga kila mara huwa zinatoka wapi. Kama hakuna pesa kwanini mshara wa mbunge uko juu kuliko wa muingia chumba cha upasuaji????Mimi nafikiri tunasumbuliwa na priority na lack of true love hasa hawa tuliowapa usukani wa kutuendesha.
 
Hizi gharama ni kubwa kwa kiasi fulani!

Toka 350,000 mpaka 500,000 Upasuaji. Angalau ingepanda mpaka 400,000 japokua bado ni kubwa pia!

Huyu anayepata dharura ya kujifungua bila rufaa wangemuweka kwenye kundi la wasiolipia ingependeza sana kuliko kumchaji!
Mkuu pale Muhimbili kama huna kitu panaudhi waweza jipotezea maisha hivi hivi unajiona. Wadau hebu fnyenyi kutembelea siku moja pale Muhimbili na muingie huko walikolazwa wagonjwa mjionee wenyewe. Mtu unaumwa na uko taabani unapewa panadol kisa huna hela ya vipimo sasa wanasubiria mpaka utakapopata fedha ya vipimo ndio mambo mengine yafuate. Bungeni tuliowaweka kila siku wanagombana nakutetea maslahi yao na si ya mtz. Hao tuliowapa migodi yetu hivi hatuwezi kuwalazimisha kutoa %%% Fulani kwa ajili ya hizi hospt ili gharama ziweze kuwa chini. tunaambiwa wanaenda nje ili kutuletea wawekezaji sasa hao wawekezaji wanatusaidia nini kama tunakufa kwa kushindwa kulipia matibabu yetu .
 
Kupanda kwa mishahara hakufanani kabisa na kupanda kwa gharama za maisha na hili ndilo linalowaumiza Watanzania wengi kila mwaka kwa kushindwa kugharamia gharama zao za kila siku ikiwemo matibabu. Unakuta katika mshahara wa mwezi mshahara huo unamudu gharama za wiki moja tu na wakati huo huo Wabunge na Mawaziri wakijiongezea mishahara na marupurupu makubwa kila mwaka.

Ni wazi kuwa gharama za maisha zinazidi kupanda kila siku. Hata hivyo gharama zipande kulingana na kipato cha wananchi na anayeweza kurekebisha hilo ni serikali. Pindi ikitokea kutokuwa na uwiano kati ya gharama na uwezo wa kulipia huduma, matokeo yake ni kupata jamii dhaifu iliyojawa na maradhi, vifo vingi ambavyo vingeweza kuzuilika na mwishowe jamii kukosa imani na serikali. Kutoa misemo myepesi kuwa gharama zinapanda kila siku ni kushindwa kuingalia hali hiyo kwa upana wake na madhara yake katika jamii na serikali iliyopo madarakani.
 
serikali sikivu at work!! maana leo hii mie hapa hata pamoja na kuwa na bima ya afya bado nasikilizia maumivu ya hizo gharama za matibabu kuwa juu kwa vile vipengele ambavo NHIF hawalipii sasa kwa mkulima wa Tumbaku huko Inyonga ambae hata bima haijui si ni majanga hayo.
kweli itafikia sehemu wananchi watawasha moto ambao kuzima kwake itakuwa ni miaka kadhaa!
kila siku ooh serikali haina pesa na upande mwingine watu wanakwapua mabilioni!!
halafu wakitoka hapo misamaha ya kodi isiyokuwa na tija kwa wananchi na matokeo yake ndio haya wananchi kubebeshwa mizigo mizito pasipo hata matumaini ya kutuliwa.
inauma sana
 
Muigeni Rostam Aziz aliwafunda wana Igunga kuwa na Bima za afya.
 
tukituma kufanya kazi kipato cha tifa kitaongezeka na gharama zitapungua huu utamaduni wa kulazimisha mandamano kila siku badala ya kazi ni hatari sana.

Peleka ujinga wako Lumumba
 
Nadhani serikali inawapigia debe waganga wa kienyeji nao wapate wateja,wale watakaoshindwa gharama za matibabu
 
Hiyo ni upande wa fast track. Kiukweli hakuna gharama ghali kama afya. India ni rahisi baaada ya kuwekeza muda mrefu na kwenye hii fani wakawa na madaktari wengi. Tatizo bima ya afya haipo vizuri na serikali sikivu iliamua kutoa misahama ya kodi kwa wawekezaji wakubwa na waendesha boda boda kwa lugha nyingne kutoa ruzuku huko badala ya hospitali kwa vile wagonjwa hawawezi kuandamana kama boda boda
 
Back
Top Bottom